NEMC hii ya Pub Casa ni kero hapa Vi nane

Mkuu, pia kuna ile bar pale miti mitatu (TTG), aisee huwa najiuliza watoto wanao ishi maeneo yale huwa wanapataje usingizi.

Wale jamaa hawajali Afya ya wakazi wa maeneo yale, kelele usiku kucha. Hakika Serikali kupitia NEMC, waangalie upya Jambo hili,
Kuna siku nilienda kupata supu pale asubuhi kama saa 4 jamaa walifungua mziki kwa sauti ya juu sana. Can you imagine? Saa 4 aisee tulichachamaa mpaka wakazima. Inatakiwa hawa NEMC na ofisi za serikali za Mitaa wawe wakali na huu ujinga wa hawa wenye hizi bar kila sehemu makelele tu. Hakuna hata amani.
 
Bar inaitwaje?

Umenikumbusha WAMBURA PUB, 2019.

Kuna dogo meneja hapo, kila polisi wakikamata yeye hakamatwi. Anaendelea kuuza pombe mpaka asubuhi. Kumbe dogo yupo kazi ya serikali.
 
Sio huko kimara tu...sehemu nyingi Sana wamiliki wa bar wanakiuka Sheria,unakuta bar wanafungua mziki wa juu Sana inakuwa kero.
Leseni ya bar ktkt ya nyumba za watu za kazi Gani nemc wanatoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ni maafisa biashara wa hizi Halmashauri wanatoa vibali vya kuendesha biashara ya vileo katika makazi ya watu. NEMC kuna sijui yule mama mbuzi sijui wapo tu pale akina Heche ambao wanaona raha kuitwa Wakili msomi ambaye hana lolote anashindwa kuzibana hizi bar
 
Bar inaitwaje?

Umenikumbusha WAMBURA PUB, 2019.

Kuna dogo meneja hapo, kila polisi wakikamata yeye hakamatwi. Anaendelea kuuza pombe mpaka asubuhi. Kumbe dogo yupo kazi ya serikali.
Wambura ndogo
 
Nemc alikuepo Jamaa anaitwa Echa sijui alienda wapi yule alikua anachukua hatua haraka.Siku hizi hawako active sana.
 
Halafu ipigwe ile ngoma asikwambie mtu tu tu beeer tamu...utajikuta mwenyewe upo ndani unacheza😁
 
Hili ni tatizo la kitaifa.

Serikali inabidi iongeze ukali kwenye hili jambo.

Ma bar yanasumbua Sana huku mitaani kwa kupiga mziki wa sauti ya juu
Wanawalipaje mishahara watu wanaolala usingizi?
 
NEMC should become serious about their roles. Apart from bars/pubs, there are also many other worship centers that are cropping up in residential areas!!
Hilo pepo la kuandika lugha zisizoeleweka kwenye andiko la watu limekupata saa ngapi?
 
Back
Top Bottom