NEMC na urafiki na wachafuzi wa mazingira

ONDIECK OTOYO

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
254
44
KAMATI YA MGOGORO WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA ‘ KATIKA KIJIJI CHA KISEMVULE . P.O. Box 10 MKURANGA PWANI
Tarehe 18/03/2014
Kumb: KMU/KKM/MZ/III/3/2014
Kwa KATIBU MKUU Ofisi ya Makamu wa Rais P.O. Box 5380 DAR ES SALAAM Simu:+255 22 2116995
Kk. Katibu wa Baraza la Ardhi Kijiji cha Kisemvule P. O. Box 10 Mkuranga -Pwani
katibu:
YAH: UKIUKWAJI WA MAKUSUDI WA SHERIA YA MAZINGIRA NO. 20 ya 2007 Environmental Health Practitioner (Registration) act, PAMOJA NA SHERIA YA VIWANDA NO. 10 ya 1967 The National Industries(Licensing and Registration) act, JAMBO LINAYOTEKELEZWA NA KIWANDA CHA CEMENTI CHA MAWENI LIME STONE (ARM CEMENT) HIKIWA VIONGOZI HUSIKA WAKISHINDWA KUCHUKUA HATUA PAMOJA NA WANANCHI KUWAFIKISHIA MALALAMIKO, JUU YA UCHAFUZI HUO HUKU WAKIJENGA MAZINGIRA YA USWAHIBA NA WENYE KIWANDA BILA KUSIMAMIA SHERIA YA MAZINGIRA, NA KUSHINDWA KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YA KIWANDA
Katibu Mkuu husika na somo hilo hapo juu,
Kwa mujibu wa sheria ya mazingira namba 20 ya 2007, tunalazimika kuleta mgogoro huu wa kuathiriwa na uchafuzi wa mazingira inayotekelezwa na kiwanda cha cement cha maweni lime stone(ARM CEMENT) kwako ili atua za kisheria ziweze kuchuliwa na kudhibiti uchafuzi huona tupate kuishi bila madhara ya kiafya kama ilivyo kwa sasa.
Katibu Mkuu katika madhara hayo ya uchafuzi wa mazingira tupo wananchi kaya 18 tunao athirika na uchafuzi huo. Na tumejaribu kupeleka malalamiko yetu katika ngazi zote husika lakini hatua zimeshindikana, kwani tulianzia , kijiji, wilaya, mkoa na kwa mkurungezi wa NEMC lakini hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya malamiko yetu kuwajengea uswaiba viongozi tuliyolalamika kwao na huongozi wa kiwanda, hivyo baada ya kuathirika kwa muda mrefu na kutoa taarifa bila mafanikio tumelazimika kuchangua kamati ya watu 3 miongoni mwetu kufuatilia malamiko yetu, ambao ni 1. Abrahamu Mathayo 2.Sauda Omari 3.Mwamedi Heri ,kielelezo ‘’MZ1’’ taarifa ya kikao cha tarehe 04/06/03
1. Katibu Mkuu Kwa niaba ya wananchi wenzetu wa kijiji cha kisemvule tupenda kuleta malalamiko yetu kwako juu ya ukiukwaji wa makusudi wa sheria ya Mazingira namba 20 ya 2007 pamoja Sheria ya leseni ya viwanda namba 10 ya 1967 juu ya madhara ya uchafuzi wa mazingira unaotekelezwa makusudi na kiwanda cha cement cha maweni lime stone (ARM CEMENT) kilichojengwa katika kijiji cha kisemvule wilaya mkuranga, bila kuzingatia matakwa ya kisheria katika msingi ya uharibifu wa mazingira

2. Katibu Mkuu kiwanda cha cement cha maweni lime stone (ARM CEMENT) walikiuka kwa makusudi sheria ya usimamizi wa vyanzo vya maji (The Water Resources Management Act, No.11 of 2009) kwa kuaribu kisima cha asili kwa kuchafua maji ya yake kwa matope na vumbe ya cement na hivyo wananchi tukashindwa kuendelea kutumia kisima hicho bila kisima mbadala, pia matope na vumbi ndani ya makazi yetu na kutuathiri kiafya bila kupata msaada wowote wa kuzuia uharibifu huo, unaendelea kwa makusudi

3. Katibu mkuu baada ya kiwanda kuanza uchafuzi huo tulifikisha malalamiko yetu kwenye baraza ya ardhi na ustawi wa jamii cha kijiji cha kisemvule walijaribu kudhibiti uchafuzi huo wa mazingira bila mafanikio pamoja na kuwa uongozi wa kiwanda walikiri juu ya uchafuzi huo na kuaidi kuwalipa waathirika ili wahame wasiendelehe kupata madhara, lakini baadaye waligeuka wakakataa kutekeleza makubaliano mbele ya baraza huku wananchi tukiendelea kuhathirika, kielelezo ‘’MZ2” taarifa ya vikao vya baraza

