Nehemia Mchechu ni jipu lililoiva muda si mrefu litatumbuka

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,635
29,509
Yule mtaalam wa kuuza nyumba za BEI NAFUU ndugu Nehemia hana muda mrefu utasikia nae kikaangoni.

Maana amepewa dhamana ya kuongoza shirika la Umma ili wananchi waweze kupata nyumba kwa bei nafuu lakini matokeo yake unakuta eti inauzwa 165m hiyo je ndo bei rahisi au nafuu. Ila yeye ataona nafuu maana analipwa mshahara mkubwa
 
Wajenge hata maeneo ya pemben kidogo ya miji halafu wapangishe. Watakuwa wanasaidia hata kupanua na kuboresha miji
 
Si NHC pekee taasisi zingine pia ambazo serikali ilizianzisha kwa nia njema kuwa msaada kwa watz wa kada ya chini na Kati nyingi zimegeuzwa kuwa taàsisi binafsi kwa ajili ya kuwaibiwa wale zilizoundwa kwa kuwasaidia.
Nakupa Mfano mdogo ambao nimeupata kwa kufanya utafiti mdogo baada ya mimi mwenyewe kushtushwa nilipotaka mkopo benki ya posta.

Kama mstaafu nilienda ili nipate mkopo wa wastaafu kama wanavyotangaza.
Lakini baada ya kufanyiwa mahesabu ya kile ninachoweza kukopa na kiasi nitachoridisha kwa miaka 3 nilishangaa sana na kuumia kwa jinsi nilivyogundua namna waßtaafu wanavyoibiwa na benki ya posta.

Nilikuwa nikope 5m lakini ningerejesha almost 12m ambapo ingekuwa zaidi ya 50% ingekuwa ni riba ya mkopo ukiachilia mbali fedha zingine ninzokatwa kwa kupewa huo mkopo na kuendesha akaunti yangu kwa kipindi chote cha mkopo.
Niliamua kufanya utafiti nikagundua kuwa benki tayari inamgawanyiko mkubwa wa wafamyakazi wa zamani wanaolipwa mishahara ya kizamani kwa mfumo wa kizamani na wafamyakazi wapya ambao hulipwa kwa mfumo usio rasmi bali makubaliano wakati wa kuajiriwa na waajiriwa wapya wengi ni ndugu na jamaa ama kutoka taasisi aliyotokea mmoja wa wamaohitaji mwajiriwa.

Mfano; Mkurugenzi wa Operations na Mtendaji mkuu, Wetokea Stanchart hivyo tegemea wengi wa waajiriwa wapya watatoka huko. Vivyo hivyo kwa idara nyingine. Ukabila, ukanda, uhomeboy na urafiki ndiyo msingi na kigezo kikubwa kwa ajira mpya. Usipokuwa makini unaweza kudanganywa na ile wanasema wame automate system hivyo haiko biased. Ni uongo kwa sbabu kilichokuwa automated ni utumaji wa maombi, Nani aitwe kwenye interview na nani asiitwe ni kazi ya mikono ya wao.

Hivyo kwa kutumia online CV wanaweza kuchagua wale ambao wanajua kwamba ni weak wakiwapambanisha na mkusidiwa huku wale wanaoonekana strong hawaiatwi ( hawawi shortlisted )
Kuna ujanja wa kutangaza faida kubwa kana kwamba faida yote inapelekwa Muhimbili kununua vifaa tiba wakati faida hiyo ni matokeo ya kuwafukarisha masikini wa Tz.

Hutumia faida hiyo kwa kujineemesha binafsi kwa safari na manunuzi yaliyo ama inflated au kubadili bei baada ya mikataba kwa ama kuwaongezea kazi zilizokuwa sehemu ya mikataba au kwa kujifanya muonekena husika hawaupendi ili kuwaobia wananchi.

