Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Angalia viganja vya mikono yako, je vina mistari? Na kama ipo, je, kuna mtu anayeweza kuifuta na kuiondosha?! Naamini jibu litakuwa ni hapana! Basi kama hakuna, tambua kuwa hakuna anayeweza kuzuia RIZIKI ZAKO NA REHMA za mungu juu yako.
ACHA kuwaza sana kuhusu maisha yako ipo siku utafanikiwa tu kwa kile unachokitarajia kama utafanya kazi kwa bidii na uaminifu bila kusahau kumuomba sana Mwenyezi Mungu.
Waliopewa na Mungu hakuwapa kwa ujanja wao au kwa kuwa wana akili sana kuliko wengine! Mungu aliamua tu kushusha rehma zake kwao kama jinsi anavyoweza kushusha rehma hizohizo kwako na wewe ukasahau maisha ya dhiki na mapito magumu.
Cha msingi tambua kuwa upendo na heshima kwa wakubwa na wadogo ndio tunu ya utu. Usimdharau mtu maana Mungu hana dharau juu yako. Sali sana kama vile utaondoka duniani dakika sifuri ijayo.
Mwenyezi Mungu atujalie tuwe watu wema tusio chukiana kwa rangi zetu au tofauti za imani zetu na itikadi zetu.
Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke na mbarikiwe hadi mpigwe na butwaa.