Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Ni mawazo gani ya kwanza yanayokujia kichwani juu ya moja au baadhi ya mambo kati ya haya yanapotekea juu ya mme/mke/mpenzi wako?
Kama wazo la kwanza linalokujia ni kuwa 'itakuwa yuko/alikuwa anakusaliti na mtu mwingine', then ujue uhusiano au ndoa yako iko matatani
Ushauri
Wazo la kwanza; Kila kitu kiko ok, au itakuwa kajisahau, simu imeisha chaji n.k
Wazo la pili; atakuwa na dharura...
Wazo la tatu; ananisaliti (najua ni vigumu kupotezea moja kwa moja hasa kwa mtu unayempenda, lakini hata hivyo utakapojiridhisha kuwa sio moja kati ya mawazo hayo mawili ya kwanza, then angalau kwa mbaali anza kufikiria usaliti...
Kwa bahati mbaya hata huku JF, kuna watu wanakuja kuomba ushauri juu ya kuwa na tatizo katika mahusiano yao, lakini ukifuatilia utakuta ni kwa sababu alikuwa na 'negative' thinking kama wazo lake la kwanza...
- Unapiga simu hata mara tano, haipokelewi...
- Unapiga simu unaambiwa inatumika, subiri au piga baadae, unasubir, na bado hakati inayoongea nayo apokee ya kwako...
- Unapiga simu jioni nzima au usiku mzima unaambiwa haipatikani...
- Unapiga simu anapokea, na kwa haraka anakwambia sory, ntakupigia baadae na anakata...
- hajakupigia simu siku nzima, tofauti na siku nyingine...
- Kasafiri, na frequency ya kukupigia simu inapungua...
- Unampigia simu usiku anakwambia yuko baa...
- Kasafiri kufikia nyumba ya wageni, na baada ya kukuambia amefika, simu yake haikupatikana tena usiku mzima...
- Ni mwanachuo anayekaa hosteli, siku za mwanzo alikuwa anakuja home weekend lakini sasa kila weekend anakuambia kuna discusion...
- Ni nesi na unampigia simu usiku anakuambia siku hiyo hana raha maana yuko zamu na Dr anayemtongozaga, kisha baadae simu yake inazimwa au ukipiga haipokelewi...
- Ana kawaida ya kurudi nyumbani mapema, then siku hiyo hajarudi hadi usiku sana na ukipiga simu inaita bila kupokelewa...
- Amerudi nyumbani kachelewa na anaonekana mchovu na akilala anakugeuzia mgongo...
- Karudi nyumbani late, asubuhi unaingia kwenye gari unakuta harufu kali ya manukato...
- Kachelewa kurudi home/hakurudi home kabisa/yuko safarini na unapiga simu alafu sauti ya kwanza kusema 'alooo' ni ya opposite sex na unayempigia...
- n.k...