Neno fasaha ni lipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno fasaha ni lipi?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Jibaba Bonge, Apr 30, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nimekua naona vyombo vya habari hasa magazeti wakitumia neno "Hairisha" likimaanisha (kwa kiingereza) postpone. Wataalamu wa kiswahili naomba mnisaidie neno fasaha ni Hairisha au Ahirisha?
  utakuta gazeti limeandikwa (kwa mfano) " mkutano umehairishwa". kwa jinsi ninavyo fahamu, ingekuwa " Mkutano Umeahirishwa". msaada tafadhali
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi si mtaalam wa kiswahili ila na mimi ninafahamu kama AHIRISHA
   
 3. MARIJANI

  MARIJANI Member

  #3
  Apr 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sina uhakika wa kutosha lakini nadhani neno sahihi ni "ahirisha" kama kuna wadadavuzi wa lugha nadhani watatuweka sawa maana naona kama bado tunaongea kwa kuhisia tuu.
   
 4. G

  GodHaveMercy Member

  #4
  May 2, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo neno fasaha ni 'AHIRISHA' na si 'HAIRISHA'. Media zetu siku hizi zinatupeleka chaka sana! For more information tembelea www.kamusiproject.org au books.google.co.tz... Nadhani hiyo itakuondolea utata, JB!
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Neno fasaha ni "Ahirisha" na si "Hairisha". Kuna watu wengi tu hata humu JF wana shida na matumizi ya "h". Pale ambapo inapaswa kuwepo wanaitoa, na pale ambapo haipaswi kuwepo wanaiweka. Ndipo unapokutana na madudu haya ya "hairisha".
   
 6. M

  Msavila JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  hii inatokana na lafudhi ya watu wakutoka mikoa fulani huweka h endapo a ni ya kwanza na wengine huifuta h k.m hamna huwa amna.
  sahihi ni ahirisha. Kinachokera unakuta huandikwa hivyo kwenye magazeti kama vile hakuna proof reader, labda tu awe na tatizo hilo. Tuenzi lugha yetu kwa kuandika kwa usanifu
   
 7. N

  Ngala Senior Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata neno budi. kianzio chake sahihi ni sina budi lakini wengi wetu hutamka nina budi.
   
 8. k

  klf Member

  #8
  Aug 6, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jibaba:
  Katika muktadha huu, hebu angalia makala ya Bwana Stephen Maina ambaye ni mpekuaji wa hali ya juu wa makosa, mategu na madudu ya Kiswahili! Maoni yake yanapatikana kwa kawaida kwenye gazeti la Mwananchi Tanzania.
  Mimi naendelea kupata elimu ya kuridhishsa sana nikisoma taarifa zake kuhusu namna watu mbalimbali wanavyotumia Kiswahili vibaya au kiuzembe.
  Anakaribisha mawasiliano. Yuko simuni: 716694240
   
 9. k

  klf Member

  #9
  Aug 6, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Marijani: Tafadhali nielezee jinsi ulivyoumba neno hili la "wadadavuzi". Linanipendeza lakini siwezi kulikubali bila ya maarifa mengine kuhusu hadhi yake ya neno jipya ... ? Asante.
   
 10. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ahirisha ndo sahihi
   
Loading...