Neema Arusha; RC Gambo kukabidhi pikipiki 200 tarehe 10 Disemba, 2016

Yani boda boda ndio neema...?
Watu wanakatika miguu nyie mnaita neema?
Gambo hili jimbo hutalipata kirahisi
 
1481264013742.jpg
 
RC Gambo kukabidhi pikipiki 200 - Jumamosi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.

Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.

Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.

Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.

Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.

Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.

Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:

Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.

Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wote Mnakaribishwa kushuhudia Tukio hili la Kihistoria.

2db004e086910c499ff902e32a70536b.jpg
Zitatumika kwenye Mapokezi ya Mfalme Lema na Zitakuwa Msaada sana kwenye Operation Kata Funua
 
Kumdanganya aliye elimika na kukomaa kisiasa na kiuchumi ni kazi!;Lumumba hiyo kick ishastukiwa na machalii,
 
Vijana wanao jua nini maana ya fursa
Hawata fuata upumbavu wa wanasiasa uchwara
 
Nawaonea huruma maccm hivi nayohii Mbinu et ee!
Machadema bana! Vijana wanapatiwa uwezo wa kujiajiri, nyie mnataka waendelee kunyweshwa viroba na Lema na kubaki wakiandamana bila hata kujua kwa njnj wanaandamana! Nyie hamna nia ya kuleta maendeleo bali fujo na vurugu na ufisadi tu.
 
Hivi Bodaboda ni neema? Aibu sana hii nchi badala ya kutuliza akili na kufufua viwanda tuwapatie vijana wetu Ajira salama na zenye hadhi tunakomaa na Bodaboda vijana wanavunjika na kufa kila kukicha na ubunifu ndio umeishia hapo
Wapinzani Akili zenu sawa na za Ng'ombe, hata hamueleweki huwa mnataka nini, kila kitu kwenu ni kibaya tu.!
 
Wapinzani Akili zenu sawa na za Ng'ombe, hata hamueleweki huwa mnataka nini, kila kitu kwenu ni kibaya tu.!
Akili za Ng'ombe ndio kama zako uende kwenye hizo Ajira za kuendesha Bodaboda.
Vijana wa nchi hii wanastahili ajira bora kuliko hizo za kuendesha Bodaboda. Geuzeni nchi kuwa ya viwanda watu wapate Ajira zenye hadhi na heshima, na hata wewe utaachana na kazi ya buku Saba hapo Lumumba ukawe mpigwa grisi kwenye kiwanda
 
Mafisadi chadema hawawezi na hawatakaa waweze kufifisha hamu ya jembe Gambo kuwatumikia wana arusha
Hivi na nyie tunatakiwa twende wote kwenye nchi ya viwanda? Ama kweli kwenye msafara wa mamba na mijusi wamo
 
Heheheheee wazilete tu bt wanatufanya tuwe na ajira ila kama ni Hongo wasahau 2020 ni#lema tena
 
Pikipiki mia mbili zitatoshereza machalii wote wa Atown??
Mtoeni Lema ndani maana hakuna sababu ya kumdharirisha.
Mnazidi kujenga chuki kwa wana Arusha.
Mamoderator wacha kunizibia mada za maana kuchangia, tuwe huru!!
 
Back
Top Bottom