Neema Akeyo alivyolipwa mshahara wake na NMB Plc baada ya kufukuzwa kazi kwa kutohudhuria kazini siku ya Jumamosi

Sawa kabisa. Sasa kuna zile kazi ambazo ni mandatory, mfano manesi, Madaktari, nk,
Hakuna mtu anaye ingilia imani ya mtu.
Cha msingi, unaongea kwa unyenyekevu na Bosi wako, anafanya arrangement kwamba siku yako ya ibada anapangwa mtu mwingine.
Siyo unajiamulia tu unaingia mitini kisa, wewe Msabato! Na mbaya sana watu fulani hutumia sababu hiyo kwa uwongo mtupu, kumbe alikuwa ameenda kufanya mambo yake!
Mambo ya imani bwana yako very complicated na ukiamua kuyaendekeza sana kuna siku yanaweza kukutokea puani.
 
Kesi ya Neema Akeyo vs- National Microfinance Bank- NMB

HOJA:-
  • HAKI YA KUABUDU SIKU YA SABATO
  • Kuachishwa kazi kutokana na utoro (siku ya Jumamosi kwa muumini mwadventista) na utovu wa nidhamu
  • Ubaguzi wa kutokana na dini/imani ya mtu

Tarehe 01/11/2010 Neema Akeyo aliajiriwa katika Benki ya NMB Arusha kwa nafasi ya Bank Teller hadi alipoachishwa kazi tarehe 05/06/2014 kwa makosa mawili

1. Utoro/absenteeism.
2. Utovu wa nidhamu/insubordination.

Kinyume na NMB Human Resource Manual Policy 2013, Staff Rules, na NMB Code of Good Practice.

Neema hakuridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi hivyo aliwasilisha madai yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi- (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) Arusha akipinga uhalali wa kusitishiwa ajira yake na kudai kwamba USITISHWAJI WA AJIRA ULIKUWA BATILI KWANI HAUKUTOKANA NA SABABU ZA MSINGI, NA HAUKUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHERIA. Katika hatua zote Neema alikuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi Asubuhi Yoyo.

Uamuzi wa TUME- CMA

Hatimaye tarehe 05/08/2015 kupitia Mhe. Lomayan Stephano- Muamuzi Tume iliamua kwamba usitishwaji kazi ulikuwa batili kwani NMB hakuwa na sababu za msingi wala hakuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria kabla ya kumwachisha kazi Neema Akeyo.

Tume iliamuru NMB kumlipa NEEMA fidia ya mishahara ya miezi 36 kutokana na usitishaji kazi kutokana na ubaguzi wa kidini kwani Neema alinyimwa haki ya kuabudu siku ya Jumamosi kinyume na Katiba ya JMT na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kazi - (High Court Labour Division)-HCLD @ Arusha

Baada ya Uamuzi/Tuzo ya Tume NMB hakuridhika hivyo aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama kuu kitengo cha Kazi, na hatimaye tarehe 02/06/2017 kupitia Mhe. Jaji Aisha Nyerere (kama alivyokuwa) Mahakama ilitupilia mbali /dismiss hoja zote za marejeo zilizowasilishwa na NMB, na Mahakama ilithibitisha/confirm Tuzo/Uamuzi wa CMA kwamba usitishaji kazi dhidi ya Neema Akeyo haukuwa halali.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa/ Court of Appeal of Tanzania- CAT iliyoketi Arusha

Baada ya kutoridhishwa tena na Hukumu ya Mahakama Kuu, NMB waliwasilisha Rufaa yao katika Mahakama ya Juu kabisa nchini kuiomba itengue Hukumu ile, na baada ya kusikilizwa kikamilifu tarehe 21/02/2022 Mahakama ilitoa Hukumu yake kupitia waheshimiwa Majaji watatu Mhe. MUGASHA, Mhe. SEHEL, na Mhe. KAIRO ambapo hoja zote za NMB zilitupiliwa mbali na Mahakama ilithibitisha Hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi, na Uamuzi wa Tume.

Hukumu hii ni Muhimu kwani imegusa eneo ambalo limekuwa likileta changamoto kwa waumini mara nyingi hususan waumini Waadventista Wasabato.
  • Haki ya kuabudu
  • Uhuru wa kuabudu
  • Ubaguzi kutokana na dini/imani ya mtu
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii. 🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Liked
 
Hii kesi nilisikia miaka iliyopita..huyu dada nadhani ni yule mwimbaji ya kwaya ya sabato SDA kurasini..kapambana miaka yote hiyo now imefika hitimisho .so kwa kwa hiyo miaka yote Ni dhahiri atavuta pesa ndefu..waajiri makini haya Mambo huwa wanamaliza mapema hata isingefika huko. Haki ya kuabudiwa kwa kila Imani lazima iheshimiwe.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wakili wa Nmb kawaingiza Chaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi ya Neema Akeyo vs- National Microfinance Bank- NMB

HOJA:-
  • HAKI YA KUABUDU SIKU YA SABATO
  • Kuachishwa kazi kutokana na utoro (siku ya Jumamosi kwa muumini mwadventista) na utovu wa nidhamu
  • Ubaguzi wa kutokana na dini/imani ya mtu

Tarehe 01/11/2010 Neema Akeyo aliajiriwa katika Benki ya NMB Arusha kwa nafasi ya Bank Teller hadi alipoachishwa kazi tarehe 05/06/2014 kwa makosa mawili

1. Utoro/absenteeism.
2. Utovu wa nidhamu/insubordination.

Kinyume na NMB Human Resource Manual Policy 2013, Staff Rules, na NMB Code of Good Practice.

Neema hakuridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi hivyo aliwasilisha madai yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi- (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) Arusha akipinga uhalali wa kusitishiwa ajira yake na kudai kwamba USITISHWAJI WA AJIRA ULIKUWA BATILI KWANI HAUKUTOKANA NA SABABU ZA MSINGI, NA HAUKUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHERIA. Katika hatua zote Neema alikuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi Asubuhi Yoyo.

Uamuzi wa TUME- CMA

Hatimaye tarehe 05/08/2015 kupitia Mhe. Lomayan Stephano- Muamuzi Tume iliamua kwamba usitishwaji kazi ulikuwa batili kwani NMB hakuwa na sababu za msingi wala hakuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria kabla ya kumwachisha kazi Neema Akeyo.

Tume iliamuru NMB kumlipa NEEMA fidia ya mishahara ya miezi 36 kutokana na usitishaji kazi kutokana na ubaguzi wa kidini kwani Neema alinyimwa haki ya kuabudu siku ya Jumamosi kinyume na Katiba ya JMT na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kazi - (High Court Labour Division)-HCLD @ Arusha

Baada ya Uamuzi/Tuzo ya Tume NMB hakuridhika hivyo aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama kuu kitengo cha Kazi, na hatimaye tarehe 02/06/2017 kupitia Mhe. Jaji Aisha Nyerere (kama alivyokuwa) Mahakama ilitupilia mbali /dismiss hoja zote za marejeo zilizowasilishwa na NMB, na Mahakama ilithibitisha/confirm Tuzo/Uamuzi wa CMA kwamba usitishaji kazi dhidi ya Neema Akeyo haukuwa halali.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa/ Court of Appeal of Tanzania- CAT iliyoketi Arusha

Baada ya kutoridhishwa tena na Hukumu ya Mahakama Kuu, NMB waliwasilisha Rufaa yao katika Mahakama ya Juu kabisa nchini kuiomba itengue Hukumu ile, na baada ya kusikilizwa kikamilifu tarehe 21/02/2022 Mahakama ilitoa Hukumu yake kupitia waheshimiwa Majaji watatu Mhe. MUGASHA, Mhe. SEHEL, na Mhe. KAIRO ambapo hoja zote za NMB zilitupiliwa mbali na Mahakama ilithibitisha Hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi, na Uamuzi wa Tume.

Hukumu hii ni Muhimu kwani imegusa eneo ambalo limekuwa likileta changamoto kwa waumini mara nyingi hususan waumini Waadventista Wasabato.
  • Haki ya kuabudu
  • Uhuru wa kuabudu
  • Ubaguzi kutokana na dini/imani ya mtu
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii. 🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Haya mambo yatatuchelewesha sana Wa Africa yani, haswa Tanzania.
Huyo Mungu mwenyewe anatutaka tufanye Kazi.

Sasa huyu yeye anataka kuwa zaidi ya Yesu
 
Wale wazee wa blue Monday dini yenu muisajili tu na kuanza kuabudu jumatatu. Na imani yenu ikataze kufanya kazi siku ya jumatatu 🤣🤣🤣
 
Delay mechanism ya taasisi Vs Njaa ya mlalamikaji (2022-2014=8 years) bado gharama za mawakili.
Njaa au haki ya mlalamikaji? WaTz tunapuuzia kila kitu hata vya msingi, na hapo ndio wenye mamkaka wanatuibia haswa.
 
Utaparangana miaka 8 kudai tumilioni twa mboga? Hapo umlipe Mwanasheria? Hapo Huna kazi
 
Ujinga tu, na wa Islam ijumaa nao waabudu
Mimi si Muislam lakini niliwahi kusikia kuwa dini yao inasema baada ya Swala Ijumaa watu wanaweza kurudi kwenye majukumu yao. All in all Waislamu huwa hawana complications hasa kwa mambo ambayo hayaoneshi kuutweza Uislamu
 
Kesi ya Neema Akeyo vs- National Microfinance Bank- NMB

HOJA:-
  • HAKI YA KUABUDU SIKU YA SABATO
  • Kuachishwa kazi kutokana na utoro (siku ya Jumamosi kwa muumini mwadventista) na utovu wa nidhamu
  • Ubaguzi wa kutokana na dini/imani ya mtu

Tarehe 01/11/2010 Neema Akeyo aliajiriwa katika Benki ya NMB Arusha kwa nafasi ya Bank Teller hadi alipoachishwa kazi tarehe 05/06/2014 kwa makosa mawili

1. Utoro/absenteeism.
2. Utovu wa nidhamu/insubordination.

Kinyume na NMB Human Resource Manual Policy 2013, Staff Rules, na NMB Code of Good Practice.

Neema hakuridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi hivyo aliwasilisha madai yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi- (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) Arusha akipinga uhalali wa kusitishiwa ajira yake na kudai kwamba USITISHWAJI WA AJIRA ULIKUWA BATILI KWANI HAUKUTOKANA NA SABABU ZA MSINGI, NA HAUKUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHERIA. Katika hatua zote Neema alikuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi Asubuhi Yoyo.

Uamuzi wa TUME- CMA

Hatimaye tarehe 05/08/2015 kupitia Mhe. Lomayan Stephano- Muamuzi Tume iliamua kwamba usitishwaji kazi ulikuwa batili kwani NMB hakuwa na sababu za msingi wala hakuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria kabla ya kumwachisha kazi Neema Akeyo.

Tume iliamuru NMB kumlipa NEEMA fidia ya mishahara ya miezi 36 kutokana na usitishaji kazi kutokana na ubaguzi wa kidini kwani Neema alinyimwa haki ya kuabudu siku ya Jumamosi kinyume na Katiba ya JMT na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kazi - (High Court Labour Division)-HCLD @ Arusha

Baada ya Uamuzi/Tuzo ya Tume NMB hakuridhika hivyo aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama kuu kitengo cha Kazi, na hatimaye tarehe 02/06/2017 kupitia Mhe. Jaji Aisha Nyerere (kama alivyokuwa) Mahakama ilitupilia mbali /dismiss hoja zote za marejeo zilizowasilishwa na NMB, na Mahakama ilithibitisha/confirm Tuzo/Uamuzi wa CMA kwamba usitishaji kazi dhidi ya Neema Akeyo haukuwa halali.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa/ Court of Appeal of Tanzania- CAT iliyoketi Arusha

Baada ya kutoridhishwa tena na Hukumu ya Mahakama Kuu, NMB waliwasilisha Rufaa yao katika Mahakama ya Juu kabisa nchini kuiomba itengue Hukumu ile, na baada ya kusikilizwa kikamilifu tarehe 21/02/2022 Mahakama ilitoa Hukumu yake kupitia waheshimiwa Majaji watatu Mhe. MUGASHA, Mhe. SEHEL, na Mhe. KAIRO ambapo hoja zote za NMB zilitupiliwa mbali na Mahakama ilithibitisha Hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi, na Uamuzi wa Tume.

Hukumu hii ni Muhimu kwani imegusa eneo ambalo limekuwa likileta changamoto kwa waumini mara nyingi hususan waumini Waadventista Wasabato.
  • Haki ya kuabudu
  • Uhuru wa kuabudu
  • Ubaguzi kutokana na dini/imani ya mtu
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii. 🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Kwaio mkuu vipi? Atalipwa mshahara hadi 2022? Kwa maana inaonekana hakulipwa kokote kule
 
Wasabato wana maisha magumu sana.

Nakumbuka nilikuwa nawatembelea ndugu zangu fulani wakati niko shule

Chakula kinapikwa ijumaa mchana kinaliwa hadi jumamosi jioni

Jumamosi hawapiki kitu mnakuoa kiporo na chai ya jana

Maisha yao ni magumu kwakweli
 
Kwa hiyo waislamu ijumaa nao waende masjid!
Waislam kila siku tuna abudu, maisha yote ya Muislam ni ibada. Mara tano kwa siku tunaenda Masjidkufanya ibada mojawa[po au zaidi na tunachapa kazi kama kawaida.

Ijumaa sio siku ya mapumziko kwa Waislaam, ni siku ya kukutana Jamaa. Ukitaka usitake Muislaam mwanamme mwenye uwezo wa kutembea unatakiwa uende msikiti wa karibu yako, ukajumuike na wengine na msali pamoja na Imam atoe hotuba (khutba) aelezee ya muhimu kwa jamii inayowazunguka na mkubushane mema na mkatazane mabya.
 
Back
Top Bottom