Nenda Malinzi,pamoja na yote hili la under 17 na COSAFA umejitahidi

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,398
Habar wadau,katika uchaguz huu WA TFF ningetamani sana kuona Ally Mayai akipata nafasi ili tuone nini hawa watu wanaoitwa watu wa mpira watakifanya.

Huenda akawa na nafasi nzuri tu hasa baada ya Yale yaliyomtokea Jamal Malinzi aliyekuwa awe mtetez wa kiti hicho.

Mnyonge tumnyonge lakin haki yake tusimnyime,TFF ya Jamal Malinzi binafsi naipongeza kwa mambo mawili makubwa nayo ni

1. Hatua waliyofikia vijana wa under 17. Sote tulifurah kwa Hatua ya vijana wale kwenda kutuwakilisha Gabon ktk michuano Ile mikubwa Africa,kufika kwao pale hakukuwa kwa kubahatisha bali ni matokeo ya kuandaliwa na kuhudumiwa vyema na TFF,ni hatua ambayo hatujawahi kufika kwa vijana wa umri ule.

2. Hatua ya nusu fainali waliyofika Taifa Stars. Hatua hii waliyofika taifa stars huko Afrika kusini ilianza kuleta matumaini kwa watanzania kwamba huenda tukaanza kuwa na matabasamu ktk medani ya soka la kimataifa,hii pia haikutokea tu hewani bali ni kazi iliyofanywa na TFF.

Ndio maana nikasema pamoja na yote aliyokosea bwana Malinzi sitajisikia vizur nikiacha kumpa credit angalau kwa Yale aliyofanya vizuri. Karibuni wadau wenye nyongeza ya mazuri aliyofanya bwana Malinzi na wenzake ktk uongozi wake.
 
Hiyo ilikuwa kazi yake btw hivi zile hela walizochangiwa madogo Wa Serengeti boys zimeenda wapi maana madogo wanalia hasa yule captain wao... sio fair kabisa kula jasho la mtu
 
Hiyo ilikuwa kazi yake btw hivi zile hela walizochangiwa madogo Wa Serengeti boys zimeenda wapi maana madogo wanalia hasa yule captain wao... sio fair kabisa kula jasho la mtu
Ang'oke tu,hakuwa na lolote.
 
Back
Top Bottom