Neno La Leo: Akili Ya Kaa...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Ni kazi ngumu na ya hatari sana kujaribu kumkomboa mwanadamu aliyeridhika kubaki utumwani. Ni rahisi zaidi kumkomboa mwanadamu aliye utumwani na anayetamani kuwa huru. Hayo yalipata kusemwa na Mwanafalsafa, Nicollo Machiavelli.

Kaa ni aina ya samaki baharini. Kaa walio ndani ya kikapu huonyesha tabia ya ajabu sana. Pale kaa mmoja anapotaka kutambaa kutoka kikapuni, wenzake humvuta arudi kikapuni. Pwani ukiliacha kapu lako la kaa, unaweza kwenda zako na ukarudi. Utawakuta kaa wote wamo kapuni.

Kaa hawana ushirikiano, na ni wenye kuumizana wenyewe kwa wenyewe. Wenye akili za kaa utawakuta kwenye familia zetu na hata vyama vya siasa. Kimsingi, akili ya kaa ni kielelezo cha ujinga na ubinafsi uliokithiri.

Ni hatari zaidi pale nchi inapotaka kusonga mbele kutoka hali iliyopo, na inapojikuta, kuwa miongoni mwa Wana wa Nchi, kuna wachache walio na akili za kaa, na walio tayari kufanya lolote lile, alimradi nchi na watu wake wasisonge mbele.

Na unaanzia wapi kujaribu kuifanya kazi ngumu na ya hatari ya kuwakomboa wenye akili za kaa?

Ni Neno La leo.

Maggid Mjengwa,
 

Attachments

  • 8.jpg
    8.jpg
    98.2 KB · Views: 31
Back
Top Bottom