Neema Akeyo alivyolipwa mshahara wake na NMB Plc baada ya kufukuzwa kazi kwa kutohudhuria kazini siku ya Jumamosi

Kesi ya Neema Akeyo vs- National Microfinance Bank- NMB

HOJA:-
  • HAKI YA KUABUDU SIKU YA SABATO
  • Kuachishwa kazi kutokana na utoro (siku ya Jumamosi kwa muumini mwadventista) na utovu wa nidhamu
  • Ubaguzi wa kutokana na dini/imani ya mtu

Tarehe 01/11/2010 Neema Akeyo aliajiriwa katika Benki ya NMB Arusha kwa nafasi ya Bank Teller hadi alipoachishwa kazi tarehe 05/06/2014 kwa makosa mawili

1. Utoro/absenteeism.
2. Utovu wa nidhamu/insubordination.

Kinyume na NMB Human Resource Manual Policy 2013, Staff Rules, na NMB Code of Good Practice.

Neema hakuridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi hivyo aliwasilisha madai yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi- (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) Arusha akipinga uhalali wa kusitishiwa ajira yake na kudai kwamba USITISHWAJI WA AJIRA ULIKUWA BATILI KWANI HAUKUTOKANA NA SABABU ZA MSINGI, NA HAUKUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHERIA. Katika hatua zote Neema alikuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi Asubuhi Yoyo.

Uamuzi wa TUME- CMA

Hatimaye tarehe 05/08/2015 kupitia Mhe. Lomayan Stephano- Muamuzi Tume iliamua kwamba usitishwaji kazi ulikuwa batili kwani NMB hakuwa na sababu za msingi wala hakuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria kabla ya kumwachisha kazi Neema Akeyo.

Tume iliamuru NMB kumlipa NEEMA fidia ya mishahara ya miezi 36 kutokana na usitishaji kazi kutokana na ubaguzi wa kidini kwani Neema alinyimwa haki ya kuabudu siku ya Jumamosi kinyume na Katiba ya JMT na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kazi - (High Court Labour Division)-HCLD @ Arusha

Baada ya Uamuzi/Tuzo ya Tume NMB hakuridhika hivyo aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama kuu kitengo cha Kazi, na hatimaye tarehe 02/06/2017 kupitia Mhe. Jaji Aisha Nyerere (kama alivyokuwa) Mahakama ilitupilia mbali /dismiss hoja zote za marejeo zilizowasilishwa na NMB, na Mahakama ilithibitisha/confirm Tuzo/Uamuzi wa CMA kwamba usitishaji kazi dhidi ya Neema Akeyo haukuwa halali.

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa/ Court of Appeal of Tanzania- CAT iliyoketi Arusha

Baada ya kutoridhishwa tena na Hukumu ya Mahakama Kuu, NMB waliwasilisha Rufaa yao katika Mahakama ya Juu kabisa nchini kuiomba itengue Hukumu ile, na baada ya kusikilizwa kikamilifu tarehe 21/02/2022 Mahakama ilitoa Hukumu yake kupitia waheshimiwa Majaji watatu Mhe. MUGASHA, Mhe. SEHEL, na Mhe. KAIRO ambapo hoja zote za NMB zilitupiliwa mbali na Mahakama ilithibitisha Hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi, na Uamuzi wa Tume.

Hukumu hii ni Muhimu kwani imegusa eneo ambalo limekuwa likileta changamoto kwa waumini mara nyingi hususan waumini Waadventista Wasabato.
  • Haki ya kuabudu
  • Uhuru wa kuabudu
  • Ubaguzi kutokana na dini/imani ya mtu
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii. 🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Ilikuwa sahihi kufukuzwa kazi, yaani wateja tusihudumiwe kisa eti yeye kaenda kushabikia dini isiyomuhusu. Huyu kajitakia mwenyewe.
 
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii.

Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Hii itasaidia, mana NMB hata jumapili nowadays wanafungua matawi....waache watu wapumzike waende kuabudu...maisha sio kazi tu ..
 
Hii itasababisha wasabato wale ban hapo nmb….Na taasisi nyingine kuwaogopa dah hatari sana..Bora angepiga kimya
 
Back
Top Bottom