4. Katibu Mkuu baada ya uongozi wa wa kiawanda kubadilika kinyume na makubaliano kwenye baraza huku wananchi wakiendelea kuathirika baaza na waathirika waliamua wapereke malamiko yao kwa mkuu wa wilaya na baaraza iwaandikiea barua yenye maelezo yote kielelezo ‘’MZ3’’ taarifa ya kikao na barua ya kumpelekea mkuu wa wilaya mkuranga

5. Katibu Mku baada ya wananchi tuyoteuliwa kufika kwa mkuu wa wilaya na kumwezea matatizo hayo ya madhara ya kiafya dhidi ya uchafuzi wa mazingira inayotekezwa na kiwanda naye akatupereka kwa mkurugenzi, mkurugenzi naye akatupeleka kwa mwanasheria wa wilaya, atimaye mwanasheria akatueleza atafuatilia, kilichofuata viongozi hao kwa wakati tofauti wamekuwa wakifika kiwandani hapo na kujenga uswaiba badala ya kusimamia sheria ya mazingira huku wananchi wakiendelea kuathirika na uchafuzi huo, kielelezo ‘MZ4’’ taarifa ya kikao pamoja na orodha ya waathirika na makubaliano yao na uongozi wa kiwanda,

6. Katibu Mkuu mnamo tarehe 10/09/2013 tuliandika barua ya malamiko kwenda kwa mkurugenzi mkuu wa mazingira (NEMC) pamoja na kufikisha barua hiyo tangia wakati huo hakuna jibu lolote wala atua zozote za kisheria zilizochuliwa dhidi ya uchafuzi huo yenye madhara katika afya zetu, jambo linalotushawishi kuwepo kwa mazingira ya rushwa katika kuchukua atua juu ya malamiko kwani kushindwa kwa mkurugenzi kujibu barua yetu na kukaa kimya bila bila kuchukua atua imetokesha imani na ofisi yake, kielelezo,”MZ5” barua tuliyomuandikia mkurugenzi

7. Katibu Mkuu maswali ya msingi ya kujiuliza kiwanda kiwezaje kupewa kibali cha ujenzi bila kufanyika kwa environmental impact assessment jambo ambalo lingezuia kutokea kwa madhara kwa binadamu na uharibifu, uzembe wa aina hii aipaswi kuvumiliwa hata kidogo.

8. Katibu Mkuu watendaji kushindwa kuchukua hatua na kujenga uswaiba na uongozi wa kiwanda pamoja na malalamiko ya wananchi pia inatupa picha nyingene juu mazingira ya rushwa na kusababisha utekelezaji kuwa mgumu kwao,

9. Katibu Mkuu Madai ya Msingi katika Sheria za Mazingira ni:- (a) uongozi wa kiwanda kufikishwa mahakamani juu ya uvunjifu wa sheria ya nchi (b) waathirika kulipwa kulingana na madhara tuliyopata (c) kukomeshwa kwa uchafuzi huo au waathirika kuamishwa kwa kulipwa sitaiki zao kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 ya 1999kipengele 1(1)(g) ili wasiendelee kuathirika (d) viongozi wote waliyozembea na kushindwa kuchukua hatua kuchuliwa hatua za kinidhamu, (e) kupitia upya juu ya vibali alivyopewa muwekezaji katika kujenga kiwanda katikati ya makazi ya watu kama yalikidhi matakwa ya kisheria katika ujenzi huo (f)malipo ya gharama za usumbufu kwa mujibu wa sheria
Wako katika ujenzi wa taifa

…………………………… …………………………… ……………………….. 1. Abrahamu Mathayo 2. Sauda Omari 3. Mwamedi Heri Simu 0762763252, 0655763252 Waathirika/Wakilishi wa Wanakijiji wa Kisemvule Waliyoporwa Ardhi yao
Nakala kwa
1. Mwenyekiti wa kamati ya Bunge OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA P.O. Box 9133 Dar es Salaam

2. Katibu wa Waziri(Mazingira) Ofisi ya makamu wa Rais-Mazingira P.O. Box 5380 Dar es Salaam Simu +255 22 2122470

3. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Na Biashara P.O. Box 9503 Dar es Salaam Simu +255 22 2127884

4. Mkurugenzi wa Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu ya Rais - Mazingira P.O. Box 5380 Dar es Salaam Simu +255 22 2113983

5. Mkurugenzi wa Tathmini Athari za Mazingira Baraza la Hifadhi ya Mazingira Ofisi ya Makamu ya Rais Mazingira P.O. Box 5380 Dar es Salaam Simu +255 22 2134603

6. Katibu wa Mkuu wa Mkoa Pwani P.O. Box 30080 Kibaha – Pwani

7. Mkuu wa Wilaya Mkuranga P.O. Box 1 Mkuranga – Pwani

8. Mkurugenzi wa Wilaya Mkuranga
P.O. Box 1
Mkuranga –Pwani

9. Mkurugenzi Mtendaji
Maweni Lime Stone (ARM CEMENT)
P.O. Box
Mkuranga
 
Back
Top Bottom