Neno La Leo: Bundi Huanza Kuruka Jua Linapozama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Bundi Huanza Kuruka Jua Linapozama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Sep 28, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,
  Bundi ana kawaida ya kuanza kuruka jua linapozama. Bundi haoni kwenye mwanga, ndio maana ya kulisubiri giza.  Nchi yetu imeingiwa na giza nene na bundi ameanza kuruka. Ngoja nikutafunie msomaji, giza hilo ni ufisadi uliotamalaki na hali ya kukosa maarifa. Ufisadi chanzo chake ni maradhi ya kuendekeza ubinafsi. Na kibaya zaidi, ubinafsi huo unapofanywa na viongozi.


  Ndio, aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!


  Waongozwa wengi wako gizani, lakini hata wale viongozi waliodhaniwa kuwa wako kwenye mwanga na wana uwezo wa kuwasaidia kuwatoa wananchi gizani, nao yaonekana ndio walio gizani na wanaochangia kutubakisha gizani .


  Hakika, mambo mengine wayafanyao wanayafanya kama vile hawakusoma hata madarasa matano ya Shule ya Msingi, ni ya ajabu, ni mambo yanayofanywa au kusemwa na watu wajinga. Watu walio gizani.


  Ndio, tatizo kubwa kwa baadhi ya hao viongozi ni kuendekeza ubinafsi na kupenda sana U-bwana Mkubwa. Ni ushamba fulani hivi. Na kwa hali ilivyo sasa, wananchi wameanza kuonyesha kuchoshwa na hali iliyopo inayosababishwa na baadhi ya viongozi wao. Wananchi hawa hawawezi kukaa kimya daima, ni mjinga tu atakayeamini kuwa jambo hilo linawezekana. Umma umeanza sasa kuamka na kusema, ‘ basi, inatosha’.


  Maggid,
  Iringa,
  Jumatano, Septemba 28, 2011
  http:://mjengwablog.com
   
 2. KIDESELA

  KIDESELA Senior Member

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Mwenyekiti nimekuapata,hawa jamaa 2015 watakuwa na hali mbaya sana kwa sbb zao la wanaolitegemea litakuwa limepungua sana,wazee,, 2015 usisahau wapiga kura wengi watakuwa vijana wa miaka ya 75 kuja juu hawa hawadanganyiki kabisa tuombe mungu atufikishe
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Utaambiwa wewe ni mchochezi usiyetaka amani itamalaki na nchi isitawalike.
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Nakushangaa kwanini umechelewa kuliona hili....yaani unavuta shuka asubuhi, duh
   
Loading...