Neno Fupi La Usiku Huu; Na Mukama Naye Ameusema Ukweli Wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno Fupi La Usiku Huu; Na Mukama Naye Ameusema Ukweli Wake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, May 31, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,  Vijana wengi leo wanaikimbia CCM na hawataki kuhusishwa nayo. Tujiulize; ni kwa namna gani vijana hawa watakuwa na mapenzi na chama kinachohusianishwa mara kwa mara, na kashfa kubwa za kifisadi. Kashfa zinazoathiri maisha yao? Kwao wao, wanayaona ‘madudu’ kwenye vazi la chama. Hatuyaoni?


  Ni sawa na kisa kile cha ‘ Mfalme aliyetembea uchi’. Watu wazima walijipanga barabarani kusifia vazi jipya la mfalme huku wakiifumbia macho kasoro kubwa ya vazi hilo, kuwa lilimwacha mfalme nusu uchi. Na hata pale mtoto alipotamka; “ Jamani, mfalme yuko uchi!” Kuna waliofunika nyuso zao kwa aibu. Maana, mtoto aliusema ukweli wake.


  Na leo nimesoma kwenye moja ya magazeti yetu; kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Wilson Mukama ameweka bayana, kuwa kuna Wana- CCM wasaka madaraka. Kwamba CCM ina makundi ; kuna Nato, G8 na kadhalika. Wilson Mukama ameusema ukweli wake.


  Na hakika, ukweli ni mzigo mzito. Mwanadamu hupaswi kuubeba na kutembea nao, bali kuutua na kila mmoja akauona. Naam, kuna wanaokimbilia CCM kusaka madaraka na si uongozi. Kiu ya madaraka ni kiu ya kutawala, wakati uongozi ni dhamana.


  Iweje basi Wana- CCM leo wakatumia muda na fedha kushiriki semina ya ‘ Utawala Bora’ badala ya ‘ Uongozi Bora’? Maana kazi ya chama cha siasa ni kuongoza, si kutawala. Hata Mwalimu alitumwambia, kuwa ili tuendelee tunahitaji mambo manne; Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora, si ’ utawala bora’, Au?


  Na hilo ni Neno Fupi la usiku huu.
  Maggid Mjengwa,
  Iringa
  [FONT=&quot]0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
  [/FONT]
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  pombe zinawasumbua, Mjengwa hawana lolote hawa nakumbuka sana enzi zangu hizo yaani unaweza kukataliwa siku kadhaaa kumbe kule kukataliwa kulikua kuna maanisha kukubaliwa, yaani hawa walikataaaa kabisa kuwa hakuna makundi na sasa wanakubali hadharani, mmmh ngoja nishushe net yangu (siyo ya msaada) nilale zangu
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Mjengwa Mkama na secretariati yake maji yamewafika shingoni.Mwenyekiti wao anakumbuka shuka asubuhi anasema wanasiasa wasibaguliwe na wakuu wa wilaya na mikoa nadhani kweli wanaona nyakati zao za kukaa Ikulu zimeisha
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kila wakigusacho na kukisema kinanajisika...they give foolish examples to polish the rotten party and very strong counter examples to sidprove their own lies... si walikuwa wanadai ku improve na kuwa kitu kimoja mbona yanazidi zaliwa makundi tena? Naona wana terminology mpya kuwa wana minyukano.Wanaponda chadema huku wamejisubscribe na wanajibainisha km CDM fans copy cats

  Cha kuchekesha wana ccm waliopo mbali na meza yakaramu wanapata matuamini sana na mijirangi ya Yanga ktk kanga, ktk t-shirts etc na porojo na akina Nape, plus ile imani kuwa CCM is immortal ndo inawafanya wanajisadikisha kiasi cha kupoteza muda kisafisha.

  Nakumbuka yule mlibya rafiki yangu aliyekuwa akipatakichefuchefu anapomwona Membe anapiga pose ktk TV halafu anatoa msimamo wa Tanzania na AU. Jamaa akasema kuwa membe anajiona kuwa yupo very presntable sana, na anawakilisha wajinga wa africa waliokuwa programmed kwa manuafaa wa eastern countries ,kwa sababu ya ujamaa. Mwisho AKANIAMBIA PIA KWA MBALI VITU VINGI VINAPENDEZA,ILA KWA KARIBU VINGI NI VIBAYA YANA. so walio mbali na CCM wapo busy doing something for the party.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Mjengwa Mkama na secretariati yake maji yamewafika shingoni.Mwenyekiti wao anakumbuka shuka asubuhi anasema wanasiasa wasibaguliwe na wakuu wa wilaya na mikoa nadhani kweli wanaona nyakati zao za kukaa Ikulu zimeisha
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Samtaims Mjengwa huandika vitu vya maana, ingawaje mara kadhaa huandika vitu vya kudakia dakia tu.
   
Loading...