Taasisi zimeanzishwa kwa kodi zetu kwa nini zitumike kutuibia wenyewe? Mheshimiwa Magufuli na Mheshimiwa Majaliwa
Ni wakati wa kumulika wezi walioko kwenye taasisi za umma ambao hutumia ujanja wa kibepari kuwaibia wanachi ili serikali ione wanafanya kazi wakati matokeo hayatokani na mipango ya kiuchumk ma ukuzaji biashara bali ni ujanja wa kuwaibia wanyonge wa taifa hili.
 
H1N1 haya sasa ndo majipu unajua, nepotism kuiondoa imekua ngumu sana maana hata Don mwenyewe ukimchungulia vizuri nae anapitia mistari hyo hyo. Kwa Nehemia alitakiwa ajenge nyumba nyingi ambazo zingekua msaada kwa masikini lkn amefanya kinyume chake kwa mfano mdogo tu karume baba alijenga nyumba kule kwao zanzibar ndeeefu na kuwapa masikini bureee kitu ambacho mcechu angeeza pale magomeni kutengeneza na kuuza au kupangisha kwa bei rahisi kweli
 
Kwa mishahara ya watanzania wengi zaidi watumishi wa umma ni ngumu kununua hizo nyumba za NHC..Watumishi waliokuwa wakinunua wengi ni kwa hela za magumashi sasa JPM kaziba mianya ndio zitadoda mbaya..hata hao wafanyabiashara huwaga hawanunui nyumba za NHC kutokana na ufinyu wake na bei kubwa.Kajumba ka vyumba viwili na sebule tena gorofani huna hata parking ya wageni kinauzwa mill 250..shiit
 
ANACHOKIFANYA Nehemia kwa sasa mnaweza kutomuelewa usipoangalia mbali. Support ya serikali. Kwa mfano Magufuri akisaport shirika vya kutosha wanaweza kujenga na kugawa nyumba bure (yataka sera ya mtawala).

Nehemia Amelichukua shirika katika mazingira magumu. Tupia macho miaka ya mbele wakati wamejenga majumba kama hayo kibao nchi zima. Yamtaka raisi mmoja atakae ingia madarakani akaamua nyumba hizo ziuzwe kwa milioni10. Yes inawezekana kwa taifa tajiri kama letu. Yeye anachojua ni kujenga tu hiyo mijumba mpaka huyo rais atakapokuja.

Sijui mmepata picha hawezi kujenga vijumba vya ovyo kwa bajeti zao wanazopewa na serikali za sasa. Inambidi aingie mikataba na mabenki kujenga na bei ndio hizo. ila hakuna kustop dawa ni kujaza tu mijumba kama hatutapata uongoz wa juu makini kwa sasa watoto wetu watapata. Natamani nchi nzima jaza iumba hiyo halafu tuone sera za wanasiasa zinasemaje. MSECHU maono yake ya mbali ndio hayo!!!

Mie namsapot kwa kuwa picha ya mbele nimeisoma vizuriIE. MSECHU jaza mijumba hiyo nchi nzima, hapo mbele tutapata serekali itakayorahisisha mambo.
 
Ila nahisi hata serikali ina shida katika hili, ilipaswa kodi ya ongezeko la thamani ( VAT) iondolewe kuanzia kwenye materials za ujenzi mpaka kwenye nyumba wanazo uza. Nafikiri ikiwa hivyo bei inaweza shuka sio kwa sasa kajumba ka vyumba viwili tena kamejengwa kwa tofali za choma eti milioni 45.
 
Licha ya jamaa kuleta mapinduzi NHC ila kabugi sana maana shirika halisaidii watu wa kipato cha chini. Nyumba zao ziko bei sana hata mtu wa kipato cha chini hawezi nunua, rais amulike na huku.
 
