Neno KAMBI RASMI lilikaziwa na Hamad Rashid kwenye kanuni za bunge

MushyNoel

Senior Member
Jan 13, 2011
104
9
Neno kambi rasmi liliwekwa ndani ya kanuni za sasa kwa shinikizo la Hamad rashid wakati wa kuunda kanuni hizi mpya za bunge.Alifanya hivyo ili kuzuia wenzake kutoka nje ya kambi rasmi kuongoza kamati hizi.

Taarifa zinasema Hamad litaka kuwekwa kwa kifungu hicho kwa kuwa aliamini kuwa chama chake ndicho kitaongoza upinzani bungeni kwa kuwa kina mtaji wa kutosha visiwani Pemba.

Kilichosababisha Hamad kushinikiza kuandikwa neno rasmi kulikuja kufuatia hatua ya mbunge wa Bariadi Mashariki,John Cheyo kumshinda Hamad mwaka 2005.Wakati CUF ilikuwa inaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni peke yake.Cheyo akaenda kugombea nafasi ya mwenyekiti PAC.Akamshinda Hamad ndani ya kamati.Sasa ilipoundwa kamati ya kanuni kuangalia kanuni mpya Hamad akasisitiza kuwekwa kwa neno rasmi.
 
Mchimba kisima kaingia mwenyewe
 
HR ana uchu wa madaraka, na hapo kakutana na kisiki cha mpingo.imekula kwakwe.
 
Mimi nawashangaa viongozi wanaopenda umimi sana kama hawa wa CUF, wamejivua magwanda ya mapambano dhidi ya dhuluma za za CCM kwa wananchi na kuanza mashambulizi dhidi ya CDM wamcontact Mrema sasa yuko wapi kisiasa je ndio malengo yake kuzeeka namna ile huku kila mtanzania akikuona kigeugeu?

Waache mzaha wasome alama za nyakati, CUF walikuwa na haki ya kuongoza Zenji toka 1995 wanalalama kivyao, na sulihisho ni kuanza kuishmbuli CDM watu wataanz kuwakimbiza majukwaani na kuwalazimisha msalimie ki CDM believe me.
 
Kama aliweka Hamad au si yeye kilichopo sasa ni sehemu ya kanuni. Si kwamba aliweka Hamad pia anaweza kuondoa, hapa tunaongelea suala la kanuni. CUF waendelee Znz huku bara wameshapoteza mwelekeo kama kaka zao wa CCM.
 
Nyundo aliyotumia kugongea ndiyo inayomgonga yeye sasa hivi - ama kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu...
Pole sana Mh. HR!
 
Back
Top Bottom