NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
NECTA imetangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2019 na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanya udanganyifu
*****

Baraza la Mtihani la Taifa (Necta) limesema katika Mtihani wa Darasa la saba uliofanyika Septemba 11, 2019 wamebaini walimu Wakuu, Wasimamizi na walinzi walihusika kufanya udanganyifu

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba na kueleza kuwa katika kikao kilichokaa leo tayari wameshazitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie hatua waliohusika na udanganyifu huo. Ambapo kwa sasa udanganyifu kwa ujumla umepungua ambapo mwaka 2011 ulikuwa 9,736 na mwaka huu umefikia 900.

Amesema kuwa katika matokeo hayo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu, matokeo ya jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asilikia 3.78.

"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.

Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.

Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.

Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.

Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.

Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha.
 
Inalea ujumbe huo
Screenshot_20191015-121348.jpeg
 
Tulizoea ufaulu wa watoto wawili au watano kwenye shule kwenda sekondari le mnatuambia asilimia hizo??? Je wasiojua kusoma na kuandika ni wangapi na mtawajuaje ikiwa tumeambiwa mpaka F. 5 wapo wasiojua kusoma na kuandika? Sawa hiyo? haaaaata.
 
Back
Top Bottom