NEMC: Kunywa bia na kufanya sherehe na matamasha kwenye fukwe ni makosa kisheria

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,217
2,000
Mkurugenzi wa Baraza la Kutunza Mazingira NEMC, Dr Samwel Gwamaka asema baraza la mazingira linashauri kuwa si salama kunywa vileo, kufanya matamasha makubwa ktk fukwe za bahari kwani ni hatari kwa umma mpana na pia inapelekea kuharibu mazingira

Source : millard ayo.
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
10,553
2,000
Mkurugenzi wa Baraza la Kutunza Mazingira NEMC, Dr Samwel Gwamaka asema baraza la mazingira linashauri kuwa si salama kunywa vileo, kufanya matamasha makubwa ktk fukwe za bahari kwani ni hatari kwa umma mpana na pia inapelekea kuharibu mazingira

Source : millard ayo.

Hao NEMC washamba sana, watu wa vijijini huko kuja mjini na kujidai wanajua kila kitu, kumbe ushamba mtupu.

Watembee duniani waone.
Uingereza kuna Brighton Pier Beach, kusini mwa Uingereza.
Imetengenezwa na kuwekezwa hadi ni kituo cha kuvutia sana na kuingiza pesa nyingi.
Lakini Brighton Beach haifikii robo ya uzuri wa fukwe za Tanzania.

Waende Brazil kuona Capo cabana na Beach football.
Waende hapa Zanzibar tu na Lamu,Kenya.

Nchi ikianza kuendeshwa na hao washamba wasio na exposure, ni hasara kwa Taifa.
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,353
2,000
Tuna wasomi wa ajabu Dr ; Profeseli wa kukariri! Jenga kingo imara, toa elimu mazingira dunia ya kufikiri matumizi ya nguvu ya Dola inapita.
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,055
2,000
Hao NEMC washamba sana, watu wa vijijini huko kuja mjini na kujidai wanajua kila kitu, kumbe ushamba mtupu.

Watembee duniani waone.
Uingereza kuna Brightin Pier Beach.
Imetengenezwa na kuwekezwa hadi ni kituo cha kuvutia sana.

Waende Brazil kuona Capo Cabana na Beach football.
Waende hapa Zanzibar tu na Kenya.

Nchi ikianza kuendeshwa na hao washamba wasio na exposure, ni hasara kwa Taifa.
Brighton..... siyo Brightin
Copa Cabana..... siyo Capo Cabana
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,217
2,000
Rio De Janeiro, Brazil

COPACABANA

Copacabana Beach & Boardwalk 🇧🇷 | Rio de Janeiro, Brazil |【4K】2021

Copacabana Beach is the most famous beach in Brazil. This video brings the best of a series of other videos from the channel about Copacabana Beach and the Copacabana boardwalk (calçadão) that were recorded between 2019 and 2021.Source : Vort-V Ambience
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066

Hawa viongozi wasiojijua changamoto sana
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Tuna wasomi wa ajabu Dr ; Profeseli wa kukariri! Jenga kingo imara, toa elimu mazingira dunia ya kufikiri matumizi ya nguvu ya Dola inapita.
Mwingine kaibua hoja
Kumtunza mtu pesa kosa
Watu jela wanaweka pesa makunduchi unataka kutuambia pesa hazichafuki
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,405
2,000
Kichwa cha habari kinapotosha.
Mkurugenzi ameshauri kuhusu mazingira , hajatamka kuwa ni kosa kisheria.
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,405
2,000
Hao NEMC washamba sana, watu wa vijijini huko kuja mjini na kujidai wanajua kila kitu, kumbe ushamba mtupu.

Watembee duniani waone.
Uingereza kuna Brightin Pier Beach.
Imetengenezwa na kuwekezwa hadi ni kituo cha kuvutia sana.

Waende Brazil kuona Capo Cabana na Beach football.
Waende hapa Zanzibar tu na Kenya.

