Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,821
- 33,205
Hivi karibuni Mkurugenzi wa NEMC alitangaza uwepo wa ssheria ya kuzuia kelele na mitetemo kwenye makazi ya watu, kadhalika Waziri wa mambo ya ndani alirudia tangazo hilo na kuwataka wanaopiga muziki kwa sauti kubwa kuacha mara moja ama kufunga vizuia sauti.
Inaelekea maagizo hayo yote mawili, lile la Mkurugenzi wa NEMC na Waziri Lugola yamepuuzwa, labda kwasababu hakuna anayefanyia kazi maagizo hayo.
Ushauri: NEMC wanunue vifaa maalumu vinavyoweza kupima viwango vya kelele vilivyozidi kiasi kinachokubalika na kuajiri vijana watakaozunguka mitaani na kusoma kelele hizo kisha kutoa taarifa kwa mamlaka husika, hii itakuwa na faida mbili, moja ni ajira kwa waliokosa ajira na watalipwa kutokana na tozo zitakazopatikana, mbili serikali itaongeza mapato kutokana na adhabu kwa wanaokiuka maagizo ya viongozi husika.
POLICE: Watoe namba za wazi kwaajili ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi waliopo kwenye maeneo yenye viwango vya kelele vilivyokatazwa.
Nawasilisha