Neno la faraja kwa wanajamiiforums.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Angalia viganja vya mikono yako, je vina mistari? Na kama ipo, je, kuna mtu anayeweza kuifuta na kuiondosha?! Naamini jibu litakuwa ni hapana! Basi kama hakuna, tambua kuwa hakuna anayeweza kuzuia RIZIKI ZAKO NA REHMA za mungu juu yako.

ACHA kuwaza sana kuhusu maisha yako ipo siku utafanikiwa tu kwa kile unachokitarajia kama utafanya kazi kwa bidii na uaminifu bila kusahau kumuomba sana Mwenyezi Mungu.

Waliopewa na Mungu hakuwapa kwa ujanja wao au kwa kuwa wana akili sana kuliko wengine! Mungu aliamua tu kushusha rehma zake kwao kama jinsi anavyoweza kushusha rehma hizohizo kwako na wewe ukasahau maisha ya dhiki na mapito magumu.

Cha msingi tambua kuwa upendo na heshima kwa wakubwa na wadogo ndio tunu ya utu. Usimdharau mtu maana Mungu hana dharau juu yako. Sali sana kama vile utaondoka duniani dakika sifuri ijayo.

Mwenyezi Mungu atujalie tuwe watu wema tusio chukiana kwa rangi zetu au tofauti za imani zetu na itikadi zetu.

Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke na mbarikiwe hadi mpigwe na butwaa.
 
amen, Mungu wetu si mchoyo na wala si mwanadamu hata aseme uongo.

Barikiwa sana mkuu
 
amen, Mungu wetu si mchoyo na wala si mwanadamu hata aseme uongo.

Barikiwa sana mkuu

Nashukuru sana mkuu.
Ubarikiwe sana na wewe pia, na ikitokea umetangulia kubarikiwa wewe basi usinisahau kwenye ufalme wako. Ukitanguliziwa wewe unawavuta ulio waacha nyuma, tena hutakiwi kufanya hivyo kwa choyo au huku roho ikikuuma maana mwenyezi Mungu ana njia nyingi za kupitisha riziki za wengine, huenda riziki yangu akaamua kuipitishia mikononi mwako. Basi usiwe bahili au kuwa na roho ya konzi kutimiza mapenzi yake.

Njia yako iwe nyeupe mkuu na kama kuna miba zigeuke vumbi kabla hujapita.
 
amina.
asante sana kwa maombi yako, nawe pia Mungu akutane na haja ya moyo wako na akutumie msaada wake toka patakatifu pake.
 
Aamen. Na kweli imeandikwa, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu. Kumtegemea Mwenyezi Mungu ndo chanzo cha mafanikio. Na kufanya kazi kwa bidii, itatufikisha kwenye destiny yetu.

Asante kwa neno la faraja kaka. Haswa wakati huu wa mdororo wa uchumi binafsi na infalation isiyoelezeka.
 
Amen, nimeipenda

Mkuu.
Baraka na neema za mwenyezi Mungu zikushukie kama alivyo shusha kwa wengine. Unao tamani uwe na maisha kama yao wameyapata kwa kuwa Mwenyezi Mungu kaamua kunyoosha mkono wake, sio kwa sababu ya ujanja wao.

Usikate tamaa tutatoka maskini mwenzangu.
 
Angalia viganja vya mikono yako, je vina mistari? Na kama ipo, je, kuna mtu anayeweza kuifuta na kuiondosha?! Naamini jibu litakuwa ni hapana! Basi kama hakuna, tambua kuwa hakuna anayeweza kuzuia RIZIKI ZAKO NA REHMA za mungu juu yako.

ACHA kuwaza sana kuhusu maisha yako ipo siku utafanikiwa tu kwa kile unachokitarajia kama utafanya kazi kwa bidii na uaminifu bila kusahau kumuomba sana Mwenyezi Mungu.

Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke na mbarikiwe hadi mpigwe na butwaa.

