Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi domoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi domoni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 31, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake.  Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe.


  Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka, kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele.  Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi.


  Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ' HATULIPI!, HATULIPI! '- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu. Na Hilo Ni Neno La Leo.  Maggid
  Iringa,
  Jumatatu, Januari 31, 2011
  mjengwa
   
 2. n

  ngoko JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dowans ni zaidi ya kuku bali ni EAGLE
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unasema Dowans tayari walishalipwa?

  kwamba kinachendelea ni sisi kuwabana warudishe hela zetu walizolipwa, na si kuzuia wasilipwe?

  duh, hili kweli neno la leo kutoka kwa mwana-ccm.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Maggid hakika neno la leo limetulia. Inakupasa kuwa umekulia katika mazingira yanayofugwa kuku, hasa wa kienyeji. Neno hili linanifundisha kuwa kama kuku huyu amezunguukwa na kuku wengine basi nao pia watakuwa wanamfukuza kuku (Dowans) ili kumnyang'anya panzi aliyemdomoni ama wamle wao au waambulie hata miguu kwa kumgawana. Katika kelele hizi tuhakikishe kuwa tunawaweka hadharani kuku wengine wote wanaokimbia na kuku(Dowans) kwa kumtetea kuwa alipwe alipwe alipwe nchi itakuwa katika hali mbaya kwani mali zitakamatwa, tufuate sheria tumwache kuku(Dowans) aingie vichakani na panzi wetu, wakati kundi la kuku wenza wakifuatia huko machakani kufuata mgao wao.

  Kwa kuanzia tu wale watendaji wa serikali wote waliotoa kauli za kumwacha kuku na panzi wetu, naona tuwapigie kelele ili waache kumfuata kuku (Dowans) na kutupa sisi unafuu wa kumpigia kelele na kumnyang'anya panzi wetu kabla hajammeza. HILI NDILO NENO LILILOTOKANA NA NENO LA LEO!

  HOFSTEDE
   
Loading...