Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,781
- 3,074
Ikiwa ndugu yako au rafiki yako ambaye mna mahusiano ya karibu ana shida ya kifedha na wewe una uwezo wa kumpa fedha, usimkopeshe fedha, bali mpe msaada wa fedha aondoke kwenye tatizo hilo.
Kumkopesha ndugu au rafiki fedha, unakosa vitu viwili;
MOJA; Unakosa fedha ambazo umemkopesha.
MBILI; Unaharibu ule uhusiano ambao mlikuwa nao hapo awali.
Iko hivi ukishamkopesha mtu fedha, mahusiano mengine yote mliyokuwa nayo hapo awali yanabadilika na kinachozaliwa ni BWANA na MTUMWA. Imeandikwa kabisa ya kwamba mkopaji ni mtumwa kwa yule aliyemkopesha.
Sasa inapotokea rafiki au ndugu yako uliyemkopesha ameshindwa kulipa fedha ulizomkopesha, na mara nyingi hutokea, basi kinachofuata ni kuanza kukukwepa. Hivyo unazikosa fedha, na mahusiano nayo pia yanavurugika.
Ni bora kumpa kwa nia ya kusaidia, siyo kwa nia ya kudaiana hapo baadaye.
Kumbuka siyo mara zote na siyo kwa wote linatokea hili, lakini linatokea mara nyingi mno, na likitokea kwako, kama bado, litakuumiza sana.
Ni bora kinga kuliko tiba.
Usiseme hukuambiwa.
Nakutakia Jumapili njema rafiki yangu,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,