Neno la Jumapili: Usimkopehse ndugu au rafiki fedha

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Ikiwa ndugu yako au rafiki yako ambaye mna mahusiano ya karibu ana shida ya kifedha na wewe una uwezo wa kumpa fedha, usimkopeshe fedha, bali mpe msaada wa fedha aondoke kwenye tatizo hilo.

Kumkopesha ndugu au rafiki fedha, unakosa vitu viwili;

MOJA; Unakosa fedha ambazo umemkopesha.

MBILI; Unaharibu ule uhusiano ambao mlikuwa nao hapo awali.

Iko hivi ukishamkopesha mtu fedha, mahusiano mengine yote mliyokuwa nayo hapo awali yanabadilika na kinachozaliwa ni BWANA na MTUMWA. Imeandikwa kabisa ya kwamba mkopaji ni mtumwa kwa yule aliyemkopesha.

Sasa inapotokea rafiki au ndugu yako uliyemkopesha ameshindwa kulipa fedha ulizomkopesha, na mara nyingi hutokea, basi kinachofuata ni kuanza kukukwepa. Hivyo unazikosa fedha, na mahusiano nayo pia yanavurugika.

Ni bora kumpa kwa nia ya kusaidia, siyo kwa nia ya kudaiana hapo baadaye.

Kumbuka siyo mara zote na siyo kwa wote linatokea hili, lakini linatokea mara nyingi mno, na likitokea kwako, kama bado, litakuumiza sana.

Ni bora kinga kuliko tiba.

Usiseme hukuambiwa.

Nakutakia Jumapili njema rafiki yangu,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,
 
Mleta mada naona umechanga mambo hapa.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mkopo na Msaada.
Mkopo ni mkataba wa kibiashara, ila msaada ni hisani wa kijamii.

Mkopeshe mtu anayeweza kukulipa tu, Toa msaada kwa yule mwenye uhitaji tu na kama uwezo huo wa kusaidia unao na moyo wako unakusukuma kufanya hivyo.

Kusaidia ndugu, jamaa na marafiki ovyo ovyo, kunaweza kukufilisi mazima. Ni bora ukawakopesha tu ili kupunguza utegemezi, kujenga nidhamu ya Pesa lakini pia kusonga mbele kimaisha.

Siku zote Mkopo unaenda na nidhamu ya Matumizi, lakini msaada unaenda samba samba na kutumia ovyo ovyo.
 
Nakubaliana na wewe Mimi yamenikuta haya nilikopesha rafiki zangu kwa riba yanayonikuta najua mwenyewe
 
Hapo umenena. Nilimkopesha wife milioni tano alipe fees ya mtoto wetu chuo kikuu. Siku ya kumdai nilinyimwa haki yangu ya unyumba wiki mbili mfululizo
 
ni kweli tupu mi mwenyewe niliwahi kuwakopesha ndugu wanne kwa muda tofauti sijaambulia hata mia na ninavyoandika hapa kuna mwingine kaniomba nimwazime laki, hapa napiga mahesabu ya kumpa tuu. HAWA WATU HAWALIPI DENI
 
Mleta mada naona umechanga mambo hapa.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mkopo na Msaada.
Mkopo ni mkataba wa kibiashara, ila msaada ni hisani wa kijamii.

Mkopeshe mtu anayeweza kukulipa tu, Toa msaada kwa yule mwenye uhitaji tu na kama uwezo huo wa kusaidia unao na moyo wako unakusukuma kufanya hivyo.

Kusaidia ndugu, jamaa na marafiki ovyo ovyo, kunaweza kukufilisi mazima. Ni bora ukawakopesha tu ili kupunguza utegemezi, kujenga nidhamu ya Pesa lakini pia kusonga mbele kimaisha.

Siku zote Mkopo unaenda na nidhamu ya Matumizi, lakini msaada unaenda samba samba na kutumia ovyo ovyo.
Mleta mada naona umechanga mambo hapa.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mkopo na Msaada.
Mkopo ni mkataba wa kibiashara, ila msaada ni hisani wa kijamii.

Mkopeshe mtu anayeweza kukulipa tu, Toa msaada kwa yule mwenye uhitaji tu na kama uwezo huo wa kusaidia unao na moyo wako unakusukuma kufanya hivyo.

Kusaidia ndugu, jamaa na marafiki ovyo ovyo, kunaweza kukufilisi mazima. Ni bora ukawakopesha tu ili kupunguza utegemezi, kujenga nidhamu ya Pesa lakini pia kusonga mbele kimaisha.

