Neno jumapili:kila amwachaye mkewe na kuoa mwingine azini

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Habarini za jumapili wapendwa...kama wengine wote tukisubiri
kuelekea jumapili ni vyema tukawa tunakumbushana maneno ya MUNGU
kama inavyosema hapo juu hayo ni maandiko kutoka kwa mfalme bwana wa mabwana "KILA AMWACHAYE MKEWE NA KUOA MWINGINE AZINI""
Hata kama umezaa nae watoto 8 inasema waache nenda kwa mkeo wa ujanani...ondoka sasa anza kutii kauli ya mfalme....biblia inasema yoyote asietaka yesu amtawalehuyo ni adui mleteni mbele muwachinje mbele yangu....luk 19:29...je wewe ni mmoja watakaochinjwa???
Mungu ataubadilishe

1KOR 11:10
KWA HIYO IMEMPASA MWANAMKE AWE NA DALILI YA KUMILIKIWA KICHWANI KWA AJILI YA MALAIKA
I TIM 2:9--10

WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI...HAKUNA KUONYESHA MAPAJA..MAZIWA YAO...MIGONGOYAO..SI KWA KUSUKA NYWELE WALA KWA DHAHABU WALA KWA LULU BALI KWA MATENDO MEMA KAMA WANAWAKE WANAOUKIRI UCHA MUNGU

HHAYA WANANDUGU TUBADILIKE
 
Amwachae mkewe na kumwoa mwingine isipokuwa kwa habari ya uasherati ndie ananaezini!! Matayo 19:9 na yule atakaedhubutu kumwoa huyo mke aliye achwa atakua anazini pia. SENTESI HII INAWEZASOMEKA HIVI 'MTU ATAMWACHA MKEWE NA KUMWOA MWINGINE KWA SABABU YA UASHERATI. NA MWANAMKE ALIYEACHWA KWA SABABU YA UASHERATI HANA RUHUSA YA KUOLEWA.
 
Mkuu Mungu akubariki sana tena sana.
 
kuna kitu muhimu sana hapo huwa hakielezwi vizuri
ni hiki:

"alichokiunganisha Mungu"

maagizo yote yanayohusiana na kuachana yanahusu wale tu waliounganishwa na Mungu na sio kila wanaojiita wanandoa!

Angalizo:
ikiwa mtu haamini na anakubali kuishi na aliyeamini, huyo aliyeamini asimfukuze kwa vile tu mwenzake haamini.

natarajia siku za uoni kutunga kitabu juu ya mambo haya
 
Amwachae mkewe na kumwoa mwingine isipokuwa kwa habari ya uasherati ndie ananaezini!! Matayo 19:9 na yule atakaedhubutu kumwoa huyo mke aliye achwa atakua anazini pia. SENTESI HII INAWEZASOMEKA HIVI 'MTU ATAMWACHA MKEWE NA KUMWOA MWINGINE KWA SABABU YA UASHERATI. NA MWANAMKE ALIYEACHWA KWA SABABU YA UASHERATI HANA RUHUSA YA KUOLEWA.

Mpendwa, Mungu akubariki na akuzidishie.

Isipokuwa kwa mujibu wa "Wahubiri Waliobobea" katika neno Uasherati wa kumuacha Mke/Mume si ule wa kukutana kimwili kati ya mkeo/mumeo na asiyekuwa mkewe/mumewe bali ni KUABUDU MIUNGU MINGINE.

Mungu wa kuabudiwa pekee ni YEHOVA, Mungu wa Abraham, Isaac na Jacob. Mungu wa Musa, Mungu wa Daudi katika JINA LA YESU.
 
Back
Top Bottom