Nelson Mandela: Safari yake ya kwanza nje ya nchi

Livino Haule

Member
Mar 22, 2015
21
22
SAFARI YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI

By Livino Ngalimitumba Haule (Lingaha)

Nelson Mandela akiwa mwanaharakati wa kupigania uhuru wa watu weusi wa Afrika Kusini toka kwa serikali ya 'mkaburu.' Ndiye aliyeteuliwa na chama chake (ANC) kwenda nje ya nchi kuonana na watu wakiwemo viongozi na wanaharakati wa mataifa mbalimbali wa Afrika na duniani ili kupata mbinu, msaada na maarifa ya namna ya kujikomboa toka kwa mkoloni. Upendeleo huu aliupata yeye akiwa kama amepewa pia jukumu la kuwa Amiri Jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama vya chama chake vyenye lengo kuu la kujiandaa kuingia vitani kumwondoa mkaburu kwa nguvu. Vikosi hivyo viliitwa (kilugha) _UMKHONTO WE SIZWE_(MK) "Spear of the Nation" (kwa Tanzania sasa ni sawa na Redbrigade- Chadema na Greenguards- CCM).

Kwakuwa wapigania uhuru wote Afrika Kusini walikuwa wanatafutwa na kukamatwa na polisi wa kikoloni na kisha kufungwa ili kuzima ndoto zao za uhuru; Mandela alitakiwa kutoka nje ya nchi yake bila Hati ya kusafiria (Passport) na pia alitakiwa kutoka nje ya nchi kwa kutoroka kwa kificho (kwa njia za panya).

Hivyo tarehe 10/01/1962 Mandela alitoroka Afrika Kusini na kusafirishwa kwa gari usiku na mchana kwa siku mbili akafika nchi ya Bechwanaland (sasa Botswana) wakati huo ikiwa chini ya uangalizi wa serikali ya Mwingereza (British protectorate) ambako alifika tarehe 12/01/1962. Alisafiri akiwa na pesa taslimu zipatazo £600 (Paundi 600).

Hapa Tanganyika (Tanzania bara) alifika mwezi huohuo _January_ baada ya kusafiri kwa ndege toka Botswana, alifika wakati huo wanachi wake wanasherekea na kufurahia uhuru wao mchanga uliopatikana mwezi mmoja uliopita tu (tarehe 09/12/1961).

Dar es Salaam alipokelewa na mwanamke mwenyeji wake _FRENE GINWALA_ ambaye aliishi hapa nchini akiwa amehama toka Afrika Kusini. Mandela alifichwa miongoni mwa raia wa Tanganyika akiwa Dar ili asigundulike na kushtukiwa na wapelelezi (spies) wa serikali ya kikoloni ya Afrika Kusini wasije wakamdhuru. Hayo yalikuwa ni maelekezo ya Mwenyekiti wa ANC _Bw.OLIVER TAMBO_ambaye wakati huo alikuwa nchini Ghana.

Hapa Dar es Salaam NELSON MANDELA alikutana na MWL. NYERERE Rais wa kwanza wa Tanganyika ambapo walijadilina namna ya kuikomboa Afrika Kusini lakini Mandela hakukubaliana na Nyerere alimshauri kuachana na mpango wa kutafuta uhuru kwa kuingia vitani/kumwaga damu (Armed struggle) na kwamba ANC na MANDELA wanatakiwa kushirikiana na Chama kingine cha upinzani (PAC) kilichopigania uhuru chini na Mwenyekiti wake _ROBERT SOBUKWE_aliyekuwa mhadhiri wa Lugha za Afrika ktk Chuo kikuu cha Witwatersrand huko Afrika Kusini.

Toka hapa Mandela alienda nchini Ghana ambako alionana na Mwenyekiti wake Bw. Oliver Tambo.

Toka Ghana Mandela alienda Ethiopia ambako kiongozi Mkuu wa nchi hiyo _Emperor HAILE SELASSIE_aliitisha mkutano wa kuanzisha vuguvugu la ukombozi wa Afrika _(Pan- African Freedom Conference)_ambao ulifanyika mjini Addis Ababa.

Akiwa Ethiopia Mandela kwa mara ya kwanza alipata nafasi ya kuhutubia Mkutano wa nchi za Afrika na kufanikiwa kushawishi Afrika Kusini kuingia ktk Jumuiya iliyoitwa PAFMECA na baadaye kubadilishwa jina kuitwa PAFMECSA (Pan African Freedom movement for East, central and South Africa). Pia Mandela ndiye aliyeushawishi mkutano huo kupanua (extend) maeneo ya harakati na kujumuisha nchi za Magharibi na Kaskazini mwa Afrika. ndipo vuguvugu likakubaliwa kushughulikia ukombozi wa Afrika yote; hivyo wakaunda Umoja wa Nchi huru za Afrika "Organization of African Union" (OAU).