Siku zote Mkopo unaenda na nidhamu ya Matumizi, lakini msaada unaenda samba samba na kutumia ovyo ovyo.
Mimi naona were ndiye unaechanganya, mfano: wewe una shida alafu ukaja kwangu, ukaomba nikupatie pesa kiasi cha shida yako kwa ahadi utarejeshe fedha hizo, Siku utakapo ipata, huo sio mkopo, biashara inaingiaje hapo.
 
Ikiwa ndugu yako au rafiki yako ambaye mna mahusiano ya karibu ana shida ya kifedha na wewe una uwezo wa kumpa fedha, usimkopeshe fedha, bali mpe msaada wa fedha aondoke kwenye tatizo hilo.

Kumkopesha ndugu au rafiki fedha, unakosa vitu viwili;

MOJA; Unakosa fedha ambazo umemkopesha.

MBILI; Unaharibu ule uhusiano ambao mlikuwa nao hapo awali.

Iko hivi ukishamkopesha mtu fedha, mahusiano mengine yote mliyokuwa nayo hapo awali yanabadilika na kinachozaliwa ni BWANA na MTUMWA. Imeandikwa kabisa ya kwamba mkopaji ni mtumwa kwa yule aliyemkopesha.

Sasa inapotokea rafiki au ndugu yako uliyemkopesha ameshindwa kulipa fedha ulizomkopesha, na mara nyingi hutokea, basi kinachofuata ni kuanza kukukwepa. Hivyo unazikosa fedha, na mahusiano nayo pia yanavurugika.

Ni bora kumpa kwa nia ya kusaidia, siyo kwa nia ya kudaiana hapo baadaye.

Kumbuka siyo mara zote na siyo kwa wote linatokea hili, lakini linatokea mara nyingi mno, na likitokea kwako, kama bado, litakuumiza sana.

Ni bora kinga kuliko tiba.

Usiseme hukuambiwa.

Nakutakia Jumapili njema rafiki yangu,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Karibu kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, tuma ujumbe kwa wasap wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwenda namba 0755 953 887 (wasap tu).
Yameshanikuta,uzuri ni kuwa siku nyingine akipata shida harudi na akiwa hana aibu akarudi simpi ng'ooo
 
Usinikumbushe machungu
 
Hapo umenena. Nilimkopesha wife milioni tano alipe fees ya mtoto wetu chuo kikuu. Siku ya kumdai nilinyimwa haki yangu ya unyumba wiki mbili mfululizo
Hii ya kumkopesha waifu kama ndo naisikia mara ya kwanza, looh..., mpaka waifu anakopeshwa na matumizi ni kumlipia mwanao karo.., halafu unadai.., bado sijaoa ila hii inafanya nisielele elewe the said context.
 
Nakubaliana na wewe Mimi yamenikuta haya nilikopesha rafiki zangu kwa riba yanayonikuta najua mwenyewe
Hakika yanaleta uchungu ,uadui na mwisho unakosa marafiki/ndugu kwa pesa na jasho lako mwenyewe
 
Hapo umenena. Nilimkopesha wife milioni tano alipe fees ya mtoto wetu chuo kikuu. Siku ya kumdai nilinyimwa haki yangu ya unyumba wiki mbili mfululizo
Hapo sijaelewa ada ya mtoto unamkopesha wife mkuu samahani lakini,nilijua ni wajibu wa baba na mama
 
Mm nilikopesha mtu kudai changu eti kaninunia chaaaah..kulipa kalipa ila kwa kumkaba haswa..sasa ananuna no salamu khaaaaurafiki wenyewe wa ukubwan .....nisidai changu kisa
Kudai muhimu bora kakulipa na anakumbuka umuhimu wako mengine mwachie Mungu atashughulika naye
 
Kuna jamaa yangu nilimkopesha laki tano na sabini mwaka Jana akafungie harusi mpk Leo ninapoongea hajanilipa hata shilingi mwaka Jana mwezi wa 12 nikamfwata mbeya toka dar nikalala kwake siku mbili niliambulia sound yani alivyokuwa mstaarabu siamini mpk sasa anakaa mbeya tukuyu kk karibu na bwalo LA magereza najua anasoma humu jf aibu na iwe juu yake mbaya zaidi ananiambia mbeya kuna ugonjwa wa nguruwe hivyo hawezi kunilipa maana nguruwe wake hawanunuliwi toka mwaka Jana mpk Leo na yeye na mke ni watumishi wa umma

Kiufupi namchukia mno ameharibu uhusiano wetu simtaki hata kidogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom