Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Poleni na Majukumu,

Serikali yetu kwa sasa inapitia katika kipindi kigumu cha tatizo la ajira rasmi kwa vijana na watu wazima pia. Pamoja na Yote Serikali imekuwa ikisisitiza vijana wajiajiri bila kuwawezesha ni kwa namna gani vijana waweze kujiajiri.

Jijini Arusha mzungu mmoja aitwae Michael fortson yeye na mke wake wameanzisha kituo kiitwacho Neema Village ambapo mbali na kusaidia watoto yatima, wameamua kuwawezesha Wanawake Wajane, Waliotelekezwa(single mothers) na wale wasiokuwa na ajira au shughuli yoyote kwa kuwa patia yafuatayo :

MITAJI YA BIASHARA
mzungu huyo kwa kupitia taasisi aliyoianzisha yeye na mkewe bi Doris fortson huwapatia wanawake tajwa hapo juu mitaji ya biashara mbalimbali kulingana na uhitaji na uzoefu wao. Mfano mitaji ya mifugo ya kufuga kama vile kuku , biashara za sokoni nk.

MALIPO YA KILA MWEZI
Michael fortson hutoa kiasi cha pesa kila mwezi Kwa ajili ya Kujikimu wao na watoto wao kwa Wanawake wote tajwa hapo juu.

KODI YA NYUMBA NA VYOMBO VYA. NDANI
Wakina Mama wote ambao hawako kwenye nyumba zao huwezeshwa kwa kulipiwa kodi ya Miezi sita pamoja naKununuliwa vyombo vya ndani kama vile majiko ya gesi, majaba ya kuhifadhia maji, vitanda Magodoro na mashuka yake nk.

ELIMU /UFUNDI
Kuna wale wanawake wenye kupenda kujifunza kazi za ushonaji, ubunifu, ufugaji nk. Hupewa mafuzo yote hapo Neema Village bure na baada ya mafuzo hupewa vyeti pamoja na Kuwezeshwa kufanya kile walichokisomea au kujifunzia hapo kwenye kituo .

WAZAZI
Kuna wale wanawake waliotelekezwa na watoto wachanga Hospitalini na. Majumbani baada ya kujifungua ambao bado ni wazazi. Basi wanawake hao hupewa huduma zote muhimu katika kipindi chote cha uzazi ikiwa ni pamoja na chakula, maziwa ya unga ya watoto, pampers,lishe pamoja na nguo za watoto na gharama za kumpeleka mtoto kiliki.

Pamoja na mambo mengine mengi ambayo Neema Village imekuwa ikisaidia kwa wakinama wote wenye uhitaji mkoani Arusha pia imetoa huduma ya kuchimba visima vya maji na kuweka masimtank kwenye viunga bure kwa wananchi wote wanao zunguka eneo hilo.

Lengo la Neema Village ni kupanua wigo zaidi na Kufikia walengwa tofauti tofauti.

Je serikali yetu imeshindwa kuwawezesha vijana wetu kwa namna yoyote ile? mfano wa large scale agriculture, kilimo chenye tija.
Kuwataftia masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi,mosoko nje ya nchi yangesaidia sana katika uchumi wetu maana yanaleta /yanaingiza pesa ndani ya nchi na hivyo kuongezeka Kwa mapato

Kufungua Ranch kila wilaya ambapo vijana wengi wangeajiriwa huko

Kuomba misaada mbali mbali katika mataifa ya magharibi ikiwemo ajira za vijana na Masomo katika nchi hizo kuliko kila siku kukopa fedha ambazo hatujui zinaenda wapi.



Screenshot_20211025-160046.png
 
Duh? Hivi hata CHILD IN THE SUN Wana Mambo yao?
Kwa hivo tuwafukuze ili wale yatima wawe omba omba?
Hivi hiyo ngozi unaiangalia kwenye tv au huwa inawafuatilia in deep?..

Anakupenda kwa kiasi gani mpaka akulelee wewe na mwanao kwa maziwa ya kiwandani huku mkeo anasomeshwa ufundi na kulipwa nyumba plus mshahara every end of the month?.
 
world vision katika rangi ya pink na nyekundu.

il sio mbaya,kikubwa msoto unaregea.
 
Mbongo aka mwafrika ni mbinafsi

Utakuta mtu kakwiba mabilion ya fedha

Kayaficha,badala pesa hiyo aitumie awekeze

Afungue mradi,atoe ajira

Yeye kayakalia tu mabilionn

Ova
Mwizi Hana akili ya kuwekeza. Unakuta waziri Fulani amepiga mabilioni sana sana atakachowekeza Ni kujenga nyumba za kupangisha Mbweni na Mbezi beach, kununua shamba Kibaha misugusugu na kuweka ng'ombe na mbuzi. Zingine kumnunulia wife harrier, nyumba ndogo Nissan dualis. Hawana akili ya kuwekeza hata kiwanda Cha maji.
Bure kabisa
 
Back
Top Bottom