Nehemia Mchechu- Bosi Mkuu Shirika la Nyumba Tanzania [NHC]

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
banjako.jpg

Bw. Nehemia Mchechu

Kwa mujibu wa kifungu Na. 18 (1) cha Sheria Na. 2 ya 1990, iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (The National Housing Corporation Act No. 2 of 1990) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Ndugu Nehemia Mchechu (37) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Uteuzi huu unaanzia tarehe 1/3/2010.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nehemia Mchechu alikuwa Mkurugenzi
Mkuu (Chief Executive Officer) wa Benki ya "Commercial Bank of Africa".

Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.

Ndugu Nehemia Mchechu akishirikiana na Bodi mpya ya Shirika hili na timu ya Menejimenti ya Shirika hili, amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.

Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1990 iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Bwana K. Masudi Issa Msita kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo. Bwana K. Masudi Issa Msita ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council).

Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria hiyo hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo.
1. Msajili wa Hazina - (Wizara ya Fedha).
2. Mkurugenzi wa Nyumba - (Wizara ya Ardhi).
3. Prof. W.J. Kombe - (Chuo Kikuu cha Ardhi).
4. Bwana Enock Maganga - (Benki Kuu).
5. Bi Subira Mchumo - (Sekta Binafsi).
6. Bwana Elius Mwakalinga - (Wizara ya Miundombinu).
7. Bi. Shally Raymond - (Mbunge)
Uteuzi huu unaanza tarehe 28/02/2010 na ni wa miaka mitatu.

Imetolewa na:-
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi

Source:
Michuzi Blog​
 
Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.

............ amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.

utata mtupu hapo ktk red
kwamba hiyo ndiyo qualifications yake kuwa Dg wa NHC? was he alone huko benki to implement it?

TZ ya kufikirika.

since 1961.....hakuna kilichofanyika.....
 
utata mtupu hapo ktk red
kwamba hiyo ndiyo qualifications yake kuwa Dg wa NHC? was he alone huko benki to implement it?

TZ ya kufikirika.

since 1961.....hakuna kilichofanyika.....

Unamaana gani? wamesema amepewa jukumu la kufanya hicho kilichoandikwa na kama CEO wa CBA alifanya hayo sasa unataka nini zaidi? hakuwa peke yake lakini kumbuka yeye ndiye aliyekuwa CEO! au hujui maana ya CEO?
 
Nehemiah ni kijana ambaye yuko ambitious,mwenye integrity na mchapakazi sana. Amefanya kazi pia Standard chartered bank kabla ya kuwa CEO wa CBA. Amesoma BCom (finance) pale mlimani na alikuwa kiongozi wa DARUSO.

Amefanikiwa kupanda katika corporate radar kwa muda mfupi kutokana na kujiamini, uaminifu na uchapakazi wake. Unajua katika private sector kupanda vyeo kama yeye katika umri kama wake lazima uwe na kitu cha ziada.

NHC

Watumishi wa NHC nawashauri kama mnafanya kazi kwa mazoea,mmeletewa mtu ambaye hatafumbia macho mambo yenu ya chini. Tutegemee mabadiliko katika utendaji wa NHC hasa miradi mipya ya ujenzi nyumba.

SERIKALI

Katika uteuzi ambao umefanyika kwa kuangalia vigezo na kuitakia mema nchi yetu na mashirika ya umma,huu ni wa kwanza. Serikalini mtu akitoka private sector hatakiwi kabisa kwani analeta efficiency ambayo haitakiwi kabisa huko.

NEHEMIAH MCHECHU KYANDO

Tegemea vipingamizi kwenye kazi yako mpya kwani serikalini mwenyewe unajua kulivyo. Efficiency ni tatizo sana,barua moja inachukua mwezi kutoka office moja kwenda nyingine wakati private sector ni dakika tu.
 
Hongera Nehemiah, an hour ago nilikuwa nasubiri iwe kweli na imekuwa!!!!! He is capable na ataligeuza lile shirika!!! Tulimhitaji sana na tunashukuru umekubali maombi yetu, watanzania!!!! Head Search!!!!!!!

Ni vema kuanza kutumia watanzania wenye vipaji na uwezo kiakili kuwatumikia watanzania kwa kutumia Rasilimali tulizokuwa nazo??? Wenzetu wamemtumia tangu akiwa katika Mabenki na wamefanikiwa mno. Poleni Kenya Commercial Bank!! Walimtaka kwa udi na uvumba!!! Tumikia Tanzania sasa mkuu. Prof. M. Chijoriga, keep it up mama!!
 
Not a Professor .......Dr. Marcelina Chijoriga
 
Bravo brother Kyando, the name I have known you for yrs!!!!!!! For this I applaud Mr Chiligati and confidently blv he has a right man for the job!
 
Hongera sana ila ana kazi kubwa sana katika kuliweka sawa shirika hilo huko Tanzania.
 
Hongera Nehemiah, an hour ago nilikuwa nasubiri iwe kweli na imekuwa!!!!! He is capable na ataligeuza lile shirika!!! Tulimhitaji sana na tunashukuru umekubali maombi yetu, watanzania!!!! Head Search!!!!!!!

Ni vema kuanza kutumia watanzania wenye vipaji na uwezo kiakili kuwatumikia watanzania kwa kutumia Rasilimali tulizokuwa nazo??? Wenzetu wamemtumia tangu akiwa katika Mabenki na wamefanikiwa mno. Poleni Kenya Commercial Bank!! Walimtaka kwa udi na uvumba!!! Tumikia Tanzania sasa mkuu. Prof. M. Chijoriga, keep it up mama!!

Huyu mama chijoriga ameingiaje katika hili bandiko??? Kuna mambo mawili: moja, Mama chijoriga ndio Maane. Pili, Inawezekana unampongeza mama chijoriga kwa kumfundisha huyu kijana pale Mlimani.
 
Hongera sana Kaka na hongera ziende pia kwa Dada Mercy kwani wanasema Behind every successful man, there is a woman. Tunajua unaweza kaka na tuna imani nawe.
 
I have faith in my counttry. That slowly but surely, it will change for the better.

Huu uteuzi, unaonyesha kwamba..watanzania tusipende kulaumu tuu. Sasa kama hapa huyu amepewa hii opportunity, I earnestly believe he will be the agent of change. Make no mistake, ukifanya kazi inaonekana and you will be handsomely rewarded.

Ushauri wangu: Lets invest in education. Tufanye kazi kwa kujiamini na tulinde heshima na intergrity za ofisi na majukumu tuliyokabidhiwa. I am sure huyu kijana he has struggled and negotiated his way up there.

Hongera sana Nehemiah. I trust you will do us proud as a young man trying to prove that tunaweza kuendelea na kufanikiwa bila ufisadi.

Masanja
 
Huyu mama chijoriga ameingiaje katika hili bandiko??? Kuna mambo mawili: moja, Mama chijoriga ndio Maane. Pili, Inawezekana unampongeza mama chijoriga kwa kumfundisha huyu kijana pale Mlimani.

Mkuu mimi si Dr. Marcelina Chijoriga. Huyu mama ni lecturer pale idara ya Commerce and Managment (sijui kama ndivyo inavyojulikana siku hizi baada ya kuwa independent/autonomous)!!! Ni excellent mentor kwa watu wengi, I believe Msechu is one of them. To be frank mwanangu alisoma idara ya huyu mama. Ni katika waalimu wazuri ambao wako zaidi kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuliko kuwafelisha au supplementary. Umenipata mkuu!! Ukipata mafanikio na wote walio behind your mafanikio ni lazima wapongwezwe pia(waalimu, wazazi, watoto, mke, marafiki, etc).
 
Mkuu mimi si Dr. Marcelina Chijoriga. Huyu mama ni lecture pale idara ya Commerce and Managment (sijui kama ndivyo inavyojulikana siku hizi baada ya kuwa independent/autonomous)!!! Ni excellent mentor kwa watu wengi, I believe Msechu is one of them. To be frank mwanangu alisoma idara ya huyu mama. Ni katika waalimu wazuri ambao wako zaidi kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuliko kuwafelisha au supplemntary. Umenipata mkuu!! Ukipata mafanikio na wote walio behind your mafanikio ni lazima wapongwezwe pia(waalimu, wazazi, watoto, mke, marafiki, etc).
Umetembea upesi hadi umesahau herufi hapa so imeharibu maana ya sentensi yako.
 
-Safi sana,keep it up bro.Nathani hilo shirika sasa litajiendesha kibiashara zaidi at the sametime likishikilia umuhimu wa establishment of a welfare society

-Ana kazi kubwa sana pale,sasa inabidi serikali iangalie na iwe makini namna hii katika kufufua mashirika yetu kwa kuwapa nafasi young blood ili waendeleze professionally zaidi
 
hongera sana Nehemiah, kazi ipo kiasi manake watu wamezoea kufanya kazi kimazoea but its high time kubadilika, tafuta enginers mzuri wa kukugaid then business as usual that what we want na bima tunataka kijana ambaye anajua kiu ya watanzania kazi mbele, Dada Mercy keep it up as well tutafika mbali
 
Nafurahi kuona vijana wenzangu wanapata kazi kama hizi! Please Nehemia you have to deliver tumechoshwa na wazee akina Malecela, Kingunge, Makweta, Majiyatanga na wenzao!
 
Nfurahi kuona vijana wenzangu wanapata kazi kama hizi! Please Nehemia you have to deliver tumechoshwa na wazee akina Malecela, Kingunge, Makweta, Majiyatanga na wenzao!
FMs akiona!!!!!again hongera Nehemia
 
Kuna mdaua hapo juu kataja Kenya commercial bank.

Huyu jamaa anatokea Commercial bank of africa.

Pia kuna mdau kaongelea Engineer mzuri nadhani ni Kimambo,

Hivi si alikuwepo huko Engineer John kijazi ?kwa sasa ni Ni balozi wa tanzania nchini India.Pale inaonekana kuna kazi kweli kweli,inabidi alete revolution kule.All the best Bro

Serikali nayo iweke mazingira mazuri kumwezesha,mtu kuwa smart tu haileti changes
 
Back
Top Bottom