Baada ya mkutano huo Mandela alienda nchini Misri akazungumza na viongozi mjini Cairo.

Alipotoka Misri Nelson Mandela alienda nchini Tunisia ambako Rais _BOURGUIBA alijitolea kuisaidia chama cha ANC na MANDELA mafunzo ya kijeshi pamoja na kutoa pesa kiasi cha £5,000 (paundi) kwaajili ya kununulia Silaha.

Baada ya Tunisia Mandela alielekea Morocco na kisha alipelekwa mpakani mwa nchi hiyo na *Algeria*ambako alishuhudia vikosi vya wapiganaji wa vita vya msituni (Guerrilla Fighters) wakiwa wamejipanga gwaride la heshima kwa kiongozi wao wa ukombozi _Bw. Ahmed Ben Bella_baada ya kutoka jela na akiandaliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Algeria. Hapo Ben Bella alimtia moyo na hamasa Mandela kwa maneno yafuatayo:
_"The Freedom for Algerians is meaningless so long as Africa is under claws of imperialism"_
Yaani _Uhuru wa watu wa Algeria hauna maana kama nchi nyingine za Afrika bado zipo kwenye makucha ya ukoloni._

Baadaye Mandela alielekea nchini Mali ambako katika mazungumzo yake na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo _Ndg. Madeira Keita_ alimuonya Mandela na ANC juu ya mpango wake wa kuingia vitani kupiginia uhuru kwamba ulikuwa ni mpango hatari zaidi.
Akiwa nchini humo Mali Mr. Mandela pia alikutana na kujadiliana na _Sir MILTON MARGAI_waziri mkuu wa Sierra Leone na Rais _TRUMAN_wa Liberia. MANDELA hakufanikiwa kuonana na Rais _Sekou Toure_ wa Senegal licha ya kutamani sana kumwona.

Kutoka Mali, Nelson Mandela alirejea tena nchini Ghana ambako alikataliwa na kunyimwa kabisa nafasi ya kumwona Rais _Kwame Nkrumah_kwa madai kwamba ANC siyo chama cha siasa cha kitaifa bali ni kikundi chenye itikadi za kikabila tu _(Tribal Organization_);kwahiyo Waziri wa mambo ya nje alisisitiza kwamba Mandela hatakiwi kuonana na Rais Nkrumah. Nely Mandela alikatishwa tamaa na kujisikia kuvunjwa moyo. Zaidi aligundua kwamba Rais wa Ghana alikuwa amedanfanywa kuhusu habari za ANC na siasa za Afrika Kusini kwa ujumla.

Baada ya Ghana Mr. Mandela Alisafiri kwenda mjini London nchini Uingereza kwa ziara ya siku kumi. Alisafiri kwa kibali cha safari toka nchini Tanganyika (he got and used a _Travel Permit from Tanganyika)._

Akiwa London alipoona Afisa wa Uhamiaji amekuwa na mashaka naye, maswali mengi juu ya sababu za kwenda nchini humo; Mandela aliamua kujiokoa kwa kudanganya kwamba anafanya utafiti huko kwani anaandika kitabu.
_"I am writing a book on Evolution of Political thought in Africa; so I want to visit museums and Libraries."_
NB: By hooks and crooks one must fulfill one's ambition. Jiongeze fahamu kumshinda mpinzani wa malengo yako.*

Pia akiwa nchini Uingereza Mandela alitahadharishwa na rafiki zake wengi walioishi uhamishoni baada ya kukimbia mkono wa serikali ya mkoloni iliyotaka kuwakamata na kuwafunga wote waliopinga utawala huo kwa kuwaita "wahaini, wachichezi au wahujumu serikali." Rafiki zake hao (akiwemo mama mmoja aliyeitwa _ESME_mke wa _TODD MATSHIKIZA_) walimsisitizia Mandela abaki nje ya nchi yake asirudi tena Afrika Kusini kwani anatafutwa sana na polisi.