ANACHOKIFANYA NEEMIA KWA SASA MNAWEZA KUTOMUELEWA USIPOANGALIA MBALI. Support ya serikali. Kwa mfano Magufuri akisaport shirika vya kutosha wanaweza kujenga na kugawa nyumba bure (yataka sera ya mtawala).
NEEMIA Amelichukua shirika katika mazingira magumu. Tupia macho miaka ya mbele wakati wamejenga majumba kama hayo kibao nchi zima. YAMTAKA RAIS mmoja atakae ingia madarakani akaamua nyumba hizo ziuzwe kwa milioni10. Yes inawezekana kwa taifa tajiri kama letu. Yeye anachojua ni kujenga tu hiyo mijumba mpaka huyo rais atakapokuja.
SIJUI MMEPATA PICHA. HAWEZI KUJENGA VIJUMBA VYA OVYO kwa bajeti zao wanazopewa na serikali za sasa. Inambidi aingie mikataba na mabenki kujenga na bei ndio hizo. ila hakuna kustop dawa ni kujaza tu mijumba kama hatutapata uongoz wa juu makini kwa sasa watoto wetu watapata. NATAMANI NCHI NZIMA JAZA MIJUMBA HIYO HALAFU TUONE SERA ZA WANASIASA ZINASEMAJE. MSECHU maono yake ya mbali ndio hayo!!!
MIE NAMSAPORT KWA KUWA PICHA YA MBELE NIMEISOMA VIZURI. MSECHU jaza mijumba hiyo nchi nzima, hapo mbele tutapata serekali itakayorahisisha mambo.
...du!..hapa ndio umemaliza akili zako zote na nyingine umekopa!
...maskini weeee!...wa kuhurumiwa tu!
 
Licha ya jamaa kuleta mapinduzi NHC ila kabugi sana maana shirika halisaidii watu wa kipato cha chini. Nyumba zao ziko bei sana hata mtu wa kipato cha chini hawezi nunua, rais amulike na huku.
JIONGEZE. Serikali ikiamua bei itashuka tu. mikakati yake kwa sasa hakuna jinsi. Kama hapati msaada wa ruzuku toka serikali. unataka afanyeje.
Nyie wananchi ndio mlitakiwa muishinikize serikali bei zishuke. sasa mnamuandama yeye. Eti jipu. Hapa jipu ni wananchi kuchagua watawala
 
ANACHOKIFANYA NEEMIA KWA SASA MNAWEZA KUTOMUELEWA USIPOANGALIA MBALI. Support ya serikali. Kwa mfano Magufuri akisaport shirika vya kutosha wanaweza kujenga na kugawa nyumba bure (yataka sera ya mtawala).
NEEMIA Amelichukua shirika katika mazingira magumu. Tupia macho miaka ya mbele wakati wamejenga majumba kama hayo kibao nchi zima. YAMTAKA RAIS mmoja atakae ingia madarakani akaamua nyumba hizo ziuzwe kwa milioni10. Yes inawezekana kwa taifa tajiri kama letu. Yeye anachojua ni kujenga tu hiyo mijumba mpaka huyo rais atakapokuja.
SIJUI MMEPATA PICHA. HAWEZI KUJENGA VIJUMBA VYA OVYO kwa bajeti zao wanazopewa na serikali za sasa. Inambidi aingie mikataba na mabenki kujenga na bei ndio hizo. ila hakuna kustop dawa ni kujaza tu mijumba kama hatutapata uongoz wa juu makini kwa sasa watoto wetu watapata. NATAMANI NCHI NZIMA JAZA MIJUMBA HIYO HALAFU TUONE SERA ZA WANASIASA ZINASEMAJE. MSECHU maono yake ya mbali ndio hayo!!!
MIE NAMSAPORT KWA KUWA PICHA YA MBELE NIMEISOMA VIZURI. MSECHU jaza mijumba hiyo nchi nzima, hapo mbele tutapata serekali itakayorahisisha mambo.
Tatizo ni kuimba pasipo kuangalia maono ya uanzishwaji wa NHC au taasisi nyingine yoyote ya umma.
Kama unachukulia NHC kama taasisi ya serikali liyoanzishwa kuisadia serikali kufanya biashara ya kujenga na kuuza nyumba maono ya Msechu na wewe yako sawa kabisa. Bahati mbaya kwako na Msechu wako hakutafuta muda na nafasi ya kutaka kujua madhumuni ya kuanzishwa kwa shirika hilo.

