SoC01 Nendeni mkajiajiri vijana ni kichaka kitumikacho kuficha udhaifu wa uwajibikaji wa viongozi wetu

Stories of Change - 2021 Competition

Yuco

New Member
Sep 10, 2021
2
5
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani.
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezimungu muumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

Naam nimeamua kuandika hili andiko ili tuweze kupeana maarifa mbali mbali katika jamii yetu tunayoishi.

Ajira, Ajira, Ajira hili ni neno lenye herufi chache tuu lakini linabeba maisha mazima ya mwanadamu hii Ajira imefanya watu kuheshimika na vile vile imefanya watu kudharaulika,Ajira imefanya watu kufurahia maisha na pia imefanya watu kulia hii Ajira imeleta matabaka ya walio na Ajira na wasio na Ajira .

Ajira huleta furaha katika maisha huo ndio ukweli ima I we Ajira rasmi ama isiyo rasmi ilimradi iwe Ajira tu inayosababisha kipato cha mtu ifikapo mwisho wa mwezi.

Kwa hakika Ajira imekuwa ngumu Sana kupatikana sio kwamba watu hawana elimu la hasha hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaohitimu mafunzo ya ngazi mbalimbali katika taaluma zao baada ya hapo wanarudi mitaani huku hawajui hatma zao wengine wamesomeshwa kwa fedha za serikali ambazo walitakiwa kuajiriwa ili kuweza kurudisha mikopo hiyo ili iweze kutumika na wanafunzi wengine lakini wapi !

Kutokana na ongezeko la wasio na Ajira basi limejitokeza kundi la watawala na kuanzisha wimbo unaosema VIJANA MJIAJIRi! kwa hakika huo ni wimbo tuu na nimwepesi kuuimba lakini ni vigumu kuutekeleza tena nivigumu kweli kweli ,lawama zimekuwa zikitoka kwa vijana kwenda kwa serikali na serikali kwenda kwa vijana je ni nani anepaswa kumlaumu mwenzake?

Jibu Vijana wanahaki ya kulaumu serikali na serikali wana haki ya kuwasikiliza vijana!Nini kinakushangaza kusikia jibu hilo,kwanini unahamaki namna hiyo ,mbona unanitolea macho,acha kukunja ndita kiongozi wangu nisikilize kijana wako.

Hizi hapa sababu za hilo jibu langu

1.Serikali ndio baba na ndio mama.
Nchi uongozwa na serikali na ndio mpanga na mtunga sera,mpitisha sheria na ndio mratibu wa shunguli zote za nchi! Kwanini asiulizwe?

2.Serikali ndio walatibu wa mitaala yote ya elimu na niwamiliki wa baadhi ya mashule na vyuo.

Serikali ilipaswa kuandaa mitaala ambayo inamuwezesha mwanafunzi kujiajili baada ya kuhitimu mafunzo je ni kweli mitaala hiyo ipo? Leo unamwambia muhitimu wa masomo ya ualimu wa shule ya msingi ajiajiri na wakati tution zimepigwa marufuku na huku wazazi wakiaminishwa elimu ni bure hii imekaaje?

3.Kufungwa kwa viwanda ama kufa kabisa .
Viwanda ambayo vilianzishwa kutoa ajira kwa vijana kufungwa na kutofanya kazi ambayo hupelekea wenye Ajira kukosa Ajira na wengine kutopata Ajira kwa Nini hukatae kulaumiwa?

4.Matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.
Maranyingi tumeona viongozi wakuu wa nchi wakilalamika juu ya matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwa kuwepo baadhi ya watu ambao sio waaminifu nani mwenyejukumu la kuwaondo hao ambao sio waaminifu yani mafisadi?Baba kwanini tusikulaumu?

5.Miundo mbinu mibovu .
Nani mwenyewe jukumu la kuweka iyo miundombinu imara ili iweze kuvutia wawekezaji wa sekta binafi ili iweze kutanua wigo wa Ajira.
Bilashaka huwezi kukataa lawama kiongozi.

Hizo ni baadhi tu ya sehemu ambazo wapaswa kujiuliza na kutupa majibu yake bila shaka idadi ya vijana inafahamika aidha kwa kupitia sensa ya taifa ata mashuleni pia kwanini kusibuniwe njia maalumu ya kuwasaidia hawa vijana mnaposema vijana wajiajiri sijui huwa ni kweli inatoka moyoni ama vipi? hivi mfano vijana wawe wanauza maji kwa mfano pale stendi ya mabasi mbezi wawe vija na miatano wawe wanauza maji hivi huo ushindani wa biashara wa bidhaa zinazofanana na bei moja sijui tija itapatikana wapi yani wauzaji ni wengi kuliko wanunuaji hapo kunakuwa hakuna Ajira bali Ni udhurulaji tuu.

Hao viongozi wanaotuambia tujiajiri watoto zao wote wapo katika Ajira rasmi kwanini wao wasiwe mfano leo tunaona baba kiongozi wa serikali na watoto wao na wake zao pia bila kusahau ndugu zao hivi huu ujasili wa kusema tujiajiri unatoka wapi?

Hao viongozi utakuta wanaweka fedha katika mabenki ya nje badala ya kuanzisha miladi mbali mabli hapa nchini ili iweze kuwapa fursa vijana.
Rushwa , viongozi wamekuwa mstari wa mbele kupokea rushwa na hata kudhuia kwa makusudi miladi mbalimbali hali ya kuwa kutaka rushwa ili kupitisha bila ya kutafakari anapozuia kwa makusudi miladi kunawatu watakosa Ajira.

Kiongozi anatakiwa kuwa na sifa tunawaomba wenyemamlaka wachagueni viongozi wenye sifa na si kwakujuana na anaefanya makosa kwa makusudi kutumbuliwa haitoshi bali afilisiwe mali zake na kufungwa pia ili iwefundisho kwa wengine

Vijana tuko tayari kujiajiri lakini tuwezesheni vitendea kazi basi.
Muda mwingine tunakaa vijiweni kwasababu hatuna pakwenda na kulala muda wote kunachosha na ili uweze kujiajiri lazima upate elimu ya hicho unachotaka kujiajiri ili ufanye kazi kwa ufanisi na hiyo elimu tutaipata wapi?
Maneno tupu hayatoshi fanyeni kwa vitendo viongozi

Itungwe sheria kwa kila kiongozi wa serikali hasa wa ngazi ya juu Ni lazima aanzishe mladi unaoweza kuajiri watanzania sichini ya watu 300 kutokana na fedha walizonazo na hata kukopeshwa na mabenki na ata wabunge nao wapewe majukumu hayo.

Wazawa wapewe fursa mbalimblai hasa katika madini na kwingeneko ili Ajira zipatikane.

Ushuru kandamizi uondolewe watu wafanye biashara.

Taasisi za fedha zije na mipango maalumu ni jinsigani wanaweza kutoa pesa Kama mitaji pasina kurudisha na riba .

Sekta ya viwanda na biashara ifanye kazi ya kuanzisha viwanda na biashara kweli na sio nadharia.

Vijana tuwe wasikivu na welevu pale tunapopewa mikakati yenye tija kwa taifa na panapotokea tofauti tuhoji kwanini.

Tuijenge nchi yetu,Tupende nchi yetu,tulinde Amani yetu,Tuwapende na tuwaamini viongozi wetu.

KAZI IENDELEE
 
Nakubaliana na wewe mkuu, viongozi wote wanaodai watu kujiajiri watoto wao wameajiriwa, leo tufanye kama Ridhiwan Kikwete auze maji stendi ya bus..lol
 
Back
Top Bottom