Neno La Leo: Bundi Huanza Kuruka Jua Linapozama!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Bundi ana kawaida ya kuanza kuruka jua linapozama. Bundi haoni kwenye mwanga, ndio maana ya kulisubiri giza.

Nchi yetu imeingiwa na giza nene na bundi ameanza kuruka. Ngoja nikutafunie msomaji, giza hilo ni ufisadi uliotamalaki na hali ya kukosa maarifa. Ufisadi chanzo chake ni maradhi ya kuendekeza ubinafsi. Na kibaya zaidi, ubinafsi huo unapofanywa na viongozi.

Ndio, aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!

Waongozwa wengi wako gizani, lakini hata wale viongozi waliodhaniwa kuwa wako kwenye mwanga na wana uwezo wa kuwasaidia kuwatoa wananchi gizani, nao yaonekana ndio walio gizani na wanaochangia kutubakisha gizani .

Hakika, mambo mengine wayafanyao wanayafanya kama vile hawakusoma hata madarasa matano ya Shule ya Msingi, ni ya ajabu, ni mambo yanayofanywa au kusemwa na watu wajinga. Watu walio gizani.

Ndio, tatizo kubwa kwa baadhi ya hao viongozi ni kuendekeza ubinafsi na kupenda sana U-bwana Mkubwa. Ni ushamba fulani hivi. Na kwa hali ilivyo sasa, wananchi wameanza kuonyesha kuchoshwa na hali iliyopo inayosababishwa na baadhi ya viongozi wao. Wananchi hawa hawawezi kukaa kimya daima, ni mjinga tu atakayeamini kuwa jambo hilo linawezekana. Umma umeanza sasa kuamka na kusema, ‘ basi, inatosha’.

Maggid,
Iringa,
Jumatano, Septemba 28, 2011
http:://mjengwablog.com
 
Mwenyekiti nimekuapata,hawa jamaa 2015 watakuwa na hali mbaya sana kwa sbb zao la wanaolitegemea litakuwa limepungua sana,wazee,, 2015 usisahau wapiga kura wengi watakuwa vijana wa miaka ya 75 kuja juu hawa hawadanganyiki kabisa tuombe mungu atufikishe
 
Ndugu zangu,

Bundi ana kawaida ya kuanza kuruka jua linapozama. Bundi haoni kwenye mwanga, ndio maana ya kulisubiri giza.

Nchi yetu imeingiwa na giza nene na bundi ameanza kuruka. Ngoja nikutafunie msomaji, giza hilo ni ufisadi uliotamalaki na hali ya kukosa maarifa. Ufisadi chanzo chake ni maradhi ya kuendekeza ubinafsi. Na kibaya zaidi, ubinafsi huo unapofanywa na viongozi.

Ndio, aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!

Waongozwa wengi wako gizani, lakini hata wale viongozi waliodhaniwa kuwa wako kwenye mwanga na wana uwezo wa kuwasaidia kuwatoa wananchi gizani, nao yaonekana ndio walio gizani na wanaochangia kutubakisha gizani .

Hakika, mambo mengine wayafanyao wanayafanya kama vile hawakusoma hata madarasa matano ya Shule ya Msingi, ni ya ajabu, ni mambo yanayofanywa au kusemwa na watu wajinga. Watu walio gizani.

Ndio, tatizo kubwa kwa baadhi ya hao viongozi ni kuendekeza ubinafsi na kupenda sana U-bwana Mkubwa. Ni ushamba fulani hivi. Na kwa hali ilivyo sasa, wananchi wameanza kuonyesha kuchoshwa na hali iliyopo inayosababishwa na baadhi ya viongozi wao. Wananchi hawa hawawezi kukaa kimya daima, ni mjinga tu atakayeamini kuwa jambo hilo linawezekana. Umma umeanza sasa kuamka na kusema, ' basi, inatosha'.

Maggid,
Iringa,
Jumatano, Septemba 28, 2011
http:://mjengwablog.com
Utaambiwa wewe ni mchochezi usiyetaka amani itamalaki na nchi isitawalike.
 
Nakushangaa kwanini umechelewa kuliona hili....yaani unavuta shuka asubuhi, duh
 
Back
Top Bottom