Kweli mkuu umenena maana kama binadamu tunatakiwa tupunguze mawazo pia tunatakiwa tukubaliane na hali halisi ya maisha yetu ya kila siku (huu unakuwa ni mwanzo wa kuelekea mafanikio) alafu step ya pili ni kuchukua hatua kwa kufanya kazi kwa bidii ili kukabiliana na yote
 
Aamen. Na kweli imeandikwa, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu. Kumtegemea Mwenyezi Mungu ndo chanzo cha mafanikio. Na kufanya kazi kwa bidii, itatufikisha kwenye destiny yetu.

Asante kwa neno la faraja kaka. Haswa wakati huu wa mdororo wa uchumi binafsi na infalation isiyoelezeka.

Umenena kweli King'asti wangu.

Wanao tegemea binadamu wenzao ili wawatoe wanamkufuru Mungu. Mfuko wa ridhiki kaushika mwenyezi Mungu na yeye ndio anaamua ampe nani anapo toa mkono wake kutoka kwenye fuko hilo.

Tukijitahidi kujenga ukaribu na mwenyezi na kumuomba kwa maana ya kuomba, yeye ni msikivu na humpa yeyote anaye mtaka hata kama machoni kwa binadamu wenzie ataonekana ni nyang'au.

Ubarikiwe mpaka upigwe na butwaa hadi useme wewe Mungu wewe!
 
Last edited by a moderator:

Lilian Masilago naamini hujajaliwa roho ya kutu! Mwenyezi Mungu akikubariki usiwasahau yatima na wajane au wale wasio ijua aina ya chakula kitakacho ingia kinywani mwao.

Usisahau! Wewe si m-bora sana kuliko wengine wenye dhiki na njaa. Usikubali kumwaga chakula/vyakula wakati wengine wana lala na njaa.

Mshumaa wa mafanikio ukuwakie bila kuunguza roho yako nzuri.
 
Last edited by a moderator:
very pleasant wisdom .... upo makini sana mkuu

your wisdom is God's Grace (double G).... stay blessed ...
 
very pleasant wisdom .... upo makini sana mkuu

your wisdom is God's Grace (double G).... stay blessed ...

Mkuu mdizi.
Nashukuru sana! Uwe mshumaa wa matumaini wa kuwaonyesha mwanga wa matumaini wale wasio kuwa na tumaini, na uwe kamba ya kuwavuta wale walio oko kwenye mashimo ya wasio na tumaini ili uwavute waje wajiunge nawe kwenye uwanja wa matumaini kwa ajili ya mapigano mapya ya kuyamudu maisha.

Naamini wewe sio miongoni mwa wale wepesi wa kukata tamaa. Nakuombea maana kubarikiwa kwako kutapunguza mzigo kwa wenye uzito.

Ubarikiwe mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli mkuu umenena maana kama binadamu tunatakiwa tupunguze mawazo pia tunatakiwa tukubaliane na hali halisi ya maisha yetu ya kila siku (huu unakuwa ni mwanzo wa kuelekea mafanikio) alafu step ya pili ni kuchukua hatua kwa kufanya kazi kwa bidii ili kukabiliana na yote

Ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo na hatua unayofikia. Pia kukumbuka kwamba kila mwanadamu kajaliwa karama yake.
Ukifanya na kufahamu hilo, hakika mawazo yatapungua.

Siyo vibaya kuwa na wivu wa kimaendeleo, lakini wivu huo husikufanye ujione mnyonge na husiye bahati. La hasha. Bali ukufanye ufikie malengo yako kwa karama uliyojaliwa na Mungu.
 
Amina, Amin, amen mkuu Mohamed.....Ngoja nkalale sasa..

Mkuu tedo.
Ukalale kwa amani zote, usisahau kumuomba Mungu akuamshe salama huku akikujalia mema na mazuri, pia umuombe kama ataamua kukupenda zaidi basi akupe pumziko lililo jema na ulale kwa tabasamu lisilo kifani. Mwenyezi Mungu apushie mbali kama unaona ni mapema sana! Lakini kwa nini iwe mapema kwetu na iwe muafaka kwa kina nani? Inshaallah Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi yetu na akiamua hakuna anaye weza kumpinga.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom