Neema kubwa kwenye Bajeti ijayo: Bilioni 776 zamwagwa na wahisani baada ya kuridhishwa na CAG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neema kubwa kwenye Bajeti ijayo: Bilioni 776 zamwagwa na wahisani baada ya kuridhishwa na CAG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, May 11, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wajumbe,

  Serikali yetu sikivu inaendelea kuaminika na kukubalika na wahisani, baada ya report ya CAG na mjadala bungeni wahisani wameazimia kumwana mafweza.  WASHIRIKA wa Maendeleo nchini wametangaza kuingiza Sh bilioni 776 katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha ujao, huku wakieleza kufurahishwa na jinsi taasisi za kusimamia Serikali ikiwamo Bunge, Kamati zake na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinavyofanya kazi zao.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Umoja wa Ulaya (EU), washirika hao wa maendeleo kupitia Mfuko Mkuu wa Bajeti (GBS), wameahidi kutoa zaidi ya nusu ya fedha hizo katika robo ya kwanza ya mwaka huo wa fedha, ili kurahisisha utekelezaji wa Bajeti hiyo ya Serikali.

  Taarifa hiyo ya EU ilieleza, kwamba fedha hizo ambazo ni dola milioni 495 ni mchango mkubwa wa washirika hao wa maendeleo katika kuunga mkono utekelezaji wa mpango wa kupunguza umasikini na wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

  Washirika wa maendeleo wanaochangia GBS ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Canada, Denmark, EU, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. EU imekuwa Mwenyekiti wa kundi hilo kwa miezi 12 iliyopita na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DID) sasa litachukua jukumu hilo. Itaanza uenyekiti mwezi huu.

  Washirika hao wamesema wametoa fedha hizo kutokana na mambo makuu matatu; kuridhishwa na mapitio ya mwaka ya 2011; kuimarika kwa mazungumzo katika baadhi ya sekta muhimu mwaka uliopita na mabadiliko ya GBS kwa miaka miwili iliyopita yaliyosaidia ufuatiliaji kwa miaka kadhaa, wa jinsi fedha za umma zinavyotumika.

  "Matukio ya hivi karibuni yameonesha kwamba taasisi za kuisimamia Serikali nchini zinatimiza majukumu yake katika kufanya tathmini ya ufanisi wa Serikali na kutaka hatua zichukuliwe pale ambapo pameonekana kuwa na udhaifu," ilieleza taarifa hiyo ya EU.

  Hivi karibuni, ripoti za CAG zilionesha kuwapo ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na hali hiyo ilijibainisha katika taarifa za kamati tatu za kudumu za Bunge za usimamizi wa fedha za Serikali; Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, ya Mashirika ya Umma na ya Hesabu za Serikali.

  Kutokana na hali hiyo, wabunge walikuja juu na kuwataka mawaziri wanane ambao wizara zao zilikuwa zimetajwa kwa ubadhirifu mkubwa kujiuzulu, lakini hawakufanya hivyo na wabunge kutishia kuchukua hatua za kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

  Wakati akiahirisha mkutano huo wa Bunge, Pinda alisema Serikali imesikia kilio cha wabunge na itachukua hatua zinazopaswa haraka; na kufuatiwa na tamko la Rais Jakaya Kikwete kwenye Kamati Kuu ya CCM kuwa anakusudia kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

  Alirejea kauli hiyo alipohutubia Taifa katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa mkoani Tanga.

  Mei 4, Rais alitimiza ahadi hiyo kwa kulisuka upya Baraza la Mawaziri kwa ‘kutema' mawaziri sita kati ya wanane walionyooshewa kidole, ‘kutema' naibu mawaziri wawili, kuwabadilisha wizara mawaziri wanane wa zamani, kuteua mawaziri saba wapya huku naibu mawaziri sita wakibadilishwa wizara na kuteua sura mpya 10 kuwa naibu mawaziri.

  Aidha, taarifa ya EU ilieleza kwamba katika mwaka ujao wa fedha, mkazo mkubwa utaelekezwa katika jinsi fedha za umma zinavyotumika kwa kufuatilia kwa karibu jinsi ripoti za CAG zinavyofanyiwa kazi ikiwamo katika ngazi ya Serikali za Mitaa.

  Pia walieleza kuwa watafuatilia kwa karibu utekelezaji wa Bajeti inayoidhinishwa na Bunge. Pia washirika hao wa maendeleo, waliahidi kuendeleza mazungumzo kupitia Kundi la Kujadili Matumizi ya Umma.

  Ilieleza kuwa GBS itajielekeza katika mambo makuu matatu katika kusaidia Bajeti hiyo; kuimarisha mazungumzo kwa kuboresha jinsi washirika hao na wabia wa Serikali wanavyojadili changamoto zinazoikabili nchi; kupata matokeo kwa kuhakikisha maendeleo yanayopatikana nchini yanafuatiliwa kwa karibu na kupitiwa na kuimarisha uwajibikaji kwa kuhakisha wananchi wa Tanzania wanasimamia ipasavyo Serikali yao.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa matokeo ya maendeleo ya Bajeti ni muhimu na GBS inasaidia Serikali kuhakikisha watoto wengi wanakwenda shule, kuwekeza katika miundombinu na kupunguza gharama za kufanya biashara.

  Ilitaja matokeo yaliyopatikana mwaka 2011 kuwa ni kutoa ruzuku ya Sh 25,000 kwa wanafunzi wa sekondari na kupunguza muda wa BRELA kusajili kampuni kutoka siku 6.9 hadi tatu.

  Hata hivyo, taarifa hiyo ya washirika wa maendeleo ilieleza kuwa bado ziko changamoto, likiwamo tatizo katika sekta ya nishati na ubora wa elimu ambao umekuwa ukiandikwa na vyombo vya habari ukijikita katika matokeo mabaya ya ufaulu wa kidato cha nne.

  Pia walieleza kwamba ripoti ya hivi karibuni ya CAG imeonesha kubadilishwa kwa asilimia 41 ya matumizi ya Bajeti ya Maendeleo kulinganisha na Bajeti iliyopitishwa na Bunge.

  Balozi wa EU nchini, Filiberto Sebregondi alisema, "Matokeo yaliyopatikana kwa mwaka 2011 ni lazima yaimarishwe.

  Kwa mwaka wote ujao, washirika wa maendeleo watafuatilia kwa karibu uwazi na matumizi ya Bajeti na thamani ya fedha wanayopata Watanzania kutokana na matumizi ya Serikali. Pia tutafuatilia utekelezaji wa Serikali kuhusu mapendekezo ya CAG

  sosi: HabariLeo | Wabunge, CAG wawakuna wahisani
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kilichofanya hii report ya CAG ikapelekwa bungeni ni Pressure toka kwa wahisani. Walitishia na wengine wameshajiondoa kwenye ufadhili wa bajeti ya serikali (GBS) hadi pale serikali itakapoonesha kwa vitendo kuwa inapambana na rushwa.

  Hoja kwamba 'nilitaka watu wajadili kwa uwazi' does not hold water. Serikali imefilisika na Uncle Sam katoa masharti- take actions or else!
   
 3. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndivyo tunavojidekeza!!, wahisani kila siku mpaka lini!!.
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tanzania tunafurahia misaada kwenye bajeti????? wenzetu Kenya wao wanafurahia bajeti yao kupungua kutegemea wahisani.
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kaka yangu jifunze ku-appreciate! Hebu nipe kaushahidi ka wahisani waliojiondoa kwa kuwa serikali inanuka rushwa!
   
 6. M

  Mboko JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Duuh yaani hawa jamaa wanafurahia bajeti kutoka kwa wahisani shame on you peoples mtategemea wahisani mpaka lini?Hapo hata hakuna haja ya kufurahia ati serikali sikivu imeaminiwa nawaonea haruma wanaopoteza muda wao kuandika vitu kama hivi sasa kama serikali ni sikivu kwa nini ilisubiri Bunge likome ndio wawateme Mawaziri na kama serikali ni sikivu kwa nini iwarudishe Prof Maghembe,Mkuchika na wengine wenye skendo za ajabu ajabu kama Adam Malima na wengineo?

  Si mlaumu sana huyu mleta mada kwani ni mgeni humu ndani usione mtu kama mie sijaposti mambo mengi na ni mtu wa siku nyingi humu kwa kuwa sitaki kupost pumba mara kwa mara kwa wewe na sio ati internet inasumbua mie niko na net 24/7 so poleni sana Wabongo kwaa kusubiria misaada sasa muda si mrefu mtakubaliana na matakwa ya Obama na Cameroon na hapo Kikwete kaalikwa huko kwa Obama so kazi kwenu poleni sana.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Wahisani mpk lini??

  Wao wana nini ambacho hapa kwetu hatuna?
  Mi kwa kweli bado cjaona umuhimu wao hata kidogo.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  ....Mbona kiasi cha pesa kama hiyo kiliingizwa kwenye bajeti ya 2010/2011 na 2011/2012 lakini hakukuwa na maendeleo yoyote ya kuridhisha au kupanda kwa kiwango cha maisha cha Watanganyika wengi?

  Bajeti ya 2010/2011 ilikatika ilipofika December 2011 Serikali ikawa na ukata wa hali ya juu lakini wakawa wanaficha mpaka ilipofika January 2011 walipoandika barua kwa wafadhili kuomba pesa zaidi.

