"...nendeni kwa wakubwa wenzenu, acheni wasichana wasome" jakaya kikwete/ccm 09/09/20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"...nendeni kwa wakubwa wenzenu, acheni wasichana wasome" jakaya kikwete/ccm 09/09/20

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Japhari Shabani (RIP), Sep 10, 2010.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "...NENDENI KWA WAKUBWA WENZENU, ACHENI WASICHANA WASOME" JAKAYA KIKWETE/CCM
  09/09/2010
  1 Comment(s)


  Jakaya Mrisho Kikwete /CCM akihutumia Muheza, Tanga
  Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, ambaye pia ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Kikwete, ameendelea kuvua wafuasi toka vyama shindani katika mikutano ya kampeni zake baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Muheza, Joseph Mnyema, kukitosa chama hicho na kujiunga na CCM.

  Mbele ya mamia ya wakazi wa Muheza katika mkutano wa kampeni wa CCM, Mnyema alisema amehama CHADEMA kwa kuwa kimekosa sera zenye mwelekeo.

  “Kukaa upinzani ni kupoteza muda, Chama chenye mwelekeo sahihi kwa maslahi ya Watanzania ni CCM,” alisema Mnyema aliyekabidhi kadi ya CHADEMA kwa Rais Kikwete.

  Akasema zaidi kuwa viongozi wa CHADEMA hawajali utu na kwamba wengi wako kwa maslahi binafsi na si kwa faida ya wananchi.

  Naye Raisi Kikwete alimfahamisha mwanachama huyo mpya kuwa mateso aliyoyapata akiwa CHADEMA hatayaona CCM kwani inajali na kuthamini kero za Watanzania. Akawaasa wananchi kuungana na Mnyema kutafuta kura za CCM kwani amejiunga kipindi muafaka, wakati CCM ikiwa kazini kutafuta ushindi kwa Urais, Ubunge na Udiwani.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwaonya wanaume wanaoshiriki mapenzi na wanafunzi kuacha kufanya hivyo kwani kunaongeza umasikini kwa wananchi kushindwa kupata elimu itakayowasaidia kupiga hatua kimaendeleo.

  “Nina taarifa kuna tatizo kubwa la mimba kwa wanafunzi. Naomba muache, nendeni kwa wakubwa wenzenu, acheni wasichana wasome. Hakuna maendeleo bila elimu na ukimuelimisha mwanamke umeelimisha taifa,” alisema Raisi Kikwete.

  credit: habari - Selina Wilson-Muheza/Uhuru na picha - Michuzi blog


  credit source: "...nendeni kwa wakubwa wenzenu, acheni wasichana wasome" Jakaya Kikwete/CCM - wavuti
   
 2. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hayo ni maneno ya mtu ambae tunategemea atuongoze!!!!!!!!!kawanza alisema wanafunzi kupata mimba ni kiherere chao sasa anakuja na hii.nilitegemea ya kwamba angelitoa kauli ya wahusika kuwapatia mimba wanafunzi kuchuliwa hatua kali kuanzia kwa katibu mkuu wa ccm makamba kama mfano anakuja na kauli za kejeri mungu ibariki tanzania.
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu huyu alisema kwamba wasichana/wanafunzi wanaopata mimba ni kwa sababu ya kiherehere chao.

  Juzi akiwa Mbeya katoa kauli nyingine fyongo, kwamba, anagawa vyandarua kwa kuwa malaria inazuwilika lakini ukimwi hauzuwiliki. Amesahau kwamba alishasema Tanzania bila UKIMWI inawezekana!

  Anaposema ukimwi hauzuwiliki anamaanisha nini haswa? So anaunga mkono ngono nzembe na kusambaza ukimwi?
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  You're forgetting that he is a sick President!! His oblongata goes off!
   
Loading...