Neema Arusha; RC Gambo kukabidhi pikipiki 200 tarehe 10 Disemba, 2016

Jim007 2

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
395
247
RC Gambo kukabidhi pikipiki 200 - Jumamosi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.

Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.

Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.

Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.

Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.

Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.

Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:

Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.

Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wote Mnakaribishwa kushuhudia Tukio hili la Kihistoria.

2db004e086910c499ff902e32a70536b.jpg
 
Hii imekaa vizuri. Ajira hiyo. Pikipiki mpya. Garantii miezi 6, dahh, sasa kazi kwao.

Hili linasaidia watu, hasa vijana kujikwamua kiuchumi.
 
Hivi Bodaboda ni neema? Aibu sana hii nchi badala ya kutuliza akili na kufufua viwanda tuwapatie vijana wetu Ajira salama na zenye hadhi tunakomaa na Bodaboda vijana wanavunjika na kufa kila kukicha na ubunifu ndio umeishia hapo
 
RC Gambo kukabidhi pikipiki 200 - Jumamosi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.

Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.

Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.

Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.

Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.

Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.

Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:

Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.

Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wote Mnakaribishwa kushuhudia Tukio hili la Kihistoria.

2db004e086910c499ff902e32a70536b.jpg

Naipenda Arusha sana, machalii wa Mbauda, ,Morombo, Unga Ltd, Ngaramton, Majengo, Sakina, Sanawari n.k n.k!!! Ni fursa pekee ya kwenda kuchukua boda zenu. Wito wangu kwenu, mumtangulize MUNGU mbele. Nguvu inayotumika kupambana na upinzani ni kubwa sana! Baada ya kujihakikishia kuwa mbunge wenu hayupo mtaani, tunaangalia namna ya kuwasahaulisha habari za mbunge wenu kipenzi. Namna pekee ya kuwasahaulisha ni kucheza na matukio yatakayodumu muda mrefu! This is "creativity". Asante sana RC, Arusha itakukubali kama masahi mteule wa Arusha. Dar tayari wana mungu wao, tunataka walau kila mkoa uwe na mungu wake, ili kuweza kuharakisha maendeleo yetu, kuna watu wanatuchelewesha sana. Naona kwa mbali kila mkoa unaanza kupata ka-sir god
 
Hii ndiyo neema ya kuichagua CHADEMA,walioichagua CCM hawajapa mkupo kama huu,CCM wanapohangaika kutoa mikopo kama hii kwenye majimbo yanayoshikiliwa na wapinzani wakiamini kuwa wanawahonga wananchi ili waje wawachague wanaofaidika ni wananchi na wataendelea kuwaamini wapinzani kwa kuwachagua ili CCM wanapokazana kumwaga misaada kwa lengo la kuyatwaa tena maeneo hayo,wananchi wazidi kufaidika zaidi na zaidi.
 
Back
Top Bottom