Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Jina lake halisi ni Thomas Fuller, Mwafrika aliyezaliwa huko Benin mwaka 1710 na kuuzwa utumwani huko Alexandria,Virginia USA mwaka 1724 akiwa na mika 14.
Alipewa jina la "Virginia Calculator" kutokana na uwezo wake wa ajabu wa kufanya kufanya mahesabu magumu kichwani.
Mfano aliulizwa kuna sekunde ngapi katika mwaka mmoja na nusu?ndani ya dakika mbili alijibu kwa usahihi kwamba ni 47,304,000.
Aliulizwa tena mtu mwenye miaka 70 Siku 17 na saa 12 ameishi kwa sekunde ngapi?Ndani ya dk moja na nusu aliweza kujibu kwa usahihi kwamba ni sekunde 2,210,500,800.
Hio ni mifano michache tu kati ya mingi ambayo Negro Tom aliweza kujaribiwa kujua uwezo wake lakini alikuwa akifanya maajabu mengi tu ya kimahesabu kichwani.
Alikuwa na uwezo wa kufanya hesabu ya tarakimu tisa uizidishe kwa Tisa au saba izidishwe kwa saba na jibu lake lizidishwe kwa saba iende hivo mpaka Mara saba kichwani na akatoa jibu sahihi kwa muda mfupi tena akiwa kazungukwa na watu huku wakimkatisha kwa maswali na kelele na hapa na pale lakini alikuwa na uwezo wa kuwajibu kisha kurudia pale alipoishia na kutoa jibu.
Pia alikuwa na uwezo wa kufanya hesabu hizo huku kichwani akijumlisha au kutoa miaka mirefu na mifupi, kuhesabu idadi ya nywele kwenye mikia ya ngo'mbe, farasi nk.
Kilichowashangaza zaidi wengi ni kwamba Negro Tom pamojana na kufanya mahesabu magumu hivyo hakuwahi kujua kusoma na kuandika mpaka alipofariki mwaka 1790 akiwa na miaka 80 huko Virginia USA.
Je, Waafrika huu uwezo tuliupotezea wapi mpaka wazungu wanajidai kwamba wapo juu kuliko watu weusi?