Nchi ikianza kuendeshwa na hao washamba wasio na exposure, ni hasara kwa Taifa.
Ninachokiona NEMC ni kujitanua mabega na kujiona wana mkono mpana.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,217
2,000
Kichwa cha habari kinapotosha.
Mkurugenzi ameshauri kuhusu mazingira , hajatamka kuwa ni kosa kisheria.

https://www.nemc.or.tz
NEMC: Mwanzo

MAENEO YA FUKWE AU VYANZO VYA MAJI NI MAENEO NYETI KIMAZINGIRA- Dkt. GWAMAKA

large-1636379548-2.JPG

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa maeneo ya fukwe au vyanzo vya maji ni maeneo nyeti kimazingira kwa sababu ni maeneo ambayo yanategemewa na viumbe wa Baharini na Jamii inavitegemea.

Ameyasema hayo alipofanya ziara pamoja na wakaguzi wa mazingira kutoka NEMC katika maeneo ya fukwe za Coco jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hiyo ni kwa ajili ya ukaguzi wa mazingira katika eneo hilo.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ... MAENEO YA FUKWE AU VYANZO VYA MAJI NI MAENEO NYETI. ... ZIJUE ISTILAHI ZA .....
Aidha, Dkt. Gwamaka ameeleza kuwa ziara hiyo katika maeneo ya Fukwe za Coco ni kutokana na ujenzi au maendeleo yanayofanyika katika eneo hilo kuangalia kama yamezingatia Sheria ya Mazingira 2004 SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 (NA.20 SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 - [PDF Document] ambayo inasema maendelezo yoyote ambayo ni ya kudumu au ambayo yanaweza kuleta athari zozote za kimazingira basi yafanyiwe Tathmini ya Athari ya Mazingira.

Ameendelea kusema "mazingira ya fukwe za Coco kwa sasa yanaridhisha kutokana na ujenzi wa majengo ya muda yanayovutia yaliyojengwa maeneo hayo ambayo yanatoa nafasi kwa wajasiliamali wenye kipato cha chini kujipatia fedha za kujikimu pamoja na watu kupata sehemu nzuri ya kupumzika na kuweza kula.

Pia nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na uongozi wake wote kwa jitihada wanazofanya kuwatengea maeneo wajasiliamali wadogo na vilvile kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa utaratibu maalum kama ambavyo ujenzi wa vibanda visivyo vya kudumu unavyoendelea katika fukwe za Coco" .

Dkt. Gwamaka amesema kuwa watashirikiana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Manispaa ya Kinondoni ilikuona namna gani wataboresha maeneo hayo ili kukabiliana na changamoto za kimazingira ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa fukwe unaosababishwa na Mabadiliko ya Tabianchi kwa hiyo mahali hapa panatakiwa kufanyiwa maboresho kwa kuweka mawe ambayo yatasaidia maeneo haya yawe endelevu pamoja na kuboresha miundombinu ya maji taka na maegesho ya magari.

Amemaliza kwa kusema kuwa jambo kubwa la kuzingatia maeneo haya ni kuongeza idadi ya vyoo kwani kutokana na muonekano mzuri wa maeneo hayo basi watu wengi watavutiwa kuja hapa.

NEMC tutakuwa bega kwa bega na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mahali hapa panakuwa salama wakati wote ili eneo hili liwe eneo ambalo wananchi wa kawaida wanaendelea kufaidi matunda ya uhuru wa Nchi, na liwe eneo la mfano kwa wajasiriamali wadogo kwa nchi nzima ya Tanzania
MISINGI YA JUMLA

4. Haki ya kuwa na mazingira safi, salama na ya kiafya. 5. Haki ya kufungua mahakamani madai kuhusu
Soma zaidi kutoka chanzo :
Source : Habari | NEMC
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
3,130
2,000
Hao NEMC washamba sana, watu wa vijijini huko kuja mjini na kujidai wanajua kila kitu, kumbe ushamba mtupu.

Watembee duniani waone.
Uingereza kuna Brightin Pier Beach.
Imetengenezwa na kuwekezwa hadi ni kituo cha kuvutia sana.

Waende Brazil kuona Capo Cabana na Beach football.
Waende hapa Zanzibar tu na Kenya.

Nchi ikianza kuendeshwa na hao washamba wasio na exposure, ni hasara kwa Taifa.
Washamba hata wakisoma tofauti yao na asiyesoma ni negligible.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom