NECTA yatangaza matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne 2021

kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,271
2,000
Salaam!

Baraza la Mitihani ya Kitaifa linajiandaa kutangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ulifanyika mwishoni mwa mwaka 2021 (CSEE).

Pamoja na Mtihani wa Upimaji kidato cha Pili (FTNA).

Wahitimu wote mkae mkao wa kuvuna kile mlichopanda.

Source: NECTA news
  1. Piga *152*00#
  2. Chagua namba 8. ELIMU
  3. Chagua namba 2. NECTA
  4. Chagua aina ya huduma 1. MATOKEO
  5. Chagua aina ya Mtihani 1. CSEE (kwa kidato cha Nne)
  6. Andika namba ya Mtihani na Mwaka Mfano:S0334-0556-2021
  7. Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa kila SMS ni Tshs 100/=)
  8. Baada ya kukamilisha malipo utapokea ujumbe mfupi wa matokeo.
Kupata Matokeo ya Kidato cha Nne.
Bonyeza Link

www.necta.go.tz

PSX_20220115_112013.jpg

Wanafunzi kumi (10) bora kitaifa kwa mwaka 2021/2022 ni kama ifuatavyo;

1. Consolata Prosper Lubuva - St. Francis
2. Bhutoi Ernest Nkaganza - St. Francis
3. Wilihelmina Steven Mijarifu - St. Francis
4. Glory John Mbele - St. Francis
5. Mary George Ngoso - St. Francis
6. Holly Beda Lyimo - Bright Future Girls
7. Blandina Karen Chiwawa - St. Francis
8. Imam Suleiman - Feza Boys
9. Mfaume Hamisi Madili - Iliboru
10. Clara Straton Assenga - St. Francis
 

shinji

JF-Expert Member
Aug 31, 2013
234
250
Acha kupotosha, hakuna taarifa hadi muda ninapoandika ujumbe huu kwenye tovuti wala kurasa rasmi za NECTA kwenye mitandao ya kijamii
 

kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,271
2,000
Acha kupotosha, hakuna taarifa hadi muda ninapoandika ujumbe huu kwenye tovuti wala kurasa rasmi za NECTA kwenye mitandao ya kijamii
Unataka tubet?

Wasipoyatanga leo basi ni Jumatatu Mapema sana.
 

kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,271
2,000
Jumatatu tena? Kumbe unabahatisha tu? Matokeo ya CSEE, FTNA na SFNA 2021 lazima yatoke sooner or later. Hilo liko wazi.
Sooner or later maana yake ni nini.

Nikisema leo au Jumatatu?

Msonde lazima aangalie upepo.

Ashauriane na Prof. Mkenda then wayalipue.

Yanalipuka muda si muda au punde si punde.
 

Maxmax72

Senior Member
Nov 6, 2018
144
250
Usipotoshe umma, maisha ya watu hayako kwenye mitihani hii ya kwenye makaratasi.

Pia usiogope utakuwa umefanya vizuri au hata kama hujafanya vizuri songa mbele.

Kuna maisha baada ya mtihani
Dogo kuanzia sasa tambua kuwa chuo ulichohitimu mimi nimefundisha.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,624
2,000
Hii kitu nikipewa Urais wa 24 hrs nitafutilia mbali,kila mtahiniwa atapata matokeo yake kwa njia ya simu au kuwasiliana na shule yake,tunavyofanya hivi hatujui matokeo mabaya ya kisaokolojia wanayoyapata watihaniwa,siri ya matokeo itakuwa kwa mhusika tu,why watu wote wajue mimi nimepata 0 div?au 1div?.
 

Bukondamoyo

JF-Expert Member
May 11, 2017
411
500
Baraza la Mitihani la Tanzania leo terehe 15/01/2022 linatarajia kutangaza Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Mtihani wa Kidato cha Nne 2022. Unaweza kutazama tukio hilo live kupitia youtube channel ya NECTA (Nectaonline) kuanzia Saa 4:00 asubuhi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom