Neema ya Kijiografia, Tabia Nchi na Hali ya Hewa inaifanya Tanzania kutaka kila kitu kwenye Kilimo

nazidaka

JF-Expert Member
Mar 14, 2014
204
250
Tanzania imebarikiwa kuwa na mchanganyiko wa hali ya hewa inayoakisi karibu mabara yote duniani. Yapo maeneo yenye mvua hadi kero, maeneo yenye baridi, sehemu zenye mvua chache na kadhalika. Mbali na Bahari, maziwa, mabwawa, mito na vijito. Hali hii ikijumuisha na sifa mbalimbali za udongo inaifanya nchi yetu kukubali kustawisha mazao mbalimbali kuanzia yale ya nchi za joto, uvuguvugu na hadi nchi za baridi.

Neema hii imepelekea watoa maamuzi na watalaamu kutamani kila kuzalisha kwa wingi kila zao wanalodhani linakubali nchini. Yaani ni kama mtu anayetaka kula kila chakula kilichopo mbele yako na mwisho huwezi kula hata kimoja.

Nasema hivi kwa sababu hata kwenye mpangilio wa kuendeleza sekta ya kilimo utakuta leo watu wameshupalia, michikichiki, kesho alizeti kabla haijamalizika unakutana na mpunga, mahindi. mara ngano na shayiri, mara parachichi. Hapo sijataja Kahawa, pamba, mkonge, chai, pareto, kokoa.

Ukiacha miaka ya mwanzo wa uhuru hadi miaka ya 1980's ambapo tulifikia uzalishaji uliotukuka wa mazao kama mkonge, pamba n.k. Kipindi hiki chenye mihemko mingi ya matamko kuliko uhalisia hatujaweza kufikia uzalishaji wa mzuri kwenye mazao mengi tu. Kilimo kimekuwa ni siasa tu hakuna chapuo la zao linalopigwa na kufikia ufanisi.

Ifike mahala tuamue kama nchi kuwa pamoja na neema kubwa ya hali ya hewa yawepo mazao machache tu ya kitaifa walau 3-5 yafanyiwe kazi kwa ukamilifu wake na tija ipatikane. Hayo mengine yalimwe na watakaotaka kujifurahisha nayo tu.

Tusitamani kama nchi kulima na kupigia "kelele" kila zao na mwisho hatumudu ukamilifu wa uzalishaji wa zao lolote na tunabaki kuzishangaa nchi zenye fursa chache za kilimo kama Izrael, Misri na Ethiopia kuzalisha na kuuza mazao yao kwa wingi.

Sijagusia mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo, sungura, simbilisi nk). Bahari na samaki wake ndio usiseme.

Mtaka yote hukosa yote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom