Neno gani la "kibongo" linakupiga chenga??

Ni vigumu sana kuratibu Kiswahili ukanda wote wa EAC, kwa mfano kule Pemba na hata Unguja nilkutana na misamiati ambayo sijaisikia Dar wala Nairobi, nikipata fursa nitaileta yote humu, halafu pia kuna kisiwa kinaitwa Tumbatu, huko tulienda na Watanzania wa kutokea Dar ambao waliishia kushangaa shangaa misamiati iliyokua inatumika, hao watu wa Tumbatu walikua kila wakiongea wenyewe kwa wenyewe tunaishia kutoelewa chochote japo wanazungumza Kiswahili.

Wao wanaita lahaja ya Kitumbatu, halafu wale hawaruhusu dada zao kuolewa nje ya hicho kisiwa. Na pia hawaruhusu mtu asiye wa asili ya pale kununua kiwanja humo hata kama una pesa ngapi, hamna klabu wala pombe inayoruhusiwa pale, na zaidi hairuhusiwi dini nyingine yoyote nje ya uislamu. Wao wapo na maisha yao wanavyotaka yaendeshwe japo wanajiita Wanzazibari au Watanzania lakini hawatengamani
Kila mgeni ukiingia hicho kisiwa lazima upokelewe na sheha yaani mkuu wa shehia, ifahamike ulichokusudia kufanya na kwa muda gani na utageuza saa ngapi na lazima iwe hiyo hiyo siku uliyofikia, maana hamna gesti, haziruhusiwi, pia hawaruhusu watalii, kilichotupeleka kule kilikua mradi wa asasi ya huduma za kijamii na tuligeuza jioni moja kwa moja.
Ewaaa! Lahaja ya Kitumbatu ni ya ajabu sana. Yaani unapotea kabisaaa. Mathalani:

Bamwanamke= baba mdogo, Ami
Bebeyu= Beberu
Bupuru= fuvu la kichwa
Buchari= kisu
Gubuya= sema ukweli
Ima= simama

Wana lahaja za ajabu hawa Wakitumbatu.

Kingine Kipepeo anayeruka ruka Wapemba wanamuita Kurukufu.
 
Kutokana na lugha kuzidi kukua na ndivyo misamiati inavyozidi kuongezeka, hivyo utajikuta kuna baadhi ya maneno huelewi kabisa japo yanatamkwa na wazungumzaji wa kiswahili, hii ni kwa wakenya je ni neno gani la "kibongo" unalisikia tu ama kwenye nyimbo au kuliona kwenye mitandao ila hulielewi? Post hapa wabongo wakufafanulie

Mimi kwa upande wa kenya, kuna baadhi ya maneno siyaelewi mf. Ngori, nduthi...yafafanueni tafadhali....

Sent using Jamii Forums mobile app
Nduthi = Bodaboda
Ngori = Noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ewaaa! Lahaja ya Kitumbatu ni ya ajabu sana. Yaani unapotea kabisaaa. Mathalani:

Bamwanamke= baba mdogo, Ami
Bebeyu= Beberu
Bupuru= fuvu la kichwa
Buchari= kisu
Gubuya= sema ukweli
Ima= simama

Wana lahaja za ajabu hawa Wakitumbatu.

Kingine Kipepeo anayeruka ruka Wapemba wanamuita Kurukufu.

Yaani shida, ukiwauliza wao wanajua wanazungumza Kiswahili.
 
Mk254 maana ya kulamba lolo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hatari sana, check hapa

0fgjhs56uf33cbq75.jpg
 
Back
Top Bottom