Neno "Dengue" limedhihirisha kiwango cha kudorora kwa lugha yetu ya Taifa.

LazyDog

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
2,477
1,195
Nyenzo muhimu ya kujiendeleza kuifahamu lugha ni kwa kujisomea machapisho ya lugha husika.
Ugonjwa unaofahamika kwa jina la "dengue" kwa Kiingereza, waandishi wa magazeti yetu wameuitaje??!

Kwenye runinga nimesikia wakiuita dengu, mara denge, jana mtangazaji mwingine akauita dengi.
Nimejifunza kwamba neno "dengue" hapo juu hutamkwa [dengi] au [deng-gi].
Naanza kuamini kwamba matumizi ya neno dengu, denge au dengi sio sahihi kwa jinsi yalivyotumiwa hapo juu.

Kamusi zilizoko online zinaonesha kwamba "dengue" au "dengue fever", kwa Kiswahili ni kidinga au kidingapopo.
Mwenye ufahamu zaidi atuelimishe. Wajumbe wa TUKI mpo?
Hawa waandishi wetu, watangazaji na wahariri wa habari mbona wanasikitisha?

Neno gani lingine umesikia likitumiwa kuutaja ugonjwa huu? Changia tafadhali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom