NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne na cha pili 2020

Evans Richard Arsenal

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
365
750
NECTA wameandika matokeo ya Kidato cha nne na Upimaji wa kidato cha cha Pili na Darasa la Nne 2021, yatatangazwa hivi punde kaa tayari ndio mida hii.

All the best Comrades, see you at the top.

===

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yakionyesha kuwa asilimia 85 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Kwa mujibu wa Necta iliyotangaza matokeo hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 kupitia kwa katibu mtendaji wake, Dk Charles Msonde, watahiniwa 434,654 walifanya mtihani huo na 373, 958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali. Dk Msonde amesema kwa matokeo hayo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 5.19.

Katika mtihani huo Paul Luziga wa sekondari ya Pandahill iliyoko Mbeya amekuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa.

Orodha ya walioongoza kitaifa kidato cha nne

1. Paul Luziga - Panda Hill
2. Justina Gerald - Canossa.
3. Timothy Segu - Mzumbe
4. Isaya Rukamya - Feza Boys
5. Ashraf Ally - Ilboru
6. Samson Mwakabage - Jude
7. Derick Mushi - Ilboru
8. Layla Atokwete - Canossa
9. Innocent Joseph - Mzumbe
10. Lunargrace Celestine - Canossa.


Shule bora kitaifa ni St Francis Girls Secondary School kutoka MBEYA.

Mikoa 3 iliyofanya vizuri:
Dar es Salaam
Lindi
Arusha

Link ya matokeo kamili
emoji116.png


https://matokeo.necta.go.tz/csee2020/csee.htm

=====

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020: NECTA YASEMA UFAULU UMEONGEZEKA KWA 5.19%

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde, amesema Watahiniwa wa Shule 373,958 (85.84%) kati ya 434,654 waliofanya Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne 2020 wamefaulu

Ameeleza kuwa, idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 5.19 ikilinganishwa na matokeo ya Mitihani ya mwaka 2019 ambapo Watahiniwa waliofaulu walikuwa 340,914 (80.65%)

Amesema Wasichana 193, 672 sawa na 85.44% wamefaulu Mitihani hiyo huku Wavulana wakiwa 182,086 sawa na 86.27%. Watahiniwa wapatao 490,213 walisajiliwa kufanya Mitihani hiyo
 
Baraza la mitihani la taifa (NECTA).
Leo Tarehe 15-01-2021 litatangaza matokeo ya kidato cha pili, nne na darasa la nne ya mwaka 2020/2021
 
Mkuu Emmanuel Kasomi, Baraza la Mitihani lajulikana kama NECTA na si NACTE. Afadhali waliofanya mitihani mwaka jana wajue kama wanaendelea na kidato cha tatu au wanarudia kidato cha pili mwaka huu. Kila la heri kwa wahusika wote!
 
Back
Top Bottom