NEMC yaitoza Lake Oil faini ya bilioni 3.3 kwa kutozingatia utunzaji wa mazingira

Tanzania nchi ya ajabu sana yaani vituo vyote hivyo vinajengwa maana sio kituo ni vituo vinapata lincence ya biashara watu wa jiji au halmashauri wakagua vibali wanapita tu kimyaa leo wanaamka usingizini nani kajenga hivi bila vibali maana kama lingekuwa kuna kosa kubwa vingebomolewa lakini kupiga fine biashara iendelee ni kama kusema vibali vile sio muhimu ila ni vizuri kuwa navyo tu kuongeza ukiritimba. Hapa siwatetei Lake Oil lakini kuna watu walijenga sehemu sio wanawekewa red bomoa sasa na hawa wangewekewa bomoa maana sheria zimekiukwa au vibali hivi havina umuhimu wowote.
 
Wanabodi kuna hii Taarifa nimeiona Kwenye media zingine ikisema Shirika la Mazingira Nchini NEMC Limeitoza Kampuni ya Lake Oil Fine ya Tsh Bil 3.3 kwa kujenga vituo vingi sehemu tofauti za Nchi bila Kibali.

Hili limekua kama mshituko hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba suala la mipango miji nchini hapa sio kipaumbele. Au Wengi wetu hatuzingatii.

Ni vyema kutimiza wajibu kuepuka matatizo makubwa kama haya. Bil 3 naamini ni hela nyingi sana kwa kampuni yeyote.
Kutii sheria na kufuata taratibu ni jambo la msingi sana.

=====

NEMC iimeagiza kampuni ya mafuta ya Lake Oil kulipa faini hiyo ndani ya siku 14 la sivyo itaamuru kufungwa kwa vituo vyake vya mafuta 66 kote nchini, ikitoa mfano wa vifungu vya sheria vinavyohusika. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt Samuel Gwamaka aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa baraza hilo lilifikia uamuzi huo kufuatia malalamiko mengi ya umma katika maeneo ambayo vituo vya mafuta vilijengwa.

"Tunaendelea na uchunguzi kwa wamiliki wengine wa vituo vya mafuta na wale watakaobainika wamejenga vituo vya mafuta bila vyeti vya EIA watatozwa faini. Hiyo ni kwa mujibu wa sheria, kwani tumegundua kuwa vituo vya mafuta vimekuwa vikiongezeka kila mahali. Hatuwezi kuendelea kuwakumbusha wamiliki wake juu ya majukumu yao kwani tumeshafanya mengi tayari, ”alisema.

Alitoa siku saba kwa wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyojengwa bila vyeti vya EIA kuripoti kwa ofisi za NEMC kuelezea ni kwanini hatua hazipaswi kuchukuliwa dhidi yao. Ni miaka 17 tangu sheria ya sasa ya mazingira itungwe na NEMC imekuwa ikitoa elimu kwa njia anuwai. Lakini wamiliki wengi wa vituo vya mafuta walipuuza maagizo haya, kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua umewadia, alisema zaidi.

"Kuna vituo vya mafuta karibu 3,000 kote nchini lakini ni 600 tu ndio wameandikisha tathmini ya athari za mazingira. Kujenga vituo vya mafuta bila EIA ni hatari kwa watu katika eneo hilo ikiwa kuna dharura, kwa hivyo hatuwezi kuvumilia hii tena, ”alisisitiza. "Kila mtu anaona jinsi vituo vya mafuta vinavyoenea kila mahali, na NEMC imekuwa ikijiuliza ni kwanini wamiliki hawaripoti katika ofisi za NEMC kujiandikisha na kupata EIA,". mkurugenzi alibaini.

Alisema kanuni zinahitaji kwamba umbali kati ya kituo kimoja cha mafuta na kingine haipaswi kuwa chini ya mita 200 ili kuepuka dharura za moto, lakini wajenzi wa kituo cha mafuta wamekuwa hawazingatii mahitaji haya, alisema. Wamiliki wengi wa vituo vya mafuta huunda vituo vyao na kisha hutafuta vyeti vya EIA, na mara nyingi akitaka kuhonga maafisa wanaohusika, alishtaki, akibainisha pia kwamba watu wanaoishi karibu na mahali kituo cha mafuta kina haki ya kushiriki katika kukuza ufahamu juu ya nini cha kufanya ikiwa kuna dharura ya moto .. Kuhitaji wakaazi wa thst kuhusika wakati wa kutoa vibali vya EIA inakusudiwa kuwawezesha kujua juu ya hatari za kiafya wanazopaswa kuishi nazo, ameongeza.
Kama kile cha pale Buguruni sokoni, watu kibao siku pakitokea moto au mlipuko sijui itakuwaje.
 
Hiyo faini ya bilioni 3 ni nyingi sana.
Kuna kampuni moja ya mafuta (sio giant sana) tulifanya nao kazi fulani, tukawataka walete bank statement ya miezi mitatu.
Gross total ya miezi mitatu haikufika bilioni 8.
Sasa unapompiga faini ya bilini 3, hiyo ni faida ya miezi mingapi?
 
Kibali cha kujenga na EIA report ni vitu viwili tofauti

Tambua EIA ina kagua athari za maradi husika ktk mazingira sasa mbali na EIA kuna ukaguzi mwingine hufanyika baada ya mradi kuamza kazi kwa kipindi fulani endapo ikionekana una viashiria vya uchafuzi wa mazingira kwa kimombo wanasema Environmental audit (EA)

Sasa ikibainika mradi unachafua mazingira hapo lazima ulipe faini ya fedha

EIA hufanyika kabla ya mradi kuanza
Mkuu wewe ni mtaalamu elekezi wa mazingira ?
 
Lake oil ilikua above the law awamu zilizoita.
Mnakumbuka kisa Cha yule mhasibu mhindi waliyemla tiGO na kumpinga sana. Alishtaki kila mahali lkn alikua anaoneka Kama bwabwa Fulani mhindilicious
 
UCHELEWESHAJI MUDA MWINGINE UNACHANGIA NDIO MAANA RAISI WA AWAMU YA 5 ALIKUWA ANAHIMIZA WATU WAJENGE HUKU WANAFATILIA TARATIBU ZINGINE KUTOKANA NA UCHELEWESHAJI
 
Nawajua vituo vyao havijaenea sana wako bunju na morogoro road pia kuna maeneo wana vituo vyao!
Saa hizi wanamalizia kituo chao masasi, kama kawaida kimependeza na kitaamsha muonekano wa mji huo ,at least watapata supermarket
 
Back
Top Bottom