NEMC imetoa siku 14 Kanisa libomolewe ,lakinu Jumba la Mch Rwakatare(CCM) Limeachwa!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEMC imetoa siku 14 Kanisa libomolewe ,lakinu Jumba la Mch Rwakatare(CCM) Limeachwa!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Oct 16, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  NEMC Kanda ya Ziwa imempa siku 14 Askofu wa kanisa la Tanzania Evangilism kubomoa Kanisa lake lililo jengwa katika kijito Mtaa wa Msumbiji kata ya Pasiansi ya Jiji la Mwanza.

  Barua ya amri hiyo Namba NEMC/MZA/vol/153 ya tarehe 8/10/2012 inamtaka Askofu huyo kuvunja Kanisa lake kwa Gharama zake bila Shuruti na imesainiwa na Mhandisi Bi Anna Mdomo.


  Wakati Kanisa likibomolewa , Jumba la Mbunge wa CCM limeachwa huku yeye akihamia katika Nyumba yake kwa Mbwembwe jambo ambalo linaonyesha Serikali kuwaonea baadhi ya Maaskofu kwa kuwa hawapo CCM au hawana fedha na sheria za nchi zinakandamiza wanyonge tu!!


  [h=3]Halima Mdee: Jumba la Mch. Rwakatare nalo libomolewe ili Kuepuka Double Standard![/h] Tuesday, October 02, 2012 Prosper Mallya changia hapa


  [h=2][/h]
  [​IMG]
  Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

  Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.

  Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (Nemc).

  Operesheni hiyo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini cha kushangaza nyumba ya Mchungaji Lwakatare ambayo imejengwa kinyume cha sheria haikuguswa.​
  PICHA: HEKALU JIPYA LA MCHUNGAJI MAMA RWAKATARE  [​IMG]
  Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
  [​IMG]
  MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
  [​IMG]
  Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
  [​IMG]
  Watu wakijiachia
  [​IMG]
  Kabati la vyombo
  [​IMG]
  Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
  [​IMG]
  Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi la kifahari mjengoni humo
  [​IMG]
  Wakati wa msosi
  [​IMG]
  Mambo ya dressing table
  [​IMG]
  Kitanda chake cha kulalia
  ---
  Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
  Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.


  Posted in:
  Email This BlogThis! Share to Twitter

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Reactions:[/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...