MWananyati
Senior Member
- Feb 3, 2011
- 160
- 53
NEMC, ambao ni wasimamizi wakuu wa mazingira ya nchini wamekuwa na tabia, naweza kusema, ya kujisahau au kutusahaulisha sisi wananchi juu ya wajibu wao. Kazi zao nyingi zimekuwa ni za kimatukio na za msimu kwa kuangalia upepo kipindi hiko umevuma kuelekea wapi.
Nakumbuka mwaka juzi (2015 Nov/Dec) wakati Serikali yetu ya Hapa Kazi ilipoingia madarakani na kuona kuwa ni Serikali ya kasi sana, Mkuu wa NEMC alijitokeza katika vyombo vya habari na kututamkia kuwa Suala la Uchafuzi wa Mazingira kwa njia ya kelele, hasaaa kutoka katika baa, kumbi za starehe na makanisani nyakati za usiku ni kosa kisheria. Na yeyote ambaye anahitaji kufanya "kelele" hizo anatakiwa kupata kibali Baraza. Bila hivyo mtu/taasisi/kampuni hio itakuwa imevunja sheria na hivyo kustahili adhabu. Nafahamu kuwa Sheria itakuwa imeweka kwa undani kelele za ukubwa gani hazitakiwi na pia adhabu stahiki kwa wakosaji. Nakumbuka pia hii kero ya kelele toka katika nyumba za ibada liliwahi kuongelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Makonda.
Sasa basi, ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kutolewa kwa "tamko", utekelezaji wake nafikiri umebaki palepale Mkuu wa NEMC alipomaliza kuongea na vyombo vya habari. Kelele zinaendelea mtindo mmoja kupita ule muda ambao NEMC waliainisha (wakizingatia afya na ustawi wa watu wanaoishi karibu na maeneo hayo). Mikesha makanisani tena kwa kupiga miziki (kutumia vyombo vya muziki) kwa sauti ya juu (nikiamini usiku wa saa sita Upendo Nkone na bendi yake hawezi kuwa anaimba muda huo) limekuwa suala la kawaida hasa siku za Ijumaa. Hakuna utii wa Sheria. Hakuna Usimamizi wa Sheria. Serikali za Mitaa ndio zimelala kabisa maana viongozi wake hawana msaada katika haya matatizo kwa kisingizio cha kuingilia uhuru wa kuabudu (kuabudu? saa 6 usiku? bull shit!). Lakini nilichokibaini ni kuwa hawa viongozi wa serikali za mitaa kuanzia M.kiti na Wajumbe wa nyumba kumi, wapo kwa ajili ya kuangalia nani atamwezesha ndo hukumu yake ilalie huko. Kesho ijumaa, tembelee popote pale kwenye makanisa ya wokovu mtaona raia wanavopata tabu usiku kulala.
Pili, Nakumbuka Mwaka 2016 mwezi wa 8, Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa tangazo linalozuia uzalishaji, uingizaji, uuzaji na matumizi ya mifuko yote ya plastiki - TOTAL BAN (sikumbuki ilikuwa GN Namba ngapi, ila ilitoka wiki ya pili ya Ogasti). Nimekuwa nafatilia kuhusu hii kitu maana kimsingi hakuna asiyefahamu madhara mabaya yanayosababishwa na bidhaa hizi za mifuko ya plastiki kuanzia katika mazingira, wanyama na binadamu (hasa akina mama wajawazito). Leo hii ikiwa ni tarehe 19 Januari, sijaona popote pale ambapo NEMC au OMR (Mazingira) wameanza utekelezaji wa sheria(?) ile.
Niwaulize NEMC na OMR-Mazingira, hivi mna mipango katika utendaji wa kazi zenu au ndo masuala ya kukurupuka na kucheza na midundo ya DJ ili kuonesha kuwa mpo mnafanya kazi? tumechoka matamko yenu... utendaji sifuri kabisa. Je, mlitoa matamko hayo kwa ajili ya kutafuta "kick" kwa Mkuu wa Nchi? mnamuangusha sana Mkuu wetu maana kila nyezo ya kufanya utekelezaji mnayo ila kwa kuwa hamna utashi wa kisiasa kukomesha vitendo viovu kwa kufanya usimamizi unaopaswa wa Sheria, ndio mnakaa na kufikiria kutoa tu matamko kila mara. Tunahitaji mtoke msimamie sheria. Mbona Jeshi la Usalama Barabarani wameweza kuhusu Sport lights na Tinted windows? nyie kwanini mpo kama hampo?
Yaani kero za mazingira ni nyingi sanaa.... hamzioni au ndo mko bize kufatilia viwanda? migodi?
Mnatuchosha, mnafanya hadi nyie kudharaulika. Acheni kelele, simamieni sheria. Mkurugenzi Mkuu NEMC na Mkurugenzi wa Mazingira (OMR) jiangalieni sana na matamko yenu ambayo hamna nia ya dhati ya kuyatekeleza. Na Mh Makonda, hebu tia moto katika haya maana wewe ukisimamia kitu (baadhi) utekelezaji unafanyika na kufanikiwa.
Sasa tunaelekea kwenye masika.... wale watu wa paleeee mabondeni hamjawatoa tu. Subirini kitakachowapata kama mtakuwa na uwezo wa kukabiliana nacho.
Cheers.