Nenda katika matawi haya ya CHADEMA kachukue kadi yako leo hii

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Inawezakana unatamani kuwa mwanachama wa CHADEMA lakini hujui mahala zilipo ofc. Kuna wana-JF wengi ambao wanatoka sehemu mbalimbali Tanzania bara na visiwani zilipo ofc za Chadema.Tafadhali toa taarifa muhimu zitakazomuwezesha mtu kufika eneo husika na akajichukulie kadi yake.Kwa mfano; Taja Jina la MKOA, WILAYA,MTAA and the nearest landmark.Asanteni.
 
Mi naanza na makao makuu ya CHADEMA yaliyoko Dar es salaam, wilaya ya kinondoni - mtaa wa ufipa jirani na kinondoni MANYANYA.
 
Nimeianzisha thread hii makusudi ili tuweze kufahamishana zilipo ofc za chadema.
Asanteni kwa muitikio wenu, mwenye kujua zilipo ofc za CHADEMA Kigoma, bagamoyo na Njombe kusini tafadhali aziweke hadharani ili members waende wakachukue kadi.
Asanteni
 
KWA KIGAMBONI ofc zinapatikana maeneo ya MAWENI kabla ya kufika mji mwema.
 
Makabila mengine tunaruhusiwa kujiunga? Eti kuna mtu alinidanganya kuwa CHADEMA ni taasisi ya wachaga.
 
Makabila mengine tunaruhusiwa kujiunga? Eti kuna mtu alinidanganya kuwa CHADEMA ni taasisi ya wachaga.
Sheria ya usajili hairuhusu chama chenye ukabila, ubaguzi wa rangi au udini kuendesha shughuli zake ndani ya Tanzania. Mwambie huyo mtu kama ana ushahidi wa alichokueleza apeleke kwa Tendwa na ikithibitika ni kweli basi CHADEMA kitasambaratika mara moja.
 
Makabila mengine tunaruhusiwa kujiunga? Eti kuna mtu alinidanganya kuwa CHADEMA ni taasisi ya wachaga.
Dr. Slaa sio mchaga,
Tundu lisu sion mchagga
Mr. Sugu sion mchagga
Vicent Nyerere sio mchagga
Mchungaji Msigwa sio mchagga
Wenje sio mchagga
....
....
Endelea mwenyewe maana nimechoka kuorodhesha. Ulikua huitaji mtu kukushawishi hivyo. Una macho ungeona, una masikio ungesikia sasa una macho soma.
 
Dr. Slaa sio mchaga,Tundu lisu sion mchaggaMr. Sugu sion mchaggaVicent Nyerere sio mchaggaMchungaji Msigwa sio mchaggaWenje sio mchagga........Endelea mwenyewe maana nimechoka kuorodhesha. Ulikua huitaji mtu kukushawishi hivyo. Una macho ungeona, una masikio ungesikia sasa una macho soma.
Lakini hao uliowataja wana nguvu ya maamuzi kwenye chama kweli? Mbona mwenye maamuzi anaonekana Mhe. Mbowe tu, tofauti na wenzenu wa CCM ambao wanaonekana wanatoa uhuru mkubwa sana kwa wanachama wao.
 
Lakini hao uliowataja wana nguvu ya maamuzi kwenye chama kweli? Mbona mwenye maamuzi anaonekana Mhe. Mbowe tu, tofauti na wenzenu wa CCM ambao wanaonekana wanatoa uhuru mkubwa sana kwa wanachama wao.

Ni kweli CCM haina kiongozi madhubuti ndiyo maana mmoja ni boss, nna matokeo yake chama kinaenda alijojo. CDM kina viongozi madhubuti na ndiyo kiko byee
 
Taasisi ya wachagga!
Zitto ni mchagga
Shibuda pia mchagga
..
..
..
Hayo ni yale makubwakubwa.List ni ndefu saana ila nawashangaa hawa wasomi wasiojua/weza kutafakari malisho walishwayo hata wakameza uchafu!
 
London - United Kingdom ofisi ziko wapi?. Kuna wapenzi wengi sana wanataka kujiunga na Chadema.
 
Back
Top Bottom