*Esme:*_"Then why go back?"_
*Mandela:*_"A Leader stays with his people"_

Baada ya ziara yake Mandela alirejea tena nchini *Ethiopia* ukiwa ni Mwezi wa Sita _(June)_kwaajili ya kupata mafunzo ya kivita/kijeshi ambayo yalipangwa kuchukua muda wa miezi 6. Ni kwa madhumuni ya kujiandaa vema kama Amiri Jeshi mkuu wa vikosi vya upiganaji (MK) vya chama chake.

Mandela alipatiwa mafunzo hayo ya kijeshi katika milima iliyo nje kidogo ya mji wa Addis Ababa; ndipo kwa mara ya kwanza ktk maisha yake Mandela alianza kushika Bastola _(pistol)_na silaha nyingine za moto kama bunduki _(automatic rifle)._

Hapo Mandela alijifunza kuhusu mbinu mbalimbali za kivita;
_1.Kutengeneza na kutega mabomu (bombs)_
_2.Kufyatua mizinga (mortars)_
_3.Miondoko mbalimbali ya kijeshi ktk mapigano ya msitun_ ikiwa ni pamoja na nidhamu ya kijeshi (military descipline).
Katika DIARY yake Mandela tarehe 29/06/1962 alinukuu/alinote kwamba somo lake la kwanza lilikuwa ni _DEMOLITION (namna ya kubomoa au kuharibu ngome ya adui)._

*Hali ya kisiasa nchini Afrika Kusini wakati huo*
Mandela akiwa katika mafunzo Ethiopia, nchini kwake familia yake- mkewe na watoto walikuwa wakinyanyaswa na serikali. Mandela alikuwa akisakwa popote wakati wote. Nyumba yake ilikuwa inazingirwa na polisi karibu kila siku, huku wakiuliza Mandela yuko wapi.

_"The police searched or visited my house nearly every day, asking where Mandela is."_Alieleza WINNIE mke wa Mandela.

Wakati huo pia Serikali ya 'mkaburu' na Bunge walipitisha mswada wa sheria mpya _(The Sabotage Bill)_ya namna ya kuwadhibiti wanaharakati wanaodai uhuru wa nchi yao, ambao serikali iliwaita _wahujumu_wa serikali (saboteurs). Mswada huo uliipa nguvu mahakama kutoa hukumu ya kifo _(deah penalty)_kwa makosa madogo tu yalihusisha uharibufu wa mali (umma), uchochezi au kuhamasisha migomo na maandamano ya kuipinga serikali hiyo ya kikoloni.

*Kwahiyo*nchi ya Afrika Kusini ilikumbwa na taharuki kubwa, vijana wenye msukumo wa kimapinduzi walifika mwisho wa kuogopa, chama cha ANC kinalazimishwa na wafuasi wake kutangaza vita vya msituni dhidi ya serikali, mauaji na uharibifu vimetawala, vikosi vya upiganaji (MK) vimechoka kukaa mafichoni; wana hamu ya kuingia vitani wakati Amiri Jeshi mkuu wao Nelson Mandela hayupo.

*Mandela anaitwa kurudi nyumbani Afrika Kusini kwa dharura ili kuongoza na kudhibiti vikosi vya ulinzi na upiganaji (MK)*
Chama chake cha ANC kililazimika kutumia simu ya maaandishi (za wakati huo _telegram_) katikati ya mwezi wa 7 mwaka huo 1962, kwamba arudi haraka kwani hali ni tete kwao.

Mandela alitakiwa kukatisha mafunzo ya kijeshi Ethiopia akarudi kwao Afrika Kusini kwa ndege kupitia _Khartoum_ (Sudan) na _Dar es Salaam_(Tanganyika) hadi _Botswana_ambako alisafirishwa kwa gari kwa siri hadi nchini Afrika Kusini alipofika tarehe 24/07/1962.

Alitoka Ethiopia akiwa na zawadi ya Bastola _(pistol)_ na risasi zipatazo 200.

Alipofika nchini kwao alipokelewa na chama chake kama shujaa mkubwa ambaye kwake chama kitanufaika sana na vikosi vya ulinzi na upiganaji vitapata mafunzo na ujuzi kwa umahiri mkubwa.

*Lakini* ndani ya wiki moja baada ya furaha ya kufika kwake na matarajio makubwa, ndoto yake ilizimwa ghafla. _Mnamo tarehe 05/08/1962 tu; siku ya Jumapili NELSON MANDELA akiwa kwenye gari na rafiki yake CECIL WILLIAMS alikamatwa na Polisi bila kutarajia yeye wala *ANC*chama chake._

BY Livino Ngalimitumba Haule (Lingaha)
 
Back
Top Bottom