Neema kwa wafanyakazi, CRDB imeshusha riba hadi 13% kwa wafanyakazi na 9% kwa wakulima

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Hivi karibuni Bw. Nsekela wa CRDB alisema mabenki yatashusha riba na kweli ameishi kwenye maneno yake.

Leo CRDB wametangaza kushusha riba kutoka 20% hadi 9% kwa wakulima na kutoka 16% hadi 13% kwa wafanyakazi.

Ingawa riba bado ni kubwa sana ila kiukweli hii ni neema kwa wafanyakazi. Tunatarajia ama tunahitaji mikopo kwa wafanyakazi kushuka hadi tarakimu moja ama single digit na wakulima kushuka zaidi kwani hiyo ndio inaenda kwenye uchumi halisi.

Tunasubiri NMB, NBC, Stanbic, Standard chartered, TCB, Azania, na bank nyingine watangaze kushusha bei.

Jitihada hizi za kushusha riba alizianzisha Magufuli, kabla ya Magufuli wafanyakazi tulikua tunakopa kwa kati ya 22% hadi 26%. Baada ya Magufuli kuamua kushusha riba ya hati fungani za serikali kutoka 16% hadi 9% ndio bank zikaanza kushusha riba hadi kati ya 16% na 18% kwa wafanyakazi.

Tunaomba serikali iendelee kuzibana hizi bank zishushe riba za mikopo ili kukuza na kuchochea uchumi. Tuwapongeze pia serikali kupitia BOT kutoa fungu la kuziwezesha bank kwa riba ndogo na zenyewe zikopeshe kwa riba ndogo.

Safi sana CRDB Bank PLC.

 
I think zitashuka zaidi,
Kuna mdau WA bank ananiambia stanbink na equity wanakuja na 10-11% Kwa wafanyakazi, This year zitakomea kwenye 10%, Ila next year zitashuka zaidi baada ya serikali kupata ule mkopo wa $ 3B na kuzikopesha mabenk,

Zikifika kwenye 7-8% halafu zikawana na uwezo wa kukopesha hata 200B TSH then uchumi utapaa saana.

Neema ziendelee kushuka
 
I think zitashuka zaidi,
Kuna mdau WA bank ananiambia stanbink na equity wanakuja na 10-11% Kwa wafanyakazi, This year zitakomea kwenye 10%, Ila next year zitashuka zaidi baada ya serikali kupata ule mkopo wa $ 3B na kuzikopesha mabenk,

Zikifika kwenye 7-8% halafu zikawana na uwezo wa kukopesha hata 200B TSH then uchumi utapaa saana.

Neema ziendelee kushuka
Izo 10-11% zinakuja lini mwez na mwaka gan ili namimi nikachukue uwo mkopo
 
Sina uelewa mzuri juu ya maswala ya Riba ,naomba msaada kwa mwenye ulewa , anisaidie ufafanuzi.
 
Kama BOT wanazikopesha benki kwa riba ya 9% kwanini wao wawakopeshe wateja wao 16%? How much do they pay their customers as interest for their deposits?
 
Back
Top Bottom