Msechu alipochukua shirika angegundua kuwa sababu za kuanzishwa kwake ndizo zililifanya liwe vile na kilichotakiwa ni kutengeneza proposal ya kusaidia serikali kulifufua ili lifikie malengo yake na sio kuwa taasisi ya kujenga majumba ambayo kimsingi hayana faida kwa walengwa.
Kwa kuwa watz tunatabia ya kutotaka kujua mambo kwa kusoma hivyo kuangalia yasemwayo kwenye Luninga tu. Ndiyo maangamizi ya taifa letu yalioo na wajanja wataemdelea kupiga na kuisha kwa kuwafukarisha watu ambao tayari ni mafukara huku wachache wakineeka kwa kuendesha mashirika yaliyoanzishwa kwa kodi za watz.

Kazi ya kujenga na kuuza nyumba sio ya serikali
Tuliambiwa serikali haifanyi biashara. Sasa hizi taasisi za uma zinazofanya biashara kwa kuibiwa umma huku zikitumia address ya kuwa za serikali ni madudu gani kama sio majipu ?
 
Tatizo ni kuimba pasipo kuangalia maono ya uanzishwaji wa NHC au taasisi nyingine yoyote ya umma.
Kama unachukulia NHC kama taasisi ya serikali liyoanzishwa kuisadia serikali kufanya biashara ya kujenga na kuuza nyumba maono ya Msechu na wewe yako sawa kabisa. Bahati mbaya kwako na Msechu wako hakutafuta muda na nafasi ya kutaka kujua madhumuni ya kuanzishwa kwa shirika hilo. Msechu alipochukua shirika angegundua kuwa sababu za kuanzishwa kwake ndizo zililifanya liwe vile na kilichotakiwa ni kutengeneza proposal ya kusaidia serikali kulifufua ili lifikie malengo yake na sio kuwa taasisi ya kujenga majumba ambayo kimsingi hayana faida kwa walengwa.
Kwa kuwa watz tunatabia ya kutotaka kujua mambo kwa kusoma hivyo kuangalia yasemwayo kwenye Luninga tu. Ndiyo maangamizi ya taifa letu yalioo na wajanja wataemdelea kupiga na kuisha kwa kuwafukarisha watu ambao tayari ni mafukara huku wachache wakineeka kwa kuendesha mashirika yaliyoanzishwa kwa kodi za watz.
Kazi ya kujenga na kuuza nyumba sio ya serikali
Tuliambiwa serikali haifanyi biashara. Sasa hizi taasisi za uma zinazofanya biashara kwa kuibiwa umma huku zikitumia address ya kuwa za serikali ni madudu gani kama sio majipu ?
umesema angeandika proposal? kwa serikali hizi za ccm.
Nia ni kuwamilikisha wananchi nyumba bora. Kama zinaonekana ghali ni jukumu letu kuibana serikali au kuchagua serikali itakayokuja na sera za bei nafuu kwa hizi nyumba.
 
Maono ya uanzishwaji wa taasisi yanatakiwa kuzingatiwa, kama kulihitajika taasisi ya kujenga na kuuza nyumba, hiyo ni biashara na serikali haifanyi biashara.
Kuna neema ambayo kampuni binafßi wasingeweza kuwa nayo, kutumia anwani ya serikali.
Sipingi kujenga na kuuza kwa bei yoyote waitakayo lakini nataka waangalie sababu za kuanzishwa kwake ndizo zitoe dira ya matendo yao.
 
Back
Top Bottom