NECTA yatangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2017. Shule kanda ya Ziwa zang'aa

mod rekebisha mikoa iliyofanya vibaya, Tabora haiko ktk kundi la mikoa iliyofanya vibaya bali iko ktk kumi bora ya mikoa iliyofanya vyema!
 
Kwenda secondary ni kwa wenye A na B. Wenye C labda waende VETA au waitwe awamu ya pili kujaza mapengo shule za kata
Ikiwa hivo shule za kata zitakosa wanafunzi angalia st kayumba karibia wote wana wastan wa c
 
Kagera,Kilimanjaro na Mbeya


Kagera,Kilimanjaro na Mbeya


Kagera,Kilimanjaro na Mbeya


Kila wakati sifa zilimwagika kwao kwa elimu na utoaji viongozi wenye elimu.


Je miaka 10 ijayo nini hatma ya Kagera na Mbeya maana ni kama zinazidi kupotea na watani zao kielimu Kilimanjaro wanachanja mbuga?

Na ni nini sababu za kushuka kielimu katika kufaulisha watoto wetu?


Ni kifanyike ili wabaki katika ubora wao?



Inasikitisha Ila ndio ukweli nawaona Kagera na Mbeya mnavyotupungia mkono.
 
Mkuu yawezekana ile mikakati iliyowafanya wafaulishe wameiondoa?

Au hawajai update kulingana na kizazi cha sasa?
Huenda kuna mahali wanakosea au wanajisahau..

Pia hiyo mikakati haijatiliwa mkazo kuendana na hali ya sasa ukizingatia kuna ushindani kielimu
 
Hao wa kagera wakisoma, ule mtaa wa wahaya utakosa watu. Na sisi tunaopata huduma kutoka kwao tutateseka.
 
Mikoa iliyofanya vibaya kwa mujibu wa necta ni mikoa ya Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi, Manyara

Na ile iliyoongoza kwa kutusua kwenye mtihani huo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kagera,Geita,Njombe,Iringa,na Katavi
Singida ni ya mwisho kitaifa.Shule ya mwisho kitaifa pia ipo Singida.Wadau wa elimu ni bora kuitembelea shule hii kufahamu ina matatizo gani na ipo katika mazingira gani?
 
Kagera shule NNE zimeingia top ten kutoka mkoa mmoja, hahahaaaa huu mkoa ni balaa pongezi kwao.
 
Wamewahisha kuyatoa afadhali, maana kipindi cha nyuma walikuwa wanayatoa wakati wa sikukuu ya krismasi
Now mitihani inasahishwa na machine inaitwa OMR ndoo maana mitihani yao yote ni kuchagua tuu, huu umeua elimu sana mm kama mwlm nikilinganisha na mfumo uliokuwepo wa zamani. Now kila mtoto ana uwezo wa kufaulu ili ajaze Shula za Kata ila ss huwa tunajua wakufika mbali ni wachache tunajua wengi wao watarudi kuuza machungwa mtaani.
Elimu wameipeleka kisiasa mnoo kwa ajili ya kuwakomoa watoto wa maskni ila ss tunaofundisha tunaona huruma sana ila hatuna jinsi tunasema bora liende Mzaz atajuana na mwanae. Leo hii wanasema elim bure ni bora wangewaacha wazaz wakaendelea na michango yao ili watoto wao angalau wapate kinachostaiili. Walianza kwa kumpa mwanafunzi mmoja 550 kwa Lila mwez sasahv imeshuka mpaka 400 kwa mwezi, serikali imeishalemewa ila haitaki kusema ili kusaidiwa
 
Back
Top Bottom