Neno ‘KOLO’ hatarini kumponza Haji Manara, jela inanukia

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Kutokana na mwendelezo wa baadhi ya watu kutumia 'graphics' za Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) na kutumia kuweka maneno yao kisha kuandika maana potofu katika Lugha ya Kiswahili, baraza hilo limekuja juu.

Haji Manara ni mmoja wa watu maarufu ambao walitumia ufundi kama unaotumiwa na BAKITA kisha kuandika neno ambalo halijawahi kutumiwa na baraza hilo kisha kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram, leo Jumatano Februari 23, 2022.

BAKITA imeeleza kuwa sehemu ya adhabu ya atakayekutwa na hatia ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja.

Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Yanga aliweka graphics ambayo inafanana na ile ya BAKITA kisha kutumia jina la KOLO na kuweka maana yake kuwa: “Ni mtu anaeishabikia timu ya Simba.”


274377171_993103081293625_5482057531435977054_n.jpg


KOLOOO.JPG
 
Back
Top Bottom