comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana jamvi Salaam.
Neema ya kuwepo kwa dalili za mafuta na gesi ambayo serikali ya mapinduzi Zanzibar jana kupitia Makamo wa pili wa Rais Mh Balozi Seif Ali Iddi ilizindua ndege maalumu kwa ajili ya utafiti wa miamba yenye mafuta na gesi nchini humo ambapo kazi ya kuanza kutafuta miamba yenye mafuta na gesi Zanzibar imeanza rasmi leo.
Aidha kwa kuwa Zanzibar ina rasilimali nyingi kuliko wingi wa watu ambapo idadi ya wazanzibar haizidi milioni sita vilevile kwa kuwa katiba ya Zanzibar imeweka wazi kwamba suala la mafuta na gesi Zanzibar sio la kimuungano ni wazi SMZ ina spidi kubwa na ya haraka katika mipango ya kuijenga Zanzibar,
Kufanikisha mpango huo wa upatikanaji wa nishati hizo ni wazi kwamba Zanzibar itakuwa na uchumi imara sana kuliko nchi zote ukanda wa Afrika mashariki na maziwa makuu, jitihada zao za vitendo zimefanikisha kwa haraka sana kuanza kwa kazi hiyo ya utafutaji mafuta na gesi,
Aidha teknolojia ya kisasa ya kutumia ndege maalumu ni wazi kabisa tekinolojia hiyo itatoa jibu la haraka na uchimbaji utaanza mara tu ya taarifa ya kitaalamu juu ya uwepo wa kiasi gani cha gesi na mafuta na aina ya miamba iliyopo