Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
Gavana profesa Florence Luoga amemaliza muda wake kwa mujibu wa sheria za utumishi pale benki kuu, lakini jina lake litapakwa wino wa dhahabu kwa utumishi wake uliotukuka. Ni katika kipindi cha Gavana Luoga sheria za fedha na uchumi wa Tanzania vilisimamiwa kwelikweli kwa vitendo na siyo kwa maneno na kupelekea Tanzania kuingia uchumi wa kati mapema zaidi mwaka 2020 kuliko ilivyokuwa imetabiriwa na mabeberu kuwa Tanzania itaingia uchumi wa kati 2025.
Wazalendo wa nchi yetu ya Tanzania tunaamini bila uthubutu na ujasiri wako Prof Luoga isingewezekana kupata hayo mafanikio ndani ya muda mfupi hivyo.
Wazalendo wa nchi yetu ya Tanzania tunaamini bila uthubutu na ujasiri wako Prof Luoga isingewezekana kupata hayo mafanikio ndani ya muda mfupi hivyo.