The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,589
- 14,136
Hivi karibuni Bw. Nsekela wa CRDB alisema mabenki yatashusha riba na kweli ameishi kwenye maneno yake.
Leo CRDB wametangaza kushusha riba kutoka 20% hadi 9% kwa wakulima na kutoka 16% hadi 13% kwa wafanyakazi.
Ingawa riba bado ni kubwa sana ila kiukweli hii ni neema kwa wafanyakazi. Tunatarajia ama tunahitaji mikopo kwa wafanyakazi kushuka hadi tarakimu moja ama single digit na wakulima kushuka zaidi kwani hiyo ndio inaenda kwenye uchumi halisi.
Tunasubiri NMB, NBC, Stanbic, Standard chartered, TCB, Azania, na bank nyingine watangaze kushusha bei.
Jitihada hizi za kushusha riba alizianzisha Magufuli, kabla ya Magufuli wafanyakazi tulikua tunakopa kwa kati ya 22% hadi 26%. Baada ya Magufuli kuamua kushusha riba ya hati fungani za serikali kutoka 16% hadi 9% ndio bank zikaanza kushusha riba hadi kati ya 16% na 18% kwa wafanyakazi.
Tunaomba serikali iendelee kuzibana hizi bank zishushe riba za mikopo ili kukuza na kuchochea uchumi. Tuwapongeze pia serikali kupitia BOT kutoa fungu la kuziwezesha bank kwa riba ndogo na zenyewe zikopeshe kwa riba ndogo.
Safi sana CRDB Bank PLC.
Mama anazidi kuupiga mwingi Sana.