  Bajeti ya 2011/2012 ilikatika August 2011 ambapo tetesi zikaanza September 2011 kwamba Serikali ina ukata wa hali ya juu wakafichaficha hadi October au November walipotamka hadharani kweli Serikali ina ukata wa hali ya juu.

  Sasa hii bajeti ya 2011/2012 labda inaweza kukatika July 2012.

  Hawa magamba vingwendu hawana jipya zaidi ya kuendeleza usanii kila kukicha. Bajeti ya nchi yetu imejaa usanii mtupu!
   
 9. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wahisani watanganyika na DAVID yumo? jidhali na wahisani kuna siku tutavuliwa nguo mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeeeee!
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kwa hili kusipowekwa uangalizi wa umakini hakika liko wazi kabisaaaaaa!

  Dawa ni moja tu "VUA GAMBA" KITA GWANDA uone yajirio hapa Tanzania yetu ya Maziwa na Asali!
   
 11. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We mbona unasahau haraka hivyo au ndo ccm nini ? yote hayo yametokana na pressure ya upinzani bungeni ikiongozwa na kamanda Zitto (MB CHADEMA) dhidi ya kutaka kutokuwa na imani na waziri mkuu vinginevyo mawaziri husika wawajibike.

  HOJA YA ZITTO ILIKUWA NI YA MSUKUMO WA UWAJIBIKAJI, sababu serikali YA CCM ilikuwa haina mpango wa kuwa wajibisha wahusika (mawaziri nk)kutokana na report za CAG NA ZA KAMATI ZA BUNGEZA MASHIRIKA YA UMMA (POAC), HESABU ZASERIKALI (PAC) NA SERIKALI ZA MITAA (LAAC) KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI ZIMEKUWA ZIKITOA REPORT BUNGENI YA UBADHILIFU, LAKINI SERIKALI ILIKUWA HAICHUKUI HATUA YOYOTE NDO MAANA HATA WAHISANI WAKASITA. Ktk hizo kamati zipo zinazoongonzwa na vyama vya upinzani,
   
 12. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  This is another sh*t from our rulers.

  Tunashangilia michango ya serikali fadhili zinazopatikana kutokana na kukusanya kodi toka kwa raia wao, wakati sisi zetu tunasamehe makampuni na wafanyabiashara wakubwa, na tunapokusanya; zetu zinaishia anasa na kuibiwa na walewale tunaowalipa kuzitunza! Tunashangilia nini? Kupanda chati na kuwa nchi omba omba ya pili duniani wakati tuna rasilimali tunazozigawa bure wa ma mafia wa dunia na kugandamiza kabisa maisha ya watu wetu?

  Shame on CCM, shame on the government. Down with CCM and its cohorts.
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  hivi tujiulize swali hili sisi wote!

  wewe kama baba, una akili timamu, afya njema, uwezo wa kuzalisha mali na kutafuta hela, je utafurahia watoto wako na mkeo kuishi kwa hisani ya jirani au kuish kwa hisani yako kama baba na mwenye nyumba?

  pia wewe kama baba miongoni mwa wanao wapo ambao ni hodari wa kutafuta hela na kuzipangia matumiz na hata kufikiri mbinu mbadala za kupata fedha halali na pia wapo ambao ni wavivu, na siyo wabunifu wao kila siku hufikiri tuombe wapi hisani ili tuish, je utamtumia mtoto yupi kati ya hawa katika kazi zako?

  anyway sijui ni siasa lakin binafsi namshauri kikwete aongee na Prof Lipumba vizuri ili amsaidie katika maswala ya uchumi mbona watu wengine wanamtumia na wanatoka? au ndio staili ya nabii hakubaliki kwao? hvi hakunaga cheo cha principle economist of the country?
   
 14. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  and this is my problem... tuna uwezo wa kujilisha, tunalilengesha kwa wahisani and then wanatupa pesa zetu wenyewe

  This is heartbreaking kuiita good news
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  good pwenti... sasa je neema hapo ni ipi mkuu?? kupewa pesa?? i though neema ni sisi kuanza kuonyesha tunaweza kujitegemea....
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ku-appreciate nini hapo? Nchi na resources zote hizo bado tunategemea misaada nje kutengeneza bajeti.

  TANZANIA: Donors fault govt on Budget spending

  Donors yesterday expressed their concerns over the way the government has been implementing its Budget which draws substantial financing from them through General Budget Support (GBS). The European Union Head of Delegation in the country, Mr Tim Clarke, singled out three areas that the government has not been doing enough to show its declared commitment to properly effect the Budget.

  He listed the need to strengthen dialogue, delivering tangible and measurable results as well as improving accountability as areas where the government should focus on as it sets its priorities. Mr Clarke also asked the government to focus on providing answers to Tanzanians instead of seeking to please the donors because it is the wananchi who bear the brunt to economic hardships.

