Neno fupi la usiku; kuku unaowafuga mwenyewe wanapokukataa..!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
800px-Chicken_-_melbourne_show_2005.jpg
Ndugu zangu,
KUNA kisa cha bwana mfuga kuku aliyeshangazwa kwa kuku wake mwenyewe aliowafuga kumkataa. Alishangaa iweje kuku aliokuwa akiwapa pumba na mtama, wakala wakashiba, kisha waje wamwandame na hata kumparura.

Na mwanadamu unafanyaje unapofikwa na hali ya kuku wako unaowafuga mwenyewe kukukataa? Mwingine atajibu kwa haraka; " nitawachinja!"
Hilo ni jibu la mtu --------; maana mwanadamu hafugi kuku ili awachinje wote kwa siku moja. Mbali ya kitoweo, anahitaji kuku wamtagie mayai na wamtotolee vifaranga wapya; hivyo basi, wamuinulie kipato chake.
Mwanadamu afanye nini basi?
Ndio, kwa mwanadamu, ukiona hata kuku wako unaowafuga wanakukataa, basi, kaa chini utafakari kwa kina. Kuna tatizo. Na tatizo si kuku, ni lako mfuga kuku. Yumkini banda la kuku unaowafuga halina madirisha ya kuwapa hewa na mwanga. Na siku zote, kuku hawabanani ila ni mwenye kuku ndiye anayewabana kuku wake. Maana, hata kuku hufikwa na ukomo wa kustahimili kubanwa.
Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.(P.T)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom