NEMC: Vifungashio vya plastiki ikiwemo chupa za maji mwisho wa kutumika ni Desemba 31

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa hadi Disemba 31, mwaka huu kuwa ni siku ya mwisho ya utumiaji wa vifungashio vya chupa za maji, karanga au ubuyu, biashara inayofanywa na wachuuzi wadogo.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka, alisema hivi karibuni limekuwako ongezeko la uzalishaji wa vifungashio vya plastiki ambavyo chanzo chake hakijulikani na ni vifungashio ambavyo havina kibali cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alisema utengenezaji, usambazaji na matumizi ya vitu hivyo ni uvunjaji wa Kanuni Na 3 na 4 za Sheria ya Mazingira ya 2004, kanuni ambazo zilitungwa na kutangazwa 2019 ili kutekeleza katazo la serikali la matumizi ya plastiki.

Kanuni namba 3 inawataka wazalishaji kuwa na kibali kutoka TBS baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa, lakini hali haiko hivyo kwa sasa,” alisema Dk Gwamaka, na kuongeza kwamba kuwapo kwa vifungashio hivyo sokoni ni kinyume cha kanuni ya 4 (b) na (c) ambayo imetungwa na kutangazwa ili kulinda afya ya binadamu, wanyama pamoja na mazingira dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa kanuni za upigaji marufuku mifuko ya plastiki, ni marufuku kutengeneza, kuuza, kusafirisha ndani na nje ya nchi, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, baraza lazima lisimamie sheria na kuzuia matumizi ya bidhaa zisizoruhusiwa kisheria, alisema Dk. Gwamaka.

Chanzo: Ippmedia
 
Kiukweli hawakupaswa kufungia hii biashara za vifunganisho, kwani wengi wanaozifanya ni wafanyabiashara wa kipato cha chini, walitakiwa kutoa elimu zaidi kwa wanunuzi pamoja na watumiaji juu ya namna ya kudumisha usafi wa mazingira pamoja na kudhibiti kuenea kwa takataka zinazotokana na vifungashio hivyo....Aisee!!
 
Back
Top Bottom