  “We should not shift attention away from you (government) answering mainly to donors; towards the citizens of Tanzania, it’s Parliament, media and wider organs of civil society,” said Mr Clarke in his opening statement during the 2011 GBS annual review, which was officiated by the Finance and Economic Affairs minister, Mr Mustafa Mkulo.

  On dialogue, Mr Clarke noted that though formal and informal communication between the GBS partners and the government have improved, discussions around this year’s Budget were not good.

  “Discussions around this year’s Budget have been complicated and perhaps not as transparent as we would have liked,” he said, noting that the Finance ministry failed to implement its promise to discuss with them elements of the Budget during the preparatory stage before it was approved by Bunge.

  On delivery of measurable results, Mr Clarke noted that Performance Assessment Framework for GBS (PAF) shows that implementation of the Budget did not achieve the results in some areas. He noted, for instance, that area of Outcome Indicators was weak and “this is a concern because this is where we look for results.”

  He said both sides need a dialogue to ask constructive questions like why certain targets were not met and coming with answers that would help to improve matters in the future.

  “The reason this is of paramount importance is because Budget support is often criticised for lack of clear attributable results,” he said. Mr Clarke also noted the war on corruption, business and investment facilitation, rapid budget analysis, quality of local government administration as well as public financial management as other areas of concern.

  He was specific that donors would seek to actively engage with the government on how it responds to the findings by a national Governance and Corruption Survey, whose report was published earlier in the year following an order from President Jakaya Kikwete.

  He said though the economy has been growing well at between six and seven per cent, the government ought to be careful with fiscal deficits which have been growing as well as inflation which has also been on the upward trend for several years now.

  “The fiscal risks around the emergence energy plan and the accumulated arrears in the road sector are a concern for us all. We also have to note the recent trends in the relative stagnation of revenues as share of GDP and the decline of aid inflows,” he warned.

  On improving accountability, the EU head of delegation advised the government to strengthen the oversight organs such as parliamentary committees and media as a way of enabling the community understand well what the government was doing.

  Opening the meeting, Mr Mkulo said the government would continue to improve and use GBS because it was the appropriate system of assisting the government Budget.

  TANZANIA: Donors fault govt on Budget spending
   
 17. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah! Napita tuuuuuuuuuuuuuu
   
 18. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kufurahia ahadi hewa za wazungu.wazungu ni wazugaji kama hujui.fedha hizi walizo ahadi hazita kuja wakati zinahitajika,kama ni mbolea wataleta wakati watu wanavuna,kama ni vitabu wataleta vya shek spear,kifufi yatupasa kutegemea kodi za watanzania kuliko kuwategemea hao.mimi niliacha kutegemea ahadi zamaniiiii.
   
 19. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tume ya Katiba!
  Usishabikie kitu cha kipuuzi hizo ni sawa na Dola za kimarekani milioni 500 na wewe Kama Zuzu una furaha kama Kenge! Je umeshawahi kutumia akili yako ya kuvuka barabara ya Ali Hassan Mwnyi pale Namanga na kujiuliza migodi ya dhahabu ya African Barrick Gold wanauza dhahabu ya Dola ngapi kwa mwaka!

  Kweli Baba aw Taifa Mwalimu Nyerere aliyasema haya. Anakuja Mzungu na vipande vya chupa na kukuambia uliyo nayo sio almasi na anakubadilishia yeye anazichukua almasi wewe unabaki na chupa halafu unacheka Kama Zuzu? That what hao unaowaita wafadhili wanachokifanya and you stupid people mnacheza mdundiko na mdumange usiku kucha mkisherehekea mambo ya kipuuzi. Angalia ripoti ya mapato na matumizi ya hawa machizi wa CCM; Waziri wa fedha anapewa unlimited discretion kusamehe hata wapenzi wake kodi bila kuhojiwa na Mtu kwa mfano alisamehe kodi ya 1.2 Trillion na wafadhili wakatoa 1.6Trillion. Sasa kama sio ukichaa ni nini? It's simple algebra: Hakuna msamaha sio Balozi na sio Kanisa tukatae misaada lakini Kila mtu alipe kodi pronto! Huu uchizi aw kuwasamehe hao mnaowaita wawekezaji kutokulipa kodi ni zaidi ya Laana. Watanganyika ndiyo wapuuzi kuliko watu wote duniani just go to Nairobi Wakenya hawalii njaa Kama sisi. In fact it's a big shame kwa mtu mwenye umri aw miaka 50 kuwa omba omba. Kikwete aache Kama alivyoacha kunyonya Tabia ya kuzunguka duniani akiomba.
   
 20. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Watazila CCM zote kama zile za wabunge vijana na majumba ya 700,000 US$
   
Loading...