NECTA yatangaza matokeo ya Kidato cha 6 - 2021. Ufaulu waongezeka kwa 0.19%

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,451
29,128
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde anatangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu iliyofanyika Mei 2021.

Ameeleza kuwa ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 0.11 ikilinganishwa na mwaka 2020.

Dkt Msonde amesema hayo leo visiwani Zanzibar na kuongeza kuwa ubora wa ufaulu umeimarika kwa asilimia 0.19 kutoka asilimia 97.74 mwaka 2020 hadi asilimia 97.93 mwaka huu.
 
Sikuhizi ukifel o levo na alevo..kweli wewe ni kilaza wa mwisho..elimu imekua ya kisiasa hakuna tena ubora.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna dogo kanambia kapiga one ya nane nikasema ngoja nichek shule yao wamepataje nakuta one mia na uchafu nikaishiwa nguvu maana shule yenyewe ni hz za ovyo tu so kupata one mia zote hzo ni maajabu.
 
Kuna dogo kanambia kapiga one ya nane nikasema ngoja nichek shule yao wamepataje nakuta one mia na uchafu nikaishiwa nguvu maana shule yenyewe ni hz za ovyo tu so kupata one mia zote hzo ni maajabu.
Sasa kwA hgk kushinda kupata one si ni ukichaa huo,!
 
Back
Top Bottom