Neno gani la "kibongo" linakupiga chenga??

Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
2,667
5,243
Kutokana na lugha kuzidi kukua na ndivyo misamiati inavyozidi kuongezeka, hivyo utajikuta kuna baadhi ya maneno huelewi kabisa japo yanatamkwa na wazungumzaji wa kiswahili, hii ni kwa wakenya je ni neno gani la "kibongo" unalisikia tu ama kwenye nyimbo au kuliona kwenye mitandao ila hulielewi? Post hapa wabongo wakufafanulie

Mimi kwa upande wa kenya, kuna baadhi ya maneno siyaelewi mf. Ngori, nduthi...yafafanueni tafadhali....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chitola - chuma ulete

Matamba- ugali wa muhogo

Songola - bania chenji chenji baada ya kutumwa,au ombea kitu pate kwa bei ya chini alafu ile iliyobaki unaiweka takoni hiyo ndo tunaita songola.

Cheche- mwanaume anaekula wanaume au wanawake kwa njia ya miujiza,usiku au mchana.

Hizi ni terminologues za LINDI HUKO.
 
Duh huyu cheche ana undugu na popobawa nini?

Ngori = ndialala = lonzero = taabu = kali. Haya maneno hutumiwa Kenya jinsi Tanzania wanavyotumia neno shida ama sheeda.
 
Ni vigumu sana kuratibu Kiswahili ukanda wote wa EAC, kwa mfano kule Pemba na hata Unguja nilkutana na misamiati ambayo sijaisikia Dar wala Nairobi, nikipata fursa nitaileta yote humu, halafu pia kuna kisiwa kinaitwa Tumbatu, huko tulienda na Watanzania wa kutokea Dar ambao waliishia kushangaa shangaa misamiati iliyokua inatumika, hao watu wa Tumbatu walikua kila wakiongea wenyewe kwa wenyewe tunaishia kutoelewa chochote japo wanazungumza Kiswahili.

Wao wanaita lahaja ya Kitumbatu, halafu wale hawaruhusu dada zao kuolewa nje ya hicho kisiwa. Na pia hawaruhusu mtu asiye wa asili ya pale kununua kiwanja humo hata kama una pesa ngapi, hamna klabu wala pombe inayoruhusiwa pale, na zaidi hairuhusiwi dini nyingine yoyote nje ya uislamu. Wao wapo na maisha yao wanavyotaka yaendeshwe japo wanajiita Wanzazibari au Watanzania lakini hawatengamani
Kila mgeni ukiingia hicho kisiwa lazima upokelewe na sheha yaani mkuu wa shehia, ifahamike ulichokusudia kufanya na kwa muda gani na utageuza saa ngapi na lazima iwe hiyo hiyo siku uliyofikia, maana hamna gesti, haziruhusiwi, pia hawaruhusu watalii, kilichotupeleka kule kilikua mradi wa asasi ya huduma za kijamii na tuligeuza jioni moja kwa moja.
 
Ni vigumu sana kuratibu Kiswahili ukanda wote wa EAC, kwa mfano kule Pemba na hata Unguja nilkutana na misamiati ambayo sijaisikia Dar wala Nairobi, halafu pia kuna kisiwa kinaitwa Tumbatu, huko tulienda na Watanzania wa kutokea Dar ambao waliishia kushangaa shangaa misamiati iliyokua inatumika, hao watu wa Tumbatu walikua kila wakiongea wenyewe kwa wenyewe tunaishia kutoelewa chochote japo wanazungumza Kiswahili.

Wao wanaita lahaja ya Kitumbatu, halafu wale hawaruhusu dada zao kuolewa nje ya hicho kisiwa. Na pia hawaruhusu mtu asiye wa asili ya pale kununua kiwanja humo hata kama una pesa ngapi, hamna klabu wala pombe inayoruhusiwa pale, na zaidi hairuhusiwi dini nyingine yoyote nje ya uislamu. Wao wapo na maisha yao wanavyotaka yaendeshwe japo wanajiita Wanzazibari au Watanzania lakini hawatengamani
Kila mgeni ukiingia hicho kisiwa lazima upokelewe na sheha yaani mkuu wa shehia, ifahamike ulichokusudia kufanya na kwa muda gani na utageuza saa ngapi na lazima iwe hiyo hiyo siku uliyofikia, maana hamna gesti, haziruhusiwi, pia hawaruhusu watalii, kilichotupeleka kule kilikua mradi wa asasi ya huduma za kijamii na tuligeuza jioni moja kwa moja.
Lugha inatakiwa iwaunganishe watu lakini kwa EA ni tofauti.

Nilikua naangalia Churchill Show, kuna mwanamke hua kama mwalimu mara nyingi segment yake nilikua siwezi elewa kitu na nilikua na uhakika pale ni anazungumza kiswahili.
 
mimi hushangaa vile waBongo hutamka L karibu kama R
Matamshi huathiriwa na mahali mtu amezaliwa.

Mfano waPare wana shida katika utamkaji wa S hua wana kithembe (Lisp)

Hao wanaomix L na R waweza kuta ni wakurya.

Ni kama mHindi akiwa anatamka Kiswahili au Kiingereza
 
Chitola - chuma ulete

Matamba- ugali wa muhogo

Songola - bania chenji chenji baada ya kutumwa,au ombea kitu pate kwa bei ya chini alafu ile iliyobaki unaiweka takoni hiyo ndo tunaita songola.

Cheche- mwanaume anaekula wanaume au wanawake kwa njia ya miujiza,usiku au mchana.

Hizi ni terminologues za LINDI HUKO.
Chibudi chibude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lugha inatakiwa iwaunganishe watu lakini kwa EA ni tofauti.

Nilikua naangalia Churchill Show, kuna mwanamke hua kama mwalimu mara nyingi segment yake nilikua siwezi elewa kitu na nilikua na uhakika pale ni anazungumza kiswahili.

Natumai unazungumza kumhusu teacher Wanjiku, yule huigiza kwa kutumia lafudhi ya Kikikuyu, ikija kwenye uigizaji wa kutumia lafudhi, walengwa huwa sio watu wote, kwa mfano hata hapo Bongo kuna Bwakila na mkude simba ambao huigiza kwa lafudhi ya Kiluguru japo ukimkuta huyo huyo Kitare akiwa kitaa huzungumza Kiswahili lafudhi ya Dar kabisa.
 
